Leticia Nyerere: WaTanzania wengi wamepoteza uzalendo kwa taifa lao!

Fadhili Paulo

Verified Member
Sep 1, 2011
3,220
2,000
Mbunge Leticia Nyerere amesema waTanzania wengi wamepoteza uzalendo kwa Taifa lao.

Amesema uzalendo maana yake ni kuipenda bendera ya nchi yako na kuheshimu waasisi au viongozi wa taifa lako, anasema anashangaa siku hizi utaona kwenye daladala mtoto mdogo au kijana amekaa kwenye kiti huku mtu mzima au mzee amesimama na hakuna anayekemea hilo.

Hayo ameyasema leo bungeni wakati akichangia taarifa ya kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,274
2,000
Jamani, huyu mama anaejiita Leticia Nyerere, ni bado mke wa mtoto wa Nyerere?

Uongo anaousema ni huu, kuwa na kukaa kwake Merekani hajawahi kuona "Baba wa Taifa la Merekani George Washington" akidhihakiwa;

Dah! huo ni uongo wa wazi wazi, machache haya hapa ya kudhihakiwa George Washington:Leticia, kuna tons and tons za dhihaka kwa George Washington. Unalidanganya bunge na Watanzania kwa ujumla kwani tunakuona live, kwa kuwa eti umekaa USA.

Wewe inaonesha ulikuwa unakaa USA lakini huijui USA au unaona Watanzania tu wajinga kiasi cha kutudangaya kijinga namna hiyo?

Inaonesha u mfinyu sana wa mawazo.

Wakwanza wewe unalidhihaki jina la Nyerere kwani umeshaachika na bado unalitumia kama una hati miliki nalo.
 

Fadhili Paulo

Verified Member
Sep 1, 2011
3,220
2,000
CCM ndio imepoteza uzalendo...Na hii inaonyesha kwa maneno na matendo ya wanachama na viongozi wao.

Amesema waTanzania, hivyo automatic CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, CHADEMA na vyama vingine vyote nao wanahusika na kupotea kwa uzalendo huu
 

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
17,838
2,000
Huyu mama kwa jinsi anavyoongeaga huwa anaonekana kituko, wabunge huwa wanajipanganga kumzodoa hata kabla hajainuka.
Huwa anajiona yuko exposed sana kwa vile ameishi nje kumbe hamna kitu.
 

naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,710
2,000
Yeye amesema hajaona hizo dhihaka na wewe unalazimisha kuwa ameziona!!Kama unavyojilazimisha kushangaa mwanamke kutumia jina la mumewe wakati wameshaachana,au na wewe tukuorodheshee majina yao?
 

matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,055
1,195
Jaamni huyu mama anaejiita Leticia Nyerere, ni bado mke wa mtoto wa Nyerere? Uongo anaousema ni huu, kuwa na kukaa kwake Merekani hajawahi kuona "Baba wa Taifa la Merekani George Washington" akidhihakiwa;Dah! huo ni uongo wa wazi wazi, machache haya hapa ya kudhihakiwa George Washington: Leticia, kuna tons and tons za dhihaka kwa George Washington. Unalidanganya bunge na Watanzania kwa ujumla kwani tunakuona live, kwa kuwa eti umekaa USA.Wewe inaonesha ulikuwa unakaa USA lakini huijui USA au unaona Watanzania tu wajinga kias cha kutudangaya?Inaonesha u mfinyu sana wa mawazo.Wakwanza wewe unalidhihaki jina la Nyerere kwani umeshaachika na bado unalitumia kama una hati miliki nalo.
Hili jibu nimelipenda I really like JF
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,274
2,000
Wewe lengo lako hasa ni nini? Kwamba ihalalishwe kumdhihaki baba wa taifa?

Soma vizuri post yangu. Analidangaya bunge na Watanzania, Kama lengo lake Nyerere asidhihakiwe angesema tu hivyo na si kudanganya eti "mimi nimekaa Merekani na Washington hadhihakiwi huko".

Uongo wa nini nyinyi magwanda?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom