Let's talk about savings: Ikitokea umeachishwa/umeacha kazi leo, una akiba ya kukutosha kwa siku ngapi?

Mr.genius

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
1,369
1,169
Kulingana na usawa huu ulivyo, na jinsi kipato kilivyo kigumu upatikanaje wake na hata kinapopatinakana hakikidhi mahitaji na hapo hapo unahitajika uweke akiba i wonder how is it possible kwa uchumi huu nilionao!.

My personal story.
Ni kijana nimeajiriwa mahali mshahara wangu ni Tsh 250,000 per month najitegema lakini bado sijaoa! Kwa muda sasa nimekua nikipambana kufanya savings kwa sababu najua umuhimu wake hasa kwa wakati wa shida na pia hata kama si wakati wa shida unaweza jiwekea akiba ili uweze kufikia malengo fulani ya kiuchumi like kupata mtaji wa kuanzisha biashara e.t.c!

Lakini mambo yamekua si rahisi hivyo mshahara haunitoshi kulingana na mahitaji niliyonayo na pamoja na kujitahidi kujibana na kwa maana hiyo haufiki hata mwisho wa mwezi hua nakaaga natafakari hivi kwa mtindo huu mshahara kutotosha ikitokea nimeachishwa kazi sasa hivi ka akiba kangu kadogo ninakojiwekea kanauwezo wa kunitosha hata kwa wiki mbili zaidi kweli??

Nimeuleta uzi huu wa changamoto zangu binafsi kufahamu wenzangu linapofika suala la saving mnakabialiana nalo vipi na je, una kiwango cha kutosha cha saving ikitokea chanzo chako cha mapato mirija imekatwa? Mwenzangu unatumia njia zipi unazoziamini katika kufanya saving? Let me hear from you, let's talk about savings!
 
Humu Jf wengi watasema wa mamilioni benki...Akiba ni jambo la muhimu na ni ukweli wengi wanalipuuzia au kulichukulia kwa urahisi.
Kuna kanuni ya kuweka akiba kabla hujaanza kutumia fedha,ni nzuri inasaidia sana.
Japo kipato ni kidogo, tushirikishane mbinu za kufanya saving, ni utamaduni mzuri labda tukiongezewa maarifa tunaweza nasi kujikwamua kupitia savings ndogo ndogo!
 
Mr.genius Mshahara hua hautoshi mkuu hata ulipwe sh? OK iko ivi nlivokua sina kazi na nlivoajiriwa maisha ni yaleyale tu hela sina. Nkagungua kumbe kabla ya ajira kwenye mishe zangu napata kipato kidogo sana na matumizi madogo pia maanaake napata hela kidogo na majukumu nnayo machache mwisho wa picha hela yote inaisha nabaki sina hela,

Nlivoajiriwa maana mi ni mtumishi wa uma kipato kikaongezeka kiasi chake na matumizi yakaongezeka automatically hela inaisha nakuwa sina hela kama kawaida.

Nikagundua hata ulipwe Mara kumi ya mshahara wako wa sasa matumizi yataongezeka kuendana na kipato mwisho wa picha no saving kama kawaida.

Hela haiwezi kukosa cha kufanya eti utumie zen inayobaki ndo ufanye saving iyo haiwezekani. Hela una save kabla ya kuanza kuitumia yaan [money to be saved iwe kwenye matumizi yako] yaani unatumia mfano 150k Ku save.

Nachofanya saivi nlifungua saving account mshara ukitoka tumizi la kwanza ni saving zen mengine ndo yanafuata,

Iyo ni ngumu sana implementation lakini I'ma man of principles kila mwezi na save nusu ya mshahara 250k.

Note: najua iyo 250k nao save kila mwezi sio kitu maana hela inatakiwa iwe kwenye mzunguko izalishe zingine kufanikisha malengo makubwa,

Mia tana haiwi 500 bila kukusanya miamia 5.
Kusanya kidogo ulichonacho kikusaidie kupata kikubwa.
 
Kuna hii hapa
tapatalk_1522855232801.jpeg
 
The best way ya kufanya savings,ikifika mda wa mavuno nunua chakula cha kutosha, nunua friji yako,ukiwa na mchele hada debe 5 kwa wenye familia,na gunia la mahindi na lita kumi ya mafuta ya alizeti huo mwaka unakupita poa kabisa,kila mwisho wa mwezi nenda na sh arobaini kanunue kauzu na maharage nyanya nk nk huwezi amini route za kwa mangi kila siku mara nipe una robo nk,

Lakini ukinunua mazaga yako mfano carot unayouziwa wewe gengeni sh 200 ukienda karume unapata sadolini kwa 5000 ukiweka kwenye friji si zinakupiga kick, sado ya nyanya 4000 nk,unaweza kuta kila siku pay inayotoka mfukoni haizidi hata 3000 kwa mboga.utashangaa bajeti yako kwa mwezi kwa chakula tuu hazidi 70000 out of lakini naa,sasa hapo huja save bado?

Hapo home machalii unawapiga na uji poa wa lishe,maisha haya bila kuwa na bajeti usawa wa uncle magu hutoboi,mi kuna mzee nilimshuhudia analipwa 150000 na alikuwa anaishi hivyo huwezi amini anasomesha watoto shule kali tuu, yeye anakwambia mi dukani huwa sikanyagi kununua chakula labda niamue mwenyewe
 
Saving its all about kujali kesho yako na kuwa na nidhamu na pesa unayoingiza
Ukitaka kusave kwa lazma
Kama umeajiriwa, nenda bank unayopokea mshahara wako waambie wawe wanakukata % fulani kila mwez na kuweka kwa akaunt ya malengo

Mimi nasave laki na nusu kwa kila wiki
Challenge nimejipa nifike wiki 52 hapo December

Ni uamuz mgumu sana lakin unakupa nidham ili ikifika December unachukua chako unaenda kuinvest
 
Kuachishwa halafu ukawa umejiandaa kwa savings ya kutosha ni ngumu. Kumbuka kuachishwa huwa kunatokea kama ajali. Japo inategemea pia ulianza kazi ukiwa na malengo gan, kiwango cha mshahara na umefanya kazi kwa muda gani, ndo unaweza ku-determine savings yko.
 
The best way ya kufanya savings,ikifika mda wa mavuno nunua chakula cha kutosha,nunua friji yako,ukiwa na mchele hada debe 5 kwa wenye familia,na gunia la mahindi na lita kumi ya mafuta ya alizeti huo mwaka unakupita poa kabisa,kila mwisho wa mwezi nenda na sh arobaini kanunue kauzu na maharage nyanya nk nk huwezi amini route za kwa mangi kila siku mara nipe una robo nk,lakini ukinunua mazaga yako mfano carot unayouziwa wewe gengeni sh 200 ukienda karume unapata sadolini kwa 5000 ukiweka kwenye friji si zinakupiga kick,sado ya nyanya 4000 nk,unaweza kuta kila siku pay inayotoka mfukoni haizidi hata 3000 kwa mboga.utashangaa bajeti yako kwa mwezi kwa chakula tuu hazidi 70000 out of lakini naa,sasa hapo huja save bado? hapo home machalii unawapiga na uji poa wa lishe,maisha haya bila kuwa na bajeti usawa wa uncle magu hutoboi,mi kuna mzee nilimshuhudia analipwa 150000 na alikuwa anaishi hivyo huwezi amini anasomesha watoto shule kali tuu,yeye anakwambia mi dukani huwa sikanyagi kununua chakula labda niamue mwenyewe
Vizuri sana Mkuu

Njia mojawapo ni kuweka stock ya vitu ndani, hii hupunguza garama zisizo za lazima zitokanazo na manunuzi yz rejareja ambayo mwishoni ukija kipiha mahesabu unakuta ni hela nyingi zimetumika bila kujijua kutokana na kutoa kidogokidogo.
 
Kwangu iko hivi "10% of all I earn is mine to keep".
Haikuwa rahisi mwanzoni lakini sasa hivi imekua utamaduni jadi na kasumba.

Pesa haikosi matumizi. Vilevile kuna raha sana kuona unavijisent vyako vimetulia tu, umedunduliza kidogokidogo.
 
Mimi Siku Zote Na Principal Kutokugusa Mshahara,mishahara Ikutane Bank,nahamisha Napeleka Bank B Au Kwenye Mzunguko

Haya Yote Nayaweza Kupitia Kitu Kimoja Biashara Ndogo Tu,nkienda Kazini Natengeneza Juice Kuwauzia,chapati Au Maandazi,(hawanielewagi Sistaduu Wa Haja Nabeba Juice Nahangaika Na Ngano)napata Pesa Ya Kula,kutengeneza Nywele,n.K

Mara Nyingi Mshahara Natumia Kulipa Kodi Kufanya Maendeleo,nikaumwa Mwaka Na Kukaa Nyumbani Miaka 2,mpaka Naumwa Nilikuwa Napesa Ya Kujikimu Mwaka Na Nusu,he He He Sasa Naelekea Kupona Kabisa Na Kurudi Kazini,sina Sh Moja Hapa Ila Nina Plan Za Biashara 3 Ndogo Ndogo,moja Kwa Ajili Ya Kupata Mahitaji Ya Nyumbani,nyingine Mahitaji Ya Mwanangu Na Jamaa Jamaa,matanuzi Nyingine Kufanya Saving,mishahara Lazima Ikutane Bank, Na Ofisini Lazima Mnipe Tuhuma Mimi Mwizi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom