Letter to Mr President

Donald Marcus Hemu

JF-Expert Member
May 14, 2019
372
531
Ikiwa takriban imekamilika miaka minne toka Rais wetu kipenzi Dkt John Pombe Magufuli achukue madaraka tumeshuhudia mengi sana ya kustaajabisha ya kujenga nchi kama vile sakata la watumishi hewa, SGR, Bombardiers, sakata la mchanga na mengineyo mbali mbali.

Napenda kukupongeza sana mheshimiwa Rais kwani kwa awamu hii moja tu ambayo bado haijaisha tumeona implementations kwa zaidi ya 99% jambo ambalo Watanzania wengi hatujawahi kuona(isipokuwa mababu zetu waliokuwepo enzi za Hayati Mwalimu Julius K Nyerere).

Japo Watanzania wengi tunalalamika kwamba hali ya maisha imekuwa ngumu lakin nadhani wengi hatujui kwamba kinachofanyika sasa ni Kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Leo hii kuna baadhi ya watanzania wanadhani kwamba Ile formation iliyokuwa kwenye awamu ya nne (yaan foreign aids, foreign investment, corruption, nepotism na nk) itumike.

Naomba nizungumze kitu kimoja kinachofanyika sasa ni pure development (without depending foreign aids & loans).

Enzi zile ilikuwa ni through depending western aids ambayo tumeona ndani ya muongo mmoja deni la taifa liliongezeka kwa kiasi Kikubwa.

Mwisho wa yote napenda kuzungumzia kuhusu sera ya Serikali ya Tanzania awamu ya Tano ambayo ni "Tanzania ya viwanda"

Kuna baadhi ya wasomi feki wamekuwa wakizungumzia kwamba eti ooh sera ya nchi imefeli, mara mbona hatuoni viwanda vipya alivyojenga mheshimiwa Magufuli.

Napenda kusema kwamba thinking capacity ya hao watu ni ndogo sana kwa sababu hata mtu aliyemaliza form four ukimuuliza kuhusu sera ya nchi imefanikiwa atakujibu ndio.

Rejea factors for industrial development lakini kuna wasomi kabisa wanashindwa kulitambua Hilo.

Naombeni Watanzania tumuache mheshimiwa afanye kazi yake, criticisms zifuate baada ya kumaliza awamu.
 
Back
Top Bottom