LHRC: Wabunge upinzani wafunika CCM; Makinda dhaifu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LHRC: Wabunge upinzani wafunika CCM; Makinda dhaifu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Apr 22, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Tathmini ya utendaji wa wabunge iliyofanywa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 10 uliomalizika wiki iliyopita, umeonyesha kuwa wabunge wa upinzani wameonyesha ufanisi mkubwa ikilinganishwa na wale wa chama tawala.

  Taarifa ya tathmini hiyo iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ambacho kilifanya kazi hiyo, inaonyesha kuwa wabunge wa upinzani wametoa mchango mkubwa wa kushiriki katika mijadala mbalimbali na kuuliza maswali na kutaka serikali iwape majibu katika mkutano huo na kuwafunika wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinaunda serikali.

  Ofisa wa Uangalizi wa Bunge wa LHRC, Merick Luvinga, alisema wabunge wa upinzani walihoji mambo ya msingi na kutaka wapatiwe majibu wakati wa kuchangia muswada wa Uhuru wa Mahakama.

  LHRC kimesema mkutano wa tatu wa Bunge la 10 wabunge wa upinzani walisimama imara na kuibana serikali licha ya kuwa wapo wachache tofauti na wale wa CCM ambao mara zote walitumia muda wao mwingi kuunga mkono hoja kwa asilimia 100 hata kama hazikuwa na maslahi kwa wapiga kura wao.

  Luvinga alitoa tathmini hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kituo hicho. Alisema wabunge wa upinzani ni wachache na kwamba utafiti wa kitalaam unaonyesha kwamba ulipofika wakati wa mijadala wao walikuwa makini ikilinganishwa na wale wa CCM ambao wakati mwingi walikuwa nje na waliitwa kwa kengele ili waingie ndani kupiga kura kuamua jambo fulani kama kumeibuka utata na kisha baada ya hapo walitoka nje.

  Aliongeza kuwa wabunge hao waliitwa kuingia ndani ili kupiga kura huku wakiwa hawajashiriki katika mijadala hiyo na hivyo kuwafanya wapitishe maamuzi ambayo hawajui kiini chake.

  Source: Nipashe
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haaaa haaaa, yaani Wabunge wa CCM wanaitwa tu wakati wa kupigia kura jambo ambalo hawajui limejadiliwaje! Kaaaazi ipo jamani!
   
 3. koo

  koo JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tathmin hyo imejaa ukweri m2pu nakubaliana na ripot hyo kwa asilimia mia napenda nam kutoa pongez hasa kwa wabunge wa chadema kwan ndio walio kua makin zaid chadema kazen but juhud zenu zinaonekana jamii inathamin mchango wenu
   
 4. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Hali hiyo inatuthibitishia wazi kuwa wabunge (karibu wote) wa CCM wamekwenda kule kwa maslahi yao binafsi na hawana uchungu na nchi yetu.Pia kitendo cha kuwaita ili waje kupiga kura bila hata kujua nini kilijadiliwa ni upumbavu na hatupaswi kufumbia macho....!
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Mtu umetumwa na wapigakura wako uwawakilishe halafu unakuwa unaitwa kwa kengele aibu sana hii.
   
 6. r

  rassadata Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  wabunge wa CCM hawajui walitendalo.......................................
   
 7. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Hiki Chama Cha Magamba ni laana kubwa kwa nchi yetu!
  Hakuna jema wanalofanya hapo Bungeni na ukizingatia kuwa wao ni wengi, uharibifu wao ni mkubwa sana.
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CDM = Umma wa watanzania bila kujali itikadi, maslahi ya umma
  CCM = Ubinafsi, nafasi zao katika ubunge kupitia ccm bila kujali maslahi ya umma:whoo:
  Wabunge wengine sijui wanachaguliwaje, labda kwa rushwa
   
 9. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ple..ase Please.......... wabunge wa CCM jamani sio swala la kuwakomoa CHADEMA bali ni swala la KUJENGA NCHI, kadri MNAVYOONGEZA MADUDU ndio MNAMUONGEZEA Mwenyekiti wa CCM [ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano] mzigo wa lawama za Watanzania,na kukiongezea LAWAMA chama cha Mapinduzi kuwa ni tatizo. Hizi sio zama za kubabaisha na kukubali kila linaloletwa mbele yenu bila kuangalia lina maslahi kiasi gani kwa Umma wa Watanzania.Jamani dhambi hii ya USALITI kwa UMMA wengi wenu Umma ukielimishwa ukaambiwa wabunge wao ni BORA LIENDE,jamani wengi wenu amtafika hiyo 2015, mtafukuzwa kwenye majimbo yenu tena na safari hii sio na UMMA watakua ni WANACCM wenzenu.

  Endeleeeni kujua Bungeni ni sehemu ya kuchukulia uheshimiwa [Prestige and Class] na sio sehemu ya kutumikia UMMA na kumtwisha Mwenyekiti wenu zigo la LAWAMA kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI ni chama cha MADALALI WA UHESHIMIWA. Mpunguzieni LAWAMA Mwenyekiti wa CCM,amekubali kuwasaliti Marafiki zake [Kiafrika urafiki au uswahiba ni kitu kikubwa] kwa gharama ya kusimamia UMMA leo hii nyie bado mnaendeleza kushabikia madudu.

  Si haba kwa kuwa amekubali kusimama upande wa UMMA ,ni matumaini yangu wabunge wapiga makofi na kupiga kura za NDIO kwa UNAFIKI baada ya kumsaidia Rais kutimiza ILANI YA CCM ya kuwapa Maisha Bora Watanzania, wao kushabikia na kupokea haraka kila linaloletwa mbele ya bunge na wizara husika hata kama ni kuhujumu harakati za kumpa mafanikio Rais ni usaliti kwake na kwa UMMA wa Watanzania.

  Natumai kama ameongoza mchakato wa kujivua gamba, sasa si haba akatoa maelekezo kwa wenyeviti wa mikoa na secretariet zote za mkoa kujivua gamba kwa WABUNGE WANAFIKI [Wanawajua hata upeo wao wa kuelewa hata kama baadhi yao ni wasomi wa hadhi ya UDK na UPro].Kwani huko ndio CCM itakapo rudisha hadhi yake iliyopotea na inayoitafuta,kwa kuipoteza kupitia wabunge wa HIVIHIVI [lugha ya DOTCOM GENERATION]. Kama Mwenyekiti amejitosa kuwamwaga marafiki zake kwa sababu ya mahitaji na matakwa ya UMMA sembuse nyie Wabunge wa hivihivi.

  Please Mzee Mkama na wewe Kamanda Nape wachapeni barua WABUNGE WA HIVIHIVI, kupitia wenyeviti na secretariet ya Mkoa na Jimbo mtaona watanzania watakavyo shangilia CCM itakua imepiga bao si kidogo.Pia matakua mmepunguzia mzigo wa lawama Mwenyekiti wa CCM na kuleta heshima ya dhana nzima ya KUJIVUA GAMBA aliyoiasisi itakua ni jibu moja ya majibu wananchi wanayoyategemea.
   
 10. M

  Mpanda Member

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ni ukweli mtupu nilikuwa nafuatilia kupia runinga siku hiyo na hapa niwapongeze wabunge wote waliopiga kura ya ndiyo akiwemo waziri mkuu ingawa maadam spika alijifanya hajasikia. kikubwa hapa ni wananchi wajue kuwa wabunge na hata madiwani wa ccm hawajui walitendalo na wapo kwa maslahi yao na siyo wananchi wanaowawakilisha.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Dawa ya hawa watu ni kuwa nyima kura tu..
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  DSN

  Tuko pamoja Mwenyekiti wa CCM anajitahidi kusafisha uozo ili chama kionekane kipya ameamua kumtosa rafiki yake kipenzi ili angalau kurudisha imani ya wananchi kwa chama, lakini wabunge hawalioni hilo ndiyo wanazidi kumtwisha mzigo na wakitoka hapo wanasema hawajui kwanini wananchi wanaichukia CCM, hawajui wananchi wa sasa ni wa DOT.COM wanawaona wabunge wao wanavyopiga makofi na kupitisha mambo yasiyo maslahi kwa taifa. Ningekuwa mimi Mukama, Nape ningemsaidia Mwenyekiti wangu kwa kuwaonya wabunge wa design hii.
   
 13. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  goog work for sure....tatizo la CCM ni kulindana na kunyenyekea serikali...wanakula posho bure hawa
   
 14. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Safi sana LHRC, tatizo hawa jamaa badala ya kujirekebisha na kutetea wananchi waliowatuma watasema mmetumwa na CDM.
   
 15. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwenye nyekundu, hivi CCM-Makapi yaani CUF na TLP nao wamehesabiwa au watajihesabia?
   
 16. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama CCM wanataka kumsaidia rais kwenye dhana nzima ya kujivua gamba wangeanza na wabunge wasio tija maana ndio kioo cha chama, kwani chimbuko la umaarufu wa Chadema ni nini, ni kuwa na wabunge makini kama kina Zitto, Slaa na wengine kwenye bunge lililopita ndio waliokiuza chama hasa bungeni, na sasa tunashuhudia kina Lissu, Mdee, Lema nk mwisho wa siku CCM wanalalamika chama chao kukosa umaarufu na kuanza kuumizana kwa kuchubuana ngozi bila sababu za msingi. Kuwasafisha akina RACHEL pekee hakutoshi kuendane na kusafisha wabunge wabovu walio mzigo "MIZIGO' kwa chama, ni hasara kubeba kwenye gari mizigo mingi isiyo faida. Huwezi kuwa na mbunge asiyehoji serikali kwa vikao lukuki kazi yake ni kupiga makofi na kubadilisha vimini kila kikao halafu chama kikajidai kina wabunge wengi, chama CCM kiangalie na kupima faida wanayoipata kuwa na wabunge wengi ni ipi zaidi ya kuongeza ruzuku kama chama kinazidi kukimbiwa na wanachama na kupoza umaarufu.
   
 17. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa ccm wanaweza kuwafunika wenzao kwa kuuchapa usingizi. Hapo hamuwawezi kamwe!
   
 18. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,610
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hamna kitu chenye mwanzo na kikakosa kuwa na mwisho, so CCM ndio mwisho wake huu na mwisho wake utakuwa mbaya sana na aibu mbele za watu, tusubirie tu tuone maajabu na aibu.....
   
 19. gwino

  gwino JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kazi nzuri LHRC kwani hamjaonesha woga kusema kweli penye ukweli.hii itakuwa fundisho kwa wabunge wa ccm wanaoendelea kushikilia gamba badala ya kutanguliza maslahi ya taifa.
   
 20. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bunge letu sasa liko hivi:
  Ukipinga hoja za serikari, unaonekana unaunga mkono CDM.
  Ukitaka usionekane CDM, unakaa upande wa CCM.
  Picha Hiyo ilijionyesha wakati bunge hili linaanza, matokeo ya kura za waziri mkuu, spika, na naibu wa spika zilionyesha ukweli huo, makundi mawili yalidhihirika:
  1. CDM Halisi
  2. CCM A na B, na tanzu zao.
  Hivyo unaposikia Chama cha upinzani Tanzania inamaanisha CDM.
   
Loading...