..BOT ilianzishwa kutokana na mtaji wa fedha za Tanganyika na Zanzibar tulizopewa na EA currency board.
Hapa ndipo ambapo Mzee Mtei angesaidia kusema Tanganyika ilichangia asilimia ngapi ya mtaji wa kuanzisha BOT na Zanzibar walichangia ngapi. Hii ingepunguza/ingezima malalamiko ya tunawagawia au tunanyonywa.
Nonda,
..Baada ya kusema hayo naomba unielekeze popote pale ambapo imehalaishwa kwamba Tanganyika ilipie gharama za umeme za Zanzibar, au tuwalipe mishahara SMZ, au tuchangie shughuli za muungano na Zanzibar wasichangie suala lolote lile, au wajumbe toka Zanzibar ktk tume ya katiba walipwe na serikali ya Tanganyika.
Kwa kutaka maelezo kutoka kwangu, umekusudia kutania? Kuchekesha wanajf? Au umekusudia kupandisha mizuka ya walio "bendera hufuata upepo"?
Shirika La umeme ni shirika la kibiashara au shirika la kugawa sadaka?
Je shirika la Umeme,TANESCO linaendeshwa kibiashara au kisiasa?
Nijuavyo ni kuwa TANESCO wanafanya biashara na Shirika la Umeme Zanzibar. Hapo kuna mkataba wa kibiashara. Anaeshindwa kutimiza masharti ya mkataba, apate adhabu. Mteja/mlalahoi ambaye halipi umeme anakatiwa umeme.
Sasa kama TANESCO wanawapa sadaka Shirika la umeme Zanzibar. Huo ni udhaifu wa TANESCO.
Kama Tanganyika analipia gharama za umeme za Zanzibar inawezekana ndio kilainisho/hongo ya kuwafanya wazanzibari wakubali serikali moja.
Mimi ningesema kila mtu ababe msalaba wake! Tanganyika ilipie gharama zake, Zanzibar walipie gharama zao na pale penye mambo ya muungano ndio walipie kwa pamoja.
After all, there is no free lunch!
JokaKuu,Nonda,
..Pamoja na hayo Zanzibar wakaanzisha tena PBZ ambayo toka wakati wa Karume mpaka utawala wa Salmini ndiyo walikuwa wanahifadhi fedha zao humo. Yaani PBZ ndiyo ilikuwa benki kuu ya Zanzibar kwa muda wote huo.
..Sasa suala hili lilishughulikiwa na msuluhishi wa kimataifa ambapo pamoja na mambo mengine alielekeza kwamba Zanzibar iwe inapewa hiyo 4.5% na zaidi ilazimishwe kuweka akiba yake BOT. Baada ya uamuzi huo ndiyo ukaona hata Zanzibar inateua Naibu Gavana wa BOT.
..Baada ya kusema hayo naomba unielekeze popote pale ambapo imehalaishwa kwamba Tanganyika tuwalipe mishahara SMZ
Hapo umeandika kuwa Zanzibar wameweka pesa zao BOT sasa wakitaka kulipa mishahara ya wafanyakazi wao inawapasa wachote kutoka hiyo akiba yao. Kama walilazimishwa kuweka akiba yao BOT na kuifanya PBZ isite kuwa benki ya serikali ya Zanzibar. Hizo pesa bila shaka zitatoka katika fedha zao zilizopo BOT au BOT wakiweka akiba ya mteja wake huwa hawarudishi pale mteja anapotaka sehemu ya akiba yake?
JokaKuuNonda,
..Baada ya kusema hayo naomba unielekeze popote pale ambapo imehalaishwa kwamba Tanganyika ilipie gharama za tuchangie shughuli za muungano na Zanzibar wasichangie suala lolote lile, au wajumbe toka Zanzibar ktk tume ya katiba walipwe na serikali ya Tanganyika.
Hapa ndio utaelewa kuwa sisi wabara(watanganyika) kuwa ni wadanganyika.
Bado hujaelewa kuwa hakuna hazina ya Tanganyika? Tanganyika haipo. Tanganyika haichangii chochote katika Muungano. Hazina ni ya muungano, serikali ya Muungano.
Wabara(wadanganyika) tunapata sadaka kutoka hazina ya muungano. kwa bahati ya werevu wa "wala urojo/mayakhe"
Wao wanapata kutoka hazina ya Zanzibar na hazina ya Muungano.
Kama tutaelewa somo la leo. maujanja ni kurejesha Tanganyika ,ili iwepo hazina ya Tanganyika, hazina ya Zanzibar na hazina ya muungano. Tumelikoroga sasa inabidi tulinywe tu, kaka!
Nafikiri baada ya Mwalimu kuona kosa lake alilolifanya juu ya kuua serikali ya Tanganyika, ndio aliamua afanye jitihada ya kuua serikali ya Zanzibar. Ndio ile janja ya serikali mbili kuelekea moja.
Lakini pia alijitengenezea njia nyengine kusema kuwa EAC ikizaliwa tena, ni vyema iundwe serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar iliyopo zijiunge EAC kama serikali zinazojitegemea. Hapa lilitokea G55 lililoanza kutoka usingizini na kuidai Tanganyika.
Tukiipata Tanganyika yetu na udanganyifu wa muungano tunaupatia dawa yake.
Je wadanganyika tutaendela kudanganyika au tutarudi Tanganyika?
JokaKuu
Hakuna serikali ya Tanganyika, in principle; serikali ya Muungano kama unavyosema wewe ni de-facto serikali ya Tanganyika lakini ukweli ni kuwa serikali ya Muungano ni monster tu, anatafuna Tanganyika, anatafuna Zanzibar.