LHRC: Tume ya Katiba iongeza utoaji wa elimu kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LHRC: Tume ya Katiba iongeza utoaji wa elimu kwa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 3, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]LHRC: Tume ya Katiba iongeza utoaji wa elimu kwa wananchi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 02 September 2012 11:12 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Na Aidan Mhando
  Mwananchi

  IKIWA tayari Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeanza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kwa awamu ya pili bado kunachangamoto kubwa ilijitokeza katika awamu ya kwanza ambayo kwa sasa ni vyema ikafanyika kazi.

  Katika awamu ya kwanza changamoto kubwa ambayo ilijitokeza ambayo inapaswa kufanyiwa kazi ni kuongeza kutoaji wa elimu ya Katiba kwa wananchi.

  Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LRHC) katika awamu ya kwanza ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi imeonyesha kwamba Tume ya Katiba haikutoa elimu ya kutosha kwa wawanchi ambapo tatizo la uwelewa mdogo wa wananchi kuhusu Katiba limeonekana wazi.

  Wananchi wengi wana kiu ya kuona Katiba mpya ikianza kufanya kazi mapema kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ilikuona mawazo yao yalivyo fanyiwa kazi kwenye Katiba hiyo ijayo.
  Wakati ikonekana hivyo fatifi mbalimbali zinaonyesha kwamba bado idadi ya wananchi wanaojua umuhimu wa Katiba bado ni ndogo kutokana na ukosefu wa elimu ya Katiba.

  LHRC, kilifuatilia baadhi ya maeneo ambayo Tume hiyo ilipita kukusanya maoni ya Katiba katika awamu ya kwanza ambapo walishuhudia kuwepo kwa changamoto ambazo zinapaswa kufanyiwa kazi ilikutoa nafasi wananchi wengi kushiriki kuwasilisha maoni yao.

  Kwa mujibu wa LHRC, kuanzia Julai moja hadi 31 Mwaka huu ambapo Tume hiyo ilifanya kazi ya kukusanya maoni katika maeno mbalimbali nchini mambo makubwa yalionekana ni uelewa mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu wa katika ambapo wengine hawajui Katiba ni kitu gani.

  Baadhi ya maeneo ambayo yalifanyiwa utafiti na LHRC, ni pamoja na Kisarawe na Bagamoyo ambapo katika maeneo hayo mambo makubwa yaliyo onekana na kujitokeza niuelewa mdogo wa wananchi kuhusu Katiba mpya ambapo wengine hata Katiba ya zamani hawaifahamu.

  Akielezea utafiti huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wa LHRC Dk, Helen Kijo- Bisimba alieleza kwamba kama wananchi watakuwa hawana uelewa wa Katiba iliyopo hata utoaji wa maoni ya kupata Katiba Mpya itakuwa tatizo.

  Alieleza kwa mujibu wa utafiti huo tatizo la ulewa mdogo wa wananchi kuhusu Katiba mpya ni tatizo ambalo linapaswa kushuhulikiwa kwani idadi kubwa imeonyesha bado hawafahamu nini maana ya Katiba.

  Tume iongeze muda wa kutoa elimu kuhusu Katiba
  Bisimba anaeleza kwa awamu ya pili Tume inapaswa kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi kabla ya kukusanya maoni ili kuondoa watu flani kuwekeza mawazo yao jambo ambalo litawanyima haki watanzania wengine maoni hao kutosikilizwa.

  Anaeleza katika maeneo waliyofutilia Tume haikutoa elimu ya Katiba na kwamba kama ilitolewa ni kwa kiasi kidogo ambapo ni kinyume na kifungu 17(2) (a) sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.
  “Ufuatiliaji wa LHRC, unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wananchi hawana uelewa wa kutosha kuhusu Katiba mpya jambo ambalo Tume inatakiwa kulifanyia kazi,” anaeleza Bisimba.

  Hiyo ni moja ya changamoto ambayo katika kipindi hiki cha awamu ya pili Tume inapaswa kufanyia kazi kwa undani kwa kuongeza elimu ya Katiba kwa wananchi ilikuwezesha wananchi kutoa maoni yatakayo sikilizwa bila kubanwa na mtu yoyote.

  Bisimba anaeleza changamoto nyingine ambayo Tume inapaswa kuifanyia kazi ni kuongeza muda wawanachi kutoa maoni yao kwani muda ambao umepangwa na Tume hiyo ni tatizo kwani unawabana wananchi na kusababisha kushindwa kutoa maoni yao ipasavyo.

  “Muda uliopangwa na Tume wa masaa matatu kuanzia saa tatu mpaka saa sita mchana au saa nane mpaka saa kumi hautoshi na kwamba kila mmoja kupewa dakika tano za kutoa maoni hazitoshia kuwapa nafasi ya kutosha wananchi kujieleza,” anasema na kuongeza:
  “Tume ya Katiba kama itaweza kuyashirikisha mashirika mbalimbali katika kutoa elimu ya Katiba itawezesha kuwanufaisha wananchi kupata uelewa na kujua umuhimu wa Katiba.”


  Anasema kwa kufanya hivyo kutawezesha kujua vitu gani vitakavyosaidia kupatikana kwa Katiba yenye manufaa kwa Taifa na wananchi kwa ujumla.
  Bisimba anafafanua kwamba Tume inatakiwa kutoa hamasa ya kutosha na matangazo mengi angalau wiki moja kabla ya kwenda kukusanya maoni ili kuwezesha watu wengi kupata taarifa za uwepo wa Tume hiyo katika Kata husika.

  “Tume inaweza kutumia vyombo vya habari hususa vilivyopo kwenye maeneo husika hali hii itawezesha mijadala kwenye jamii kutambulika na kueleweka jambo ambalo litasaidia kuongeza ushiriki wa watu kwa wingi,” anaeleza na kuongeza:
  “Kama Tume haitafanya hivyo ushiriki wa wananchi utaendelea kuwa finyu kama tulivyo shuhudia Tume ikishirikiana na Wakuu wa Wilaya katika kuandaa mikutano ya kukusnaya maoni.”


  Anafafanua kwamba ni vyema Tume kufuatilia zaidi suala hili ilikuondoa hali ya kikundi flani kuwapa taarifa wakati wengine hawana kwa mfano Bagamoyo katika Kata ya Makurunge ilitokea jambo hilo kwa badhi ya vikundi kuwa na taarifa za Tume hiyo kuwepo huku wengine wakiwa hawafahamu chochote.

  Tume iongeze muda wa kuwepo kwenye Kata
  Bisimba anaeleza kwamba taarifa za uwepo wa Tume katika kipindi cha kukusanya maoni ya wananchi kwa wamu ya kwanza umekuwa mdogo jambo ambalo linasababisha wananchi waache kushiriki kufanya hivyo.

  “Taarifa za uwepo wa Tume ya kukusanya maoni katika Kata umekuwa finyu hali ambayo imepelekea watu kuacha kushiriki kutoa maoni yao jambo ambalo Tume inapaswa kufanya marekebisho kwa kutoa taarifa za kuwepo kwenye Kata kwa muda sahihi iliwananchi waweze kufahamu uwepo wao,” anaeleza.

  Bisimba alitoa mfano katika Kata ya Mkurunge Bagamoyo mmoja wa wachangiaji alisema “Nyie Tume mnafuata barabara tu kama mbio za mwenge, ujio wenu haujulikani…, mnazidiwa hata na matangazo ya Coca Cola ambayo hufikishwa hadi vijijini.”

  Anaeleza kupitia mfano huu ni vyema Tume ikafanya uhamasishaji na kutoa taarifa kwa muda mwingi ili wananchi wafahamu ujio wa Tume katika vijiji husika jambo ambalo litasaidia kuongeza hamasa ya ushiriki wa wananchi.

  “Kutokana na mambo kama haya Tume inapaswa kujipanga,ikiwezekana wiki moja kabla ya kuanza kufanya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi, iwe imefanya kazi ya uhamasishaji, hali hiyo itaongeza ushiriki na utoaji wa hoja zenye mwelekeo, malengo na manufaa,” anaeleza.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,491
  Likes Received: 4,764
  Trophy Points: 280
  Nilidhani wataanza na tamko la Daud Mwangosi..........
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  ...Nadhani hilo tamko litakuja tu Mkuu...Mama Bisimba yuko makini sana katika utetezi wa haki za Watanzania nchini unaofanywa na hii Serikali dhalimu ya wauaji. Serikali hii dhalimu wanamuona ni kero kubwa sana.

   
Loading...