Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 10,003
- 12,466
Na David Maphone
Niko bize kwa siku kadhaa sasa nikijipa kibarua cha kusaka taarifa za mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania ili kuona wametekeleza kwa kiwango gani jukumu lao la msingi kwenye kipindi hiki kigumu cha ugojwa hatari wa Corona ( COVID 19).
Watanzania walio wengi nikiwemo na mimi nilitegemea kusikia matamko ya kuwatetea watu masikini kutokana na Wafanyabiashara kupandisha bei za vifaa kinga vya kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona (Coronavirus)
Kwa uhodari ule ule mliokuwa mkitumia kuwatetea CHADEMA mpaka baadhi ya watanzani kufikia kuamini kwamba mashirika ya kutetea haki nchini Tanzania ni matawi rasmi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
MNATIA SHAKA SANA
Liko wapi tamko la Legal and Human Rights Center (LHRC) kwenye sakata hili? Mbona sioni povu la kituo hiki ilihali Watanzania wa kawaida wanapokwa uhai wao na wafanyabiasha wenye tamaa za mali kuliko utu.
Pengine nimeharakia sana labda mnajipanga kwa ajili ya kufanya utetezi wa sakata hili kwa muda mtakaona muafaka kwenu au suala hili limekosa umuhimu katika mashirika yenu.
USHAURI WANGU
Wakati mwingine mjikite kwenye kutetea utu na maisha ya watu kuliko kuelekeza nguvu zenu kwenye masuala ya kisiasa. Mnapoteza imani kubwa sana kwa Watanzania.
MTANZANIA CHUKUA HATUA JIKINGE NA CORONA.
Narudi tena hapa hapa!
Mwandishi: David Maphone.
0653246600
Dar es Salaam, Tanzania.