Leticia Musore wa CHADEMA ahamia NCCR

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.
 
Huyo atakuwa amepandikizwa kapata mrungura

Yaani hapa utasikia mengi, utasikia hata mjumbe wa chadema kijijini kahamia TLP NCCR yaani ilimradi katangazi watu wamesikia.

Mafisadi angaika CHADEMA ni cha kinachokubalika kwa watu
 
Sasa kama kahama si katumia haki yake ya kidemokrasia kama alivyofanya akina Shibuda n.k. Hauna kazi ya kufanya ila kujadili watu?
 
mwenye jibu zuri hapa atakuwa DR.MKUMBO kwani ndio alipewa kazi kama consultant kutengeneza vigezo viti maalum,atuambie kama huyu alikuwa kati ya ishirini kama anavyodai.
 
Huyo atakuwa amepandikizwa kapata mrungura

Yaani hapa utasikia mengi, utasikia hata mjumbe wa chadema kijijini kahamia TLP NCCR yaani ilimradi katangazi watu wamesikia
Mafisadi angaika CHADEMA ni cha kinachokubalika kwa watu

Kila anayehama au kutofautiana na chadema ni pandikizi, pheew!
 
Leo ndiyo amegundua kuwa NCCR hakuna ubaguzi? Achape zake mwendo hana jipya huyo! Wenye njaa utawajua tu! Hawana dhamira ya Kweli. Angefafanua ubaguzi wa CHADEMA uko wapi.
 
bado Zitto ,yaani huyu siku akiondoka ntalipia hata kikosi cha matarumbeta toka pale magomeni na wale wacheza vibao kata wamsindikize huko CCM
 
Kila anayehama au kutofautiana na chadema ni pandikizi, pheew!

Sasa wewe ulishaona wapi mtu ukikosa nafasi fula unaanza kupiga kelele wakati hata wananchi hawakufahamu, walikuwa wanatumwa kwenda kupunguza kasi ya kuwaumbua mafisadi na kuwakomboa wananchi.
 
Mleta hoja hebu ulizia huyu mama anatoka mkoa gani na kwenye huo mkoa hakuna mwingine aliyechaguliwa?

Ni mwekiti wa taifa, mkoa au wilaya? Wanasiasa wetu wakati mwingine wanapaswa kuwa wavumilivu, ingelikuwa vema kwake angevumilia akajipanga kugombea jimbo 2015 naamini kungekuwa na support ya kutosha.
 
Kila anayehama au kutofautiana na chadema ni pandikizi, pheew!

Jaaah kwa nini uondoke kwenye chama kwa sababu ya cheo?, kuna vyeo vingapi na wanachama wangapi?

Muda wa kuondoka ilifika, na huu ndio wakati mzuri, mpaka mwisho wapigananji wa kweli wataonekana
 
Jaaah kwa nini uondoke kwenye chama kwa sababu ya cheo?, kuna vyeo vingapi na wanachama wangapi?

Muda wa kuondoka ilifika, na huu ndio wakati mzuri, mpaka mwisho wapigananji wa kweli wataonekana

Wanasiasa kama hawa wapo wengi na sifa yao kubwa ni kukosa uvumilivu
 
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CHADEMA amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa. Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?

Cha hajbu ni nini, tulivyoanza nchi hii wote tulikuwa CCM, sasa hivi 80% ya wananchi wanafaa kupiga kura wako CHADEMA na vyama vingine vya upinzani. Kama Leticia kahamua kuhama chama ni haki yake ya msingi
 
Uliona hivyo mana JF ujue huyo alijiunga kwa interests zake, CHADEMA wako makini hata kama angekuwa wa kwanza katika orodha kama hakuwa na nia ya dhati out.
 
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.

Leo ndio ameona hayo siku zote alikuwa wapi?
 
Alikuwa mmoja wa wagombea Ubunge viti maalum hivyo amekosa ndio ametimka namtakia kila lakheri katika safari yake ya kisiasa ana haki ya kuenda nakotaka.

Naomba kuwasilisha
 
Zitto mfuate Mwenyekiti wa Wanawake, naona unachelewa kuitia timu NCCR-CCM Mbadala!! Mbona hata wa SSM walihamia Chadema? Huo ndo uhuru wa demokrasia. Tena huenda Chadema walishamshtukia huyu mama kuwa si mzalendo rather pandikizi ndiyo maana hawajampa ubunge wa viti maalum. Na huko kwa Mbatia Mufilisi, ameshajiweka CCM Mbadala watammaliza taratibu na chama kwishney!!
 
Back
Top Bottom