Les Wanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Les Wanyika

Discussion in 'Entertainment' started by Rabin, Jan 29, 2010.

 1. Rabin

  Rabin Senior Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wadau naomba mnisaidie majina ya lile kundi zima lililowika la hawa jamaa wa Les Wanyika maana kuna VCD naziona mitaani zina jina moja tu la mwanamuziki mtunzi anayeitwa Tom Malanga, nina shaka kama ni wenyewe au kuna kikundi kimefanya video kwa kutumia nyimbo hizo?
   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Rabin,ni kweli Tom Malanga alikuwa mwanamuziki kiongozi wa Les Wanyika.Unajua Les Wanyika ilianzishwa mwaka 1978 na wanamuziki wawili Tom Malanga(mpiga gitaa la besi) na Omar Shaban(Professor Omari-mpiga gitaa la solo) waliojiondoa katika bendi ya Simba Wanyika(huku waliwaacha ndugu wawili George na Wilson Kinyonga)..Baadaye waliongezeka John Ngereza na Issa Juma(waimbaji) kisha mwaka 1979 walianza kuwa moto wa kuotea mbali kwa kutoa nyimbo ambazo kwa kweli zilihit katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati,Nyimbo hizo ni ka Sina Makosa,Paulina,Pamela,Wazazi n.k

  Wanamuziki wengine waliounda Les Wanyika ni pamoja na Rashid Juma(drums) na Elias John(Saxaphone)

  Itaendelea......
   
 3. Rabin

  Rabin Senior Member

  #3
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nashukuru mkuu Balantanda, nimeanza kupata picha ya kundi, kama utaiona ile VCD yenye nyimbo za Pamela,wazazi,afro,kasuku,barua yako, amigo na maisha ni mapambano ningeomba unisaidie kuwajua wale washiriki wa ile albam, thanks mkuu.
   
Loading...