Less government ya Spika Ndugai naiona imekaa kisiasa zaidi, Serikali ndogo kwa sasa hatuiwezi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Nimeitazama ile video ya Mheshimiwa Job Ndugai inayotembea mtandaoni, anasema serikali ipunguze kuingilia kila kitu. Anatua maneno watu waachwe wajinafasi na sio kila wakipita wanakutana na mkono wa Serikali.

Kikatumika kingereza akisema maneno 'Less Government' akimaanisha kupungua kwa uwepo wa serikali kwenye kila kitu anachokifanya mtu. Lakini serikali kuwa ndogo kwa hao wazungu aliowatolea mfano kunamaanisha kitu kikubwa kuliko alichomaanisha yeye pale akiwa amekaa katika kiti chake.

Serikali ndogo ya Marekani kwa mfano inaambatana na wabunge kujihudumia karibu kila kitu kwa kutumia pesa ya mishahara yao wenyewe. Hata zile mamlaka zinazokuwa katikati ya mtu na serikali ni chache. Hawana masuala ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa mikoa na msururu wa vyeo wenye kwenda sambamba na malipo kutoka serikali kuu.

Wenye serikali ndogo hawana wabunge wa viti maalum ambao muda mwingi wanakuwa na ugomvi wa chini kwa chini na wale wabunge wenye majimbo yao, sababu ikiwa ni ile fitina ya kisiasa ya mbunge maalum kutafuta nafasi ya kulikamata jimbo.

Mara nyingi tu tunamuona waziri mkuu wa Uingereza, Canada au Australia akienda sokoni yeye mwenyewe na kufanya manunuzi kisha anapanda baiskeli kurudi nyumbani kwake, hiyo ni sehemu tu ya maana pana ya 'less government'. Sisi ni mwendo wa semina, warsha na makongamano ambayo ni chanzo cha mapato ya ziada ya wafanyakazi wa serikali, kuongelea udogo wa serikali katika mazingira ya aina hiyo nadhani ni kujaribu tu kupiga siasa za kupitishia muda.

Huko tuendapo tunaweza kuja kuwa na serikali ndogo zisizomuumiza mtu wa kawaida lakini ikiwa maprofesa wa vyuo vikuu na wao ni sehemu ya watafuta majimbo kinapofika kipindi cha uchaguzi sioni ni kwa namna ipi tunaweza kwa sasa hata kuongelea huo udogo wa serikali.

Ukubwa wa serikali unaambatana na urasimu unaodumisha umaskini wa mwananchi wa kawaida, unadumisha rushwa, ukabila, upendeleo na mambo kama hayo. Ukubwa wa serikali na ulaji unaoambatana nao ni chanzo cha yale makundi ya mitandao ambapo wenye madaraka wanataka wawaweke jamaa na marafiki zao katika nafasi zenye malipo mazuri.

Tukiweza kuondokana na dhana kwamba Serikalini ni mahali pa kwenda kuchuma ndipo tutaweza kuielewa maana pana ya udogo wa serikali. Kwa sasa ni vigumu kuwa wakweli tunapouongelea udogo huo wakati gharama za kuiendesha serikali ni kubwa.
 
Tatizo ni kwamba kwanini serikali ilazimishe kutia mkono kwenye kila kitu ambacho ikiona wananchi wanapata chochote hata kama haikushiriki kuwasaidia?

Mpaka vi-YouTube channel vya watu, serikali ikivyoona kuna vipesa vinapatikana ikaweka leseni uchwara kwa $900.

Na kwanini wakati huo huo watu wakililia msaada wa serikali iwasaidie kwenye kila kitu utawasikia, "kwanini mnasubiri na kulaumu serikali kwenye kila kitu"

Malizeni wenyewe, msisubiri serikali.
 
Small Government na Less Government interference ni vitu viwili tofauti sana...., Ingawa binafsi sioni merit hata ya a bigger government zaidi ya kumuumiza mlipa kodi
Spika alizungumzia less government interference lakini tunahitaji sana kuwa na Small Government siku zijazo, ni rahisi kupima ufanisi wa kila mtendaji na ni rahisi kufanya maamuzi mapema.
 
anasema serikali ipunguze kuingilia kila kitu
1622110415154.png
 
Ukubwa wa serikali unaambatana na urasimu unaodumisha umaskini wa mwananchi wa kawaida, unadumisha rushwa, ukabila, upendeleo na mambo kama hayo. Ukubwa wa serikali na ulaji unaoambatana nao ni chanzo cha yale makundi ya mitandao ambapo wenye madaraka wanataka wawaweke jamaa na marafiki zao katika nafasi zenye malipo mazuri.
1622116989537.png
 
Nimeitazama ile video ya Mheshimiwa Job Ndugai inayotembea mtandaoni, anasema serikali ipunguze kuingilia kila kitu. Anatua maneno watu waachwe wajinafasi na sio kila wakipita wanakutana na mkono wa Serikali.

Kikatumika kingereza akisema maneno 'Less Government' akimaanisha kupungua kwa uwepo wa serikali kwenye kila kitu anachokifanya mtu. Lakini serikali kuwa ndogo kwa hao wazungu aliowatolea mfano kunamaanisha kitu kikubwa kuliko alichomaanisha yeye pale akiwa amekaa katika kiti chake.

Serikali ndogo ya Marekani kwa mfano inaambatana na wabunge kujihudumia karibu kila kitu kwa kutumia pesa ya mishahara yao wenyewe. Hata zile mamlaka zinazokuwa katikati ya mtu na serikali ni chache. Hawana masuala ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa mikoa na msururu wa vyeo wenye kwenda sambamba na malipo kutoka serikali kuu.

Wenye serikali ndogo hawana wabunge wa viti maalum ambao muda mwingi wanakuwa na ugomvi wa chini kwa chini na wale wabunge wenye majimbo yao, sababu ikiwa ni ile fitina ya kisiasa ya mbunge maalum kutafuta nafasi ya kulikamata jimbo.

Mara nyingi tu tunamuona waziri mkuu wa Uingereza, Canada au Australia akienda sokoni yeye mwenyewe na kufanya manunuzi kisha anapanda baiskeli kurudi nyumbani kwake, hiyo ni sehemu tu ya maana pana ya 'less government'. Sisi ni mwendo wa semina, warsha na makongamano ambayo ni chanzo cha mapato ya ziada ya wafanyakazi wa serikali, kuongelea udogo wa serikali katika mazingira ya aina hiyo nadhani ni kujaribu tu kupiga siasa za kupitishia muda.

Huko tuendapo tunaweza kuja kuwa na serikali ndogo zisizomuumiza mtu wa kawaida lakini ikiwa maprofesa wa vyuo vikuu na wao ni sehemu ya watafuta majimbo kinapofika kipindi cha uchaguzi sioni ni kwa namna ipi tunaweza kwa sasa hata kuongelea huo udogo wa serikali.

Ukubwa wa serikali unaambatana na urasimu unaodumisha umaskini wa mwananchi wa kawaida, unadumisha rushwa, ukabila, upendeleo na mambo kama hayo. Ukubwa wa serikali na ulaji unaoambatana nao ni chanzo cha yale makundi ya mitandao ambapo wenye madaraka wanataka wawaweke jamaa na marafiki zao katika nafasi zenye malipo mazuri.

Tukiweza kuondokana na dhana kwamba Serikalini ni mahali pa kwenda kuchuma ndipo tutaweza kuielewa maana pana ya udogo wa serikali. Kwa sasa ni vigumu kuwa wakweli tunapouongelea udogo huo wakati gharama za kuiendesha serikali ni kubwa.
Ndugai hafai kuwaasa watanzania ni mtu asiye na maadili.
 
Back
Top Bottom