Let let (retreat) ya Rais Magufuli inaweza kuwa na afya kwa Taifa

superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
5,305
2,000
Wakatoliki hususan vijana ambao wako msingi na sekindari huwa wanahudhuria mafundisho ya dini kabla ya kupata komunio ya kwanza au kipaimara.

Kwa bahati mbaya sana huwa wanayaita let let ila kimsingi hushindwa kutamka retreat.

Ni kipindi kifupi kabla hawajapata hizo ekaristi.kimsingi ni kipindi cha kujidhili na kujitafakari mbele ya Mungu huku ukimuomba msamaha.

Let let na mh Rais Magufuli

Nakichukulia kipindi hiki cha mh rais magufuli kupata muda wa kukaa mbali na dar na dodoma kama kipindi cha kujifanyia self-evaluation.

Ni kipindi Cha kujitafakari na kujiboresha. Kwa yale anayolaumiwa nayo ndio kipindi cha kuyarekebisha yeye ni binadamu hivyo asione ubaya kujivua gamba la taswira tata ambalo aidha amevikwa au amejivisha.

Hivyo baada ya kuja Dar au Dom kwenye makazi yake nadhani atakuwa bora maradufu kuliko hapo kabla.

Washauri wake ndio dira ya taifa; pia wakiyumba, atayumba, tutayumba.

Good morning!
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
1,440
2,000
Uonavyo wewe ni vigumu mwingine kuwa kama uonavyo wewe na Wala haiwezekani na ndio maana kukawepo kitu kinaitwa UPINZANI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom