Leticia Nyerere (CHADEMA): Mitandao ya kijamii inatumika kutukana viongozi, wahusika wakamatwe!

Status
Not open for further replies.

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Leticia Nyerere, mbunge wa viti maalum chadema akichangia bungeni hivi sasa amesema yeye ni mtaalamu wa teknolojia ya CYBER CRIME, anaitaka serikali iwakamate mara moja watumiaji wa mitandao ambao wanatumia muda wao mwingi kutukana watu, wakiwamo viongozi mbalimbali.. ametoa mfano wa matusi yaliyotumwa kwa naibu spika na spika.
Amesema wapo watu hivi sasa wapo ndani lakini hataki kuwataja majina kwa kosa la kuchafua watu mitandaoni.

Nyerere anasema nyie kutwa mnakesha kutukana watu tuuuuu, wakati huyo unayemtukana anadunda tu hata habadiliki, si uache ufanye kazi nyingine????

Anasema watu wapo tu wanaangalia bunge anatafuta leo amtukane nani, akatolea mfano wa watu kumtukana SITTA, naibu spika akasema yeye ni mhanga ametukanwa sana.

wana JF, MNALIONAJE HILI????????????
 
Sure mkuu. Nimemsikia pia naibu spika akisema kuwa na yeye ni miongoni mwa waathirika wa matusi mitandaoni lakini anadunda tu
 
Huyu mama tokea ameanza kuongea mpaka anakaa alizungumzia swala la kutukanwa mitandaoni povu jingi lilimtoka utadhani kwimba alitumwa kuelezea mambo ya kutukanwa mitandaoni, huyu bibi mkubwa huwa simwelewagi nafikiri bado ukijani haujatoka ndani,
 
Akiongea bungeni katika kumuunga mkono mchangia hoja Leticia Nyerere kuhusu matumizi mabaya ya mitandao...Job Ndugai naye akatoa moyoni yaliyomkumba kwenye mitandao.
 
Taifa lina changamoto nyingi ktk maswala ya new technology ikiwemo watu kupoteza ajira yeye anapeleka stress zake za kutukanwa na kuanza kuwatetea mawaziri wa ccm!
 
Mbunge wa CHADEMA analalamikia watu kutukanwa kwenye mitandao ya kijami!!!!! Akimtolea mfano naibu spika! Hee! Aise! Sasa si angetoa mifano ya waliotukanwa , walivyotukana, aliewatukana na hatua walizochukuliwa hao anaosema wamekamatwa? Hata hivyo kutukana kwa ujumla wake si tabia ya kistaarabu.
 
MMh, uongozi kazi kama huna kifua
Wengine wanatukaniwa hadi wazazi wao na wanenyamaza tu
 
Bora ameongea mbunge wa chadema, angeongea wa ccm ingekuwa nongwa. Si mnakumbuka ile kauli ya juma nkamia kuhusu mtandao wa jf?
 
kwahiyo anataka wote twende tukatukanie matusi bungeni kama yale ya juzi na mengine ya nyuma? waache wanaotumia mitandao kufikisha ujumbe wao, maana viongozi wanakera.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom