EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Mtandao wa uangalizi wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga mkoani Tabora, umetoa tathmini yao na kusema kuwa zoezi hilo liligubikwa na kasoro nyingi zikiwemo za wapiga kura kuhongwa pombe, kuahidiwa kupewa nyama, kuuza shahada zao baadhi ya Mawaziri kuingilia mchakato huo pamoja na wananchi kurubuniwa kuwa mgombea wa Chadema kajitoa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa jana, Mkuu wa kitengo cha uchaguzi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Merick Luvinga, alisema walibaini kasoro hizo kabla ya upigaji kura na siku ya kupiga kura Jumapili iliyopita.
Uangalizi wa uchaguzi huo ulifanywa na Mtandao unaojumuisha mashirika 17 yasiyokuwa ya kiserikali ikiwemo LHRC ambapo wamesema maeneo mbalimali wanasiasa walihonga pombe, nyama na mawaziri kufanya shughuli zisizowahusu.
Mtandao huo ulipeleka waangalizi 243 na kila kata ikiwa na waangalizi 26.
Luvinga alisema siku ya kupiga kura, walishuhudia watu wakiwa wamenunuliwa pombe na wagombea na kunywa jirani na kituo cha kupigia kura pamoja na kupewa nyama ili kuwashawishi kuwachagua watu waliowahonga.
Aidha, alisema siku ya kupiga kura, gari la Mbunge mmoja wa mkoani Tabora lilipita mitaani na kuwatangazia wananchi kuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Kashindye, alikuwa amejitoa katika kugombea nafasi ya ubunge hivyo wamchague mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu.
Alieleza kasoro nyingine zilizojitokeza katika uchaguzi huo kuwa ni pamoja na watendaji wa vijiji kugawa mahindi kwa wapiga kura kwa lengo la kuwashawishi wamchague mgombea kutoka chama fulani.
Luvinga alisema waangalizi hao baada ya kuona matukio hayo, walipiga simu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), lakini hawakupata msaada wowote.
Source: Nipashe