LHRC kuweka watazamaji katika vituo vyote vya kupiga kura Igunga

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) kimetangaza kutuma watazamaji wake katika vituo vyote vya kupiga kura siku ya Jumapili kuangalia upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura.. Mimi ninavyoona CCM hawatapenda hii, watasema kisheria na kikanuni hakutakiwi watazamaji kutoka taasisi binafsi kuangalia upigaji kura na kuhesabu kura.

Tususbiri tuone.

Chanzo: Ch10 news saa moja usiku huu.
 
Hawatawaruhusu kuingia ndani ya vyumba vya kuhesabia kura ambapo uchakachuaji hufanyika! Magamba wakiona mambo magumu wata-delay kuhesabu kura, then giza inaingia, kazi rasmi ya uchakachuaji huanza baada ya umeme kuzimwa "kwa bahati mbaya" na Ngeleja!
 
Nadhani tutakuwa na points of reference ya kuaminika baada ya uchaguzi. Ni vema kukawa na waangalizi wa kutosha, hata ikiwezekana asasi zote za kiraia zikawa na uwakilish huko.
Tanzania yetu, ni rahisi kuiamini hata NGO kuliko serikali hii iliyopoteza legitimacy na kuendelea kutawala KWA MUJIBU WA SHERIA kandamizi za ccm.
 
Wakifanikiwa kufanya hivyo itakuwa safi,itasaidia kiasi kuondoa ukakasi wa uchaguzi,,japo si kazi ndogo hiyo kuweka OBZEVAS kila kituo
 
Hii naiona nzuri pia hata kwao ccm maana itawaepushia dhana ya kwamba wanachakachua matokeo kwa msaada wa tume ya uchaguzi kupitia mkurugenzi, acha waruhusiwe hao kupunguza maneno maneno
 
Napongeza hatua hii iliyochukuliwa na kituo hiki na vituo vingine vifuate. Mimi na rafiki zangu siku ya ijumaa tutatua igunga kwa ajili ya kuangalia zoezi zima la uchaguzi.
 
Hao LHRC ni binadamu au cmpt? Mtz gani leo alienaimani na uzalendo?
Hivi mnaijua pesa au mwaisikia?pesa ndo kila kitu
Tusubiri tuone
 
Back
Top Bottom