LHRC taasisi isiyokua na umuhimu ndani ya taifa letu.

accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,496
2,743
Nimekua nikifuatilia sana utendaji kazi wa taasisi hii, kiukweli kabisa sijui kwanini waliianzisha.

Wamekua wakitoa matamko mbalimbali lakin sikuwahi kuona hata moja likifanyiwa kazi. Tukianzia karibu tu kwenye uchaguz wa mwaka Jana, walitoa matamko mbalimbali dhidi ya mwenendo wa uchaguzi lakin yote yalitufutiliwa mbali.

Juzi wametoa Matamko dhidi ya wabunge waliofukuzwa bungeni lakini hakuna lililobadilika zaidi ya wabunge husika kuongezewa adhabu.

Sijawahi sikia wamemtetea mnyonge yyte mahakamani kwa kutumia wanasheria wao wanaokula mishahara ya bure.

Sijaona wakisaidia mtu yyte kijijini ama mijini kuisaka haki yake.

Naona hata flora show na Joyce Kiria wanafanya kazi kubwa kuisaidia jamii kuliko taasisi hii.

Au Mimi labda sielewi kiundani ni nini kazi ya taasisi hii? Mnaojua mnijuze
 
Back
Top Bottom