Let opposition fight each other !!

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
If they hope to win more elections. Keep the opposition parties "at each other's throats" and play hardball.

Ndio tuonavyo vyama vingine vinaachana na CCM na kuivaa CUF ,kuanzia viongozi wake hadi kwenye vijiji vyake bila ya kufahamu kwa kufanya hivyo kunaipa mwanya CCM kuweza kutekeleza mbinu zake za wizi.Chadema wamepoteza lengo lilowekwa la kuachiana majimbo ambayo chama fulani kinapendwa na kuungwa mkono na badala yake kimekuwa kikigeula na kujiona kuwa kitashinda matokeo yake CCM wanapenya kirahisi.Chadema wameonekana kama ni ndumila kuwili na kwa hali ilipofikia imekuwa hakiaminiki tena katika siasa za kushirikiana ,tatizo ni pale Chadema inapojiona kuwa imekubalika au inakubalika na wananchi wengi bila ya kuona ukweli kuwa WaTanzania wamejigawa katika vyama karibuni vyote na inapotokea Chama husika na sehemu kuonekana kuwekwa pembeni basi hata wananchi wa sehemu ile huwa hawapo tayari kuunga mkono chama kingine,hivyo basi kuonekana kwa Chadema kujipeleka kifua mbele na baadae kupigwa kumbo na CCM inawafanya baadhi ya watu waone kuwa Chama hicho kinatumika katika kuwagawa wananchi na kuipa CCM nafasi kubwa ya kufanya hujuma za uchaguzi.ni lazima Chadema wajifunze kushirikiana kikwelikweli na kuweka tamaa kando ,kwani waswahili wanamsemo usemao tamaa mbele mauti nyuma na mauti haya si kwa Chadema tu bali kwa vyama vingine pia.
 
Kafu inakubalika Pemba na kwenye baadhi ya majimbo kidogo tu Unguja. Huko hatutakuja tutawaachieni. Wapi kwingine mnakubalika tuwaachie? Maana nijuavyo bara hamna jimbo mnalokubaliwa. Kama lipo litaje!
 
Back
Top Bottom