LHRC wapinga tume ya JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LHRC wapinga tume ya JK

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 7, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  na Nasra Abdallah

  KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimepingana na utaratibu uliopendekezwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ule wa rais wa kuundwa kwa tume katika kushughulikia madai ya Katiba mpya.

  Mkurugenzi wa kituo hicho, Francis Kiwanga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa msimamo wa kituo hicho kuhusu Katiba, alisema wanapingana na utaratibu huo kwa kuwa kumbukumbu na uzoefu unaonyesha kuwa mara zote wananchi walipodai mabadiliko ya Katiba na serikali kuitikia kwa kuanzisha tume, maoni ya wananchi yamekuwa yakiwekwa pembeni na kupuuzwa.

  Akitolea mfano alisema tume ya Jaji Nyalali na hata ile ya Jaji Kisanga, zilifanya kazi ya kukusanya maoni na mapendekezo ya mabadiliko, lakini matokeo yake taarifa hizo hazikufanyiwa kazi kwa kiwango kinachostahili na kuleta mabadiliko ya maana ya kuboresha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa kuzingatia upungufu huo, kituo hicho kimetoa mapendekezo yao ikiwemo suala hilo kupelekwa bungeni kujadiliwa na kufanya mabadiliko madogo katika Katiba ya sasa na kuweka utaratibu wa kupata Katiba mpya.

  Pendekezo hilo linafanana na taarifa ya hoja binafsi inayokusudiwa kuwasilishwa bungeni na Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika kulitaka Bunge litoe mwongozo utakaowezesha kupatikana kwa Katiba mpya.

  Aidha, mapendekezo yao mengine ni kutaka mchakato wa kuandika Katiba mpya uanze kwa wananchi kuchagua wawakilishi watakaounda mkutano wa Katiba "constituency assembly" na kuongeza kuwa wajumbe hao wajumuishe wawakilishi wa wananchi, makundi maalumu kama ya dini, vyama vya siasa, asasi za raia na makundi mengine.

  Mkurugenzi huyo alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa mkutano huo wa Katiba ndio uandae rasimu ya Katiba ambayo itajadiliwa na wananchi na kuipigia kura ya maoni, yaani "referendum".

  Baada ya kura hiyo ya maoni, alisema ndipo utapatikana uhalali wa kuanza kutekelezwa kwa Katiba mpya.

  Awali Kiwanga alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ambayo imefanyiwa marekebisho mbalimbali takriban mara 14 tangu ilipoanza kutumika ina mabadiliko mengi ambayo yamefifisha kukubalika kwake kwa wananchi walio wengi.

  Alitaja baadhi ya upungufu huo ambao inabidi kubadilika kwa kutunga mpya baada ya mjadala mpana wa wananchi kuwa ni pamoja na muundo wa mfumo wa utawala ambao unaongeza nguvu ya Bunge ambalo lina uwakilishi mpana na waliopatikana kwa njia ya demokrasia.

  Pia alisema mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ambayo ni sehemu moja ya Muungano yanalazimisha mabadiliko katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Kuondoa nguvu ya kikatiba ya rais kuvunja Bunge, kwani Bunge limechaguliwa na wananchi, iweje rais awe na nguvu kubwa kuliko wananchi waliowachagua wabunge?

  "Kuweka idadi na muundo wa baraza la mawaziri na wizara za serikali na kupunguza madaraka ya rais ya kuteua wakuu wa idara nyeti na mihimili mingine ya dola bila kushirikisha Bunge, ambapo teuzi hizo ni lazima zipitie katika kamati za Bunge kwa uthibitisho kabla ya kukamilika," alisema.

  Katika upungufu huo, pia alisema ni vyema kukawekwa utaratibu wa ulinzi wa kikatiba wa usimamizi wa rasilimali za asili za taifa kama ardhi, madini, mafuta na rasilimali nyingine.

  Hata hivyo, alisema itakuwa busara pia endapo kutawekwa mabadiliko mengine ambayo wananchi wanadhani yanafaa kuwepo kwenye Katiba mpya.

  Kwa upande wake Wakili kutoka Shirika la Mtetezi, Rugemeleza Nshala, alisema kwa kuwa utaratibu huu unaweza kuwa wa gharama na unahitaji muda, ni vyema katika bajeti ya Julai mwaka huu ikaanza kuainisha gharama hizo.

  Nshala alisema wanaunga mkono hoja ya Profesa Shivji ya gharama zitakazotumiwa katika mchakato wa Katiba hiyo mpya zitoke katika Serikali ya Jamhuri ya Tanzania ili kuepuka uchakachuaji.

  Kuhusu suala la utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu kuijua kwanza Katiba ya zamani, wanaharakati hao walisema isitumiwe kama kigezo, kwani Watanzania si mbumbumbu kiasi hicho, ukizingatia kwamba kuna masuala mengine yapo wazi.

  Pamoja na wao kuwa na utaratibu wa kusoma Katiba mara kwa mara, walisema bado hawajajua mambo yote yaliyomo ndani ya Katiba.

  Naye mwanaharakati wa masuala ya Jamii, Hebron Mwakagenda, alisema ana matumaini makubwa Katiba hiyo mpya kupatikana lakini aliitaka serikali kusikiliza sauti za Watanzania wanataka nini wakati wa mchakato wa kuipata Katiba hiyo.

  Mwakagenda ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Citizen Information Bureau (TCIB) alisema kuwa ikiwa serikali itazingatia hayo itasaidia kuepuka kutokea kwa mambo yasiyo ya msingi.

  "Watanzania tutulie, tujipange kwa makundi yetu na kupanga mawazo yetu ili itakapotokea kwamba nasi tunajumuishwa tuwe tumejiandaa kutoa mawazo," alisema Mwakagenda wakati akuzungumza kupitia kituo cha televisheni cha ITV.

  Alisema nchi ya Kenya ilitumia miaka 20 hadi kuipata Katiba hiyo mpya na leo hii wameanza kufaidi matunda yake lakini Tanzania ni tofauti na nchi hiyo kwa mambo mengi, hivyo ikiwa kutakuwa na utulivu mchakato wa kuipata Katiba hiyo utakuwa ni wa muda mfupi tofauti na Kenya.

  Alisema wananchi wa Tanzania wanajua kwamba Katiba iliyopo haiwezi kuzuia ufisadi hivyo ikiwa nchi itatumia mtindo wa Kenya itasaidia hasa katika kuwawajibisha viongozi wanaokuwa wakifanya ufisadi.

  Alielezea pia hofu ya wananchi kuhusu tume itakayoundwa kushughulikia mchakato wa suala hilo na kuhoji iwapo itaweza kuwajibika kwa rais.

  Alisema katika kufuatilia kwa ukaribu kuhusu suala hilo, shirika lao limeandaa utaratibu wa kuzunguka nchi nzima kukiwamo Tanzania Zanzibar ili kukusanya maoni kuhusu Katiba hiyo na watafanya hivyo siku chache zijazo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Jk sasa amejifunza ya kuwa nchi hii ina wenyewe......................
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwani watawala wana-masikio?
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Katiba iliyopo imeachwa iendelee kuwa na matundu kwa makusudi! ...Aaaaah kweli CCM ni majambazi.
  Hii ina maana kwamba, katiba iliyopo haina ulinzi wa rasilimali za taifa. Can you imagine that????????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...