LHRC: Gari la CCM liliwatangazia wananchi Igunga kuwa Kashindye kajitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LHRC: Gari la CCM liliwatangazia wananchi Igunga kuwa Kashindye kajitoa

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by EasyFit, Oct 7, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mtandao wa uangalizi wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga mkoani Tabora, umetoa tathmini yao na kusema kuwa zoezi hilo liligubikwa na kasoro nyingi zikiwemo za wapiga kura kuhongwa pombe, kuahidiwa kupewa nyama, kuuza shahada zao baadhi ya Mawaziri kuingilia mchakato huo pamoja na wananchi kurubuniwa kuwa mgombea wa Chadema kajitoa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa jana, Mkuu wa kitengo cha uchaguzi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Merick Luvinga, alisema walibaini kasoro hizo kabla ya upigaji kura na siku ya kupiga kura Jumapili iliyopita.

  Uangalizi wa uchaguzi huo ulifanywa na Mtandao unaojumuisha mashirika 17 yasiyokuwa ya kiserikali ikiwemo LHRC ambapo wamesema maeneo mbalimali wanasiasa walihonga pombe, nyama na mawaziri kufanya shughuli zisizowahusu.

  Mtandao huo ulipeleka waangalizi 243 na kila kata ikiwa na waangalizi 26.

  Luvinga alisema siku ya kupiga kura, walishuhudia watu wakiwa wamenunuliwa pombe na wagombea na kunywa jirani na kituo cha kupigia kura pamoja na kupewa nyama ili kuwashawishi kuwachagua watu waliowahonga.

  Aidha, alisema siku ya kupiga kura, gari la Mbunge mmoja wa mkoani Tabora lilipita mitaani na kuwatangazia wananchi kuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Kashindye, alikuwa amejitoa katika kugombea nafasi ya ubunge hivyo wamchague mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu.

  Alieleza kasoro nyingine zilizojitokeza katika uchaguzi huo kuwa ni pamoja na watendaji wa vijiji kugawa mahindi kwa wapiga kura kwa lengo la kuwashawishi wamchague mgombea kutoka chama fulani.

  Luvinga alisema waangalizi hao baada ya kuona matukio hayo, walipiga simu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), lakini hawakupata msaada wowote.


  Source: Nipashe
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mimi nilishasema sanduku la kura halitaiondoa CCM lazima tuchinjane kidogo ili tueshimiane
   
 3. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  kweli kabisa
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  pamoja na kufanya yote hayo kununua pombe, nyama, kugawa Pesa n.k, lakini wamekula kwata la kutosha kutoka kwa Makamanda wa CDM na sidhani kama Kafumu atakubali kurudi tena ulingoni 2015 au kama kuna kiongozi wa CCM atakayerudi Igunga kukampeni...
   
 5. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Tatizo wa TZ waoga sana kumwagwa vinyesi ngoja wanyonywe kwanza ndo watie akili
   
 6. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa wezi wataendelea na uhuni huu mpaka lini daaaa!!!
   
 7. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  1047= ak 47?
   
 8. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nimesoma gazeti moja leo eti watu walipewa nyama ya Mbuni wakadanganywa ni ya ng'ombe wakaichagua ccm. Kiukweli ccm imewadhalilisha wananchi wa Igunga yaani kumhonga mtu nyama kilo 1 ni dharau ya hali ya juu, sasa hiyo nyama atakula miaka mingapi. Na hao wanaharakati walikuwa wapi kuwaeleza wanaigunga hayo ndo wajitokeze saiv?
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Someone aitishe maandamano please.
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Safari bado ni ndefu lakini inshallah tutafika.
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Everybody is someone.
   
 12. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Watanzania tunamuogopa sana Moreno Ocampo hasa tunapoona kinachoendelea kwa kina Uhuru Kenyatta na wenzake
   
 13. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  We fikiri tofauti ya kura na mbinu chafu walizotumia.
   
 14. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Jamani jama, inamaana uwezo wa mtz mwenzetu wa kufikiria na kufanya maamuzi unanunuliwa kwa Shs 4,500 (kilo moja ya nyama). Ndo maana na wawakilishi wanauza rasilimali ovyo ovyo (wanyamapori, madini, nk).
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mpira ni magoli na sio changa.
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Pole kwa wale waliopiga kura kwa ushawishi wa Pombe na Nyama
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwa kuanzia,tukuchinje ww.
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Siongezi lolote kijana nisije haaribu uliyo mwaga hapa .Ila kama kesi inaenda Mahakamani CCM itaanguka chali maana ushahidi kila kona na muuza nyama atasema kwa nini aliua mifugo 3 kwa hasara na furaha gani .
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kama jimbo moja wametumia Bil.3 fikiria majimbo zaidi ya 200 ongeza na urais watatumia sh. ngapi halafu at the end of the day waambulie 50.3% ya kura zote, and for how long will this keep on happening?
   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,976
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ukizungumzia kurudi 2015 ni mbali sana kwani kwa ushahidi uliopo sijui kama atanusurika kesi ya uchaguzi. kumbuka pia Magufuli aliwaambia wana Igunga wakimchagua Kafumu hawatajengewa lile daraja la Mbutu; sidhani kama hii ni sawa
   
Loading...