LHRC:Vyombo vya dola vimeua watu 52 mwaka10, Polisi yaongoza uvunjaji haki za binadamu

gambatoto

Senior Member
May 25, 2011
175
28
WAKATI sakata la mauaji katika Mgodi wa North Mara likiwa halijapoa, Jeshi la Polisi limezidi kuingia katika tuhuma za uvunjaji wa haki za binadamu kwa kufanya mauaji kinyume cha sheria, Ripoti ya Haki za Binadamu nchini kwa mwaka 2010 imesema kuwa kwa mwaka huo pekee, vyombo vya dola vyenye wajibu katika kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi, vimeua wananchi 52.


Source Majira:
GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Vyombo vya dola vimeua watu 73
 
Ripoti nimeisoma,inaleta matumaini. Napenda alivomalizia ripoti.
 
kama kawaida yao utasikia mwema atajitokeza kusema ripoti imejaa siasa..
 
Nathani Polisi wanatakiwa wawe na somo la human right wakiwa kwenye mafunzi yao uko vyuoni, kama tutashindwa kufundisha polisi wataendelea kuwa wakatili hivi hivi na kufata wanacho ambiwa na Wakuu wao ata kama ni Pumba.
 
Kinachoongoza Tanzania ni Udikteta wa hali ya juu, hayo mauaji na matukio mengine yaliyofuatia Tarime ni amri ya mtu mmoja. Kwa nini Kiongozi wa nchi akae kimya bila kutoa taarifa yeyote ya msingi kwa wananchi. Mbali na hao watendaji wake. Tuharakishe katiba mpya tuweze kuleta mageuzi.
 
Back
Top Bottom