Leseni Mpya: Changamoto, Mafanikio, Kushindwa, Dili na mifano binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leseni Mpya: Changamoto, Mafanikio, Kushindwa, Dili na mifano binafsi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Igwachnya, Jan 13, 2012.

 1. I

  Igwachnya Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Zoezi la kutoa leseni mpya bado linaendelea. Hapa kati kati kumetoa mengi, kwa mafano kupanuka kwa mianya ya rushwa, polisi wa usalama barabarani kupata dili, mafanikio kwenye kupunguza ajali za barabarani na mengine mengi. Lengo langu hapa ni sisi kujadiliana na kushare mambo tuliyokutana nayo kwenye leseni mpya, tujue na kujifunza nini kimeenda vibaya na nini kimeenda kama ilivyotarajiwa. Na inapobidi tupeane michongo wapi leseni za magumashi zinapatikana, zinapatikanaje na kwa gharama gani.

  Mimi nitaanza na hadithi yangu
  Tarehe 23/12/2011 nilienda pale my fair kupadilisha leseni yangu ya class D. Nilikaa kwenye foleni kwa zaidi ya masaa 8 na baadae nikafanikiwa kupiga picha na kuchukuliwa finger prints. Toka wakati huo hadi leo sijafanikiwa kupata leseni yangu, nimeenda pale zaidi ya mara nane nikawa naambiwa leseni yako bado. tar 10/1/2012 nilipoenda nikaambiwa bado sijalipia. nikawaonesha Bank deposit slip ya bank ya posta wakaniambia eti imekosewa namba waliyoandika pale sio ya kwangu... So ikanibidi kurudi bank kuomba kubadilishiwa, bank wakaniambia wameshabadilisha so nikachukue leseni yangu ijumaa tar 13/01/2012. Nilipoenda wameniambia bado inaonesha waiting for payments. Niliporudi bank wakajifanya wanashangaa shangaa na wakaniandikia slip mpya kwamba wamesharekebisha so nikachukue leseni yangu jumatano tar 18/01/2012.....

  Hii ni kuhusu leseni yangu bado leseni ya wife (its another good corruption story)
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu pole sana, lakini niweke sawa hapa shida ni bank au polisi na leseni ?
   
 3. I

  Igwachnya Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  kwa kesi yangu kuna shida mbili. Shida ya kwanza ni bank na shida ya pili ni maafisa wa TRA Wanaohusika na leseni. Walishindwaje kujua dosari kwenye slip yangu mapema?
  Lengo langu hapa ni kujadili changamoto zote zinazohusiana na leseni mpya. Hata polisi nao wanamchango wao kwenye hili. Ngoja tuendelee kusikiliza.
   
 4. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi nilikwenda mtwara tarehe za mwanzo mwezi wa kumi na mbili.ilinichukua siku 4 kukamilisha taratibu zote huku nikila gesti na kulala hotel,cha ajabu nikaambiwa mashine mbovu nifuatilie baada ya siku 3 au kama natoka mbali niagize mtu kunipokelea,ni hadith ndefu lakini kwa kifupi mpaka leo hii sijaipata leseni na wala sijui nitaipata lini au ndo nimetapeliwa tayari!na ukija barabarani askari ndo hawashikiki kazi hazifanyiki.hivi serikali ilijiandaa kweli ktk mpango huu au ni yale yaleeee!oko,speed limiter nk ktk harakati za wakubwa kutunisha matumbo?kwa nini iwe kero na usumbufu kama nia yao ni njema kweli?nchi hiii!
   
 5. M

  Masuke JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mimi nilivyoenda siku ya kwanza nilikuta foleni ndefu nikaamua kurudi, siku ya pili nilikaa foleni zaidi ya masaa matano, nikafanikiwa kupiga picha, kuweka alama za vidole na sahihi, netwoki ikawa imekata, nikaambiwa njoo siku nyingine, ijumaa last wiki nilivyoenda nikapangiwa madaraja na kupewa karatasi kwa ajili ya kwenda beki kulipia, benk napo nikaambiwa mtandao wa TRA uko chini, na jumamosi stori ikawa ni hiyo hiyo, hivyo nililazimika kwenda j/tatu ya tarehe 09 nikafanikiwa kulipia, leo ijumaa nimeenda kwa ajili ya kuchukua leseni nikaambiwa leseni yako bado hadi alhamis next wiki. Kiukweli huu utaratibu unachosha sana.
   
 6. wizaga

  wizaga Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo lenu nchi hii hamjaielewa,inavyoonekana hamsomeki.rushwa inahitajika wenzenu wanaotoa hawatumii siku zote hizo wala vikwazo hakuna ni kati ya tsh 60,000 80,000 na 300,0000
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kilasehemu imeoza. Nchi hii bana!!
   
 8. I

  Igwachnya Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hapo mkuu umenena. Baada ya usumbufu ulionikumba mimi nikaamua kumfanyia wife mchongo wa leseni. Wife hajui hata kuendesha gari. Bt nilitoa 150000 na akapata leseni yake baada ya siku tatu. Siku ya kupiga picha na finger print alipigiwa sim na kwenda moja kwa moja bila kupanga foleni. Kweli nchi imeoza, inanuka.
   
 9. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi sijabadili leseni yangu hivi utaratibu ni upii? I hope ntafanya kama nlivyofanya kuipata Tz bwana teh teh
   
 10. I

  Igwachnya Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  kama sikosei, utaratibu ni kwamba unaenda ofisi zinakotolewa leseni mpya unajaza form (kuna siku form zinakuwa zimeisha.) ya taarifa zako then unaikusanya ambapo utapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole utaenda kwa trafik polisi watacheki leseni yako ya zaman kisha unapewa form ya kulipia bank, unaenda bank unalipa 40000 then unatakiwa kupewa leseni yako after 3 days. (unatakiwa kuwa na tin No, kama hauna kuna watu wa TRA wanatoa hapo hapo..
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nimesoma thread yote inasikitisha sana. Mi nilitarajia zoezi hili litaongeza integrity kwenye leseni zetu. Ndiyo maana ukienda nchi za watu hawakukubalii kuibadili leseni yako ili uendeshe huko wanataka uanze upya mchakato kama 'Learner'.

  Hivi issue sensitive kama hizi usalama wa Taifa wapo wapi?, Leseni zinagawiwa kama njugu kwa kubadilisha na pesa?. Wenzetu ambavyo huwa wanafanya ukiihs qualify kupata leseni unapewa certificate wakati ukisubiri leseni yako. Certificate hiyo unatembea nayo na kuendesha kama kawaida traffic akikusimamisha unamuonesha anachukua namba na tarehe wewe unaendelea na safari zako.

  Kwa nini Traffic wanahoji kuhusu leseni wakati watu wanacheleweshewa makusudi?. Haya ndiyo matatizo ya kuwa na viongozi wanaoingia madarakani kwa rushwa, rushwa. Hawajali integrity ya serikali zao zaidi ya kujilimbikizia tu. Ningekuwa mimi waziri muhusika malalamiko haya yangekuwa uthibitisho tosha wa kufuta leseni zote zilizoisha tolewa mpaka sasa na kuwawajibisha wahusika wote na mchakato kuanza upya. Watu wanakaa maofisini kusubiri mshahara na posho wakati serikali inazidi kuoneka IMEOZA kwa ajili ya wapuuzi wachache wanaoona kila kitu ni dili.

  Shame shame shame shame! on all those who are responsible.
   
 12. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Je, kwa sasa huwezi kutumia leseni ya zamani? kwani inavyoonekana kuna urasimu sana kupata hiyo leseni mpya. (BTW mimi, mwaka na nusu sasa nipo safarini nje ya nchi)
   
 13. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu yangu ilichukua siku 3, kwa sh 120,000/-, kwa Madaraja A, B & D, af kipindi hicho sijui hata break inakaa upande gani na nikaletewa hadi nyumbani
  Tatizo ukifata njia halali usumbufu unakuwa mkubwa mno
   
 14. I

  Igwachnya Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Leo nimeenda kufuatilia leseni yangu pale my fair.... Baada ya mihangaiko mingii ya hapa na pale na kusubiri kwa mda mrefu ikabidi nimpe 2000 dogo fulani yumo mle ndani, (sidhani kama amefikisha miaka 20) ili anitafutie leseni yangu haraka. Haikuchukua hata dakika tatu nikawa nimeshapewa leseni yangu niliyoifuatilia kwa muda unaokaribia mwezi mmoja..... kesho nitawaonesha leseni yangu mpya na makosa yaliyopo kulinganisha na fomu niliyojaza.
   
Loading...