Leonardo da Vinci alimaanisha nini katika picha hii? Nani alizunguka dunia kusambaza hii Teknoloji miaka ya BC?

Ngamia ndiyo upande uzungukie dunia?
Mleta mada kaleta picha fikirishi zenye kufanana, ukichukulia enzi hizo hapakuwa na teknolojia ya mawasiliano kama ilivyo leo.
Kwanini urahisishe jibu kwenye swali gumu?
Mkuu ukitaka Mtanzania ajibu logically na rationally utapata jibu siku jua likianguka. Una bahati hujapewa jibu la Mungu ndiye anajua. We are very simple people.
 
Hapana mkuu..

Kwa mujibu wa wazee wa conspiracy,
Picha inaonekana ni wakati wa mtafaruko ulio tokea baada ya Yesu kusema kuna mmoja atamsaliti

Wanafunzi wakamwambia yule MWANAFUNZI ALIYE PENDWA SANA amuulize Yesu ni nani huyo atakaye msaliti?

Lakini kwa mujibu wa picha ya Vinci anaye pewa jukumu ni Magdalena na sio Yohana kama wengi tujuavyo
 
SALUTE COMRADES

Hii mijengo hapa chini ni mijengo iliyojengwa miaka mingi zaidi kabla ya Kristo, enzi hizo teknolojia ya usafiri ilikua chini!

Swali ni je, nani aliyezunguka bara moja kwenda lingine kusambaza hii teknolojia?

Ikumbukwe mpaka leo hii mzungu hajaweza gundua haya majengo yalijengwa vipi. Yapo bara la Africa, Asia na America.

View attachment 750214

Pia tujiulize kwanini yote yamejengwa na milango mitatu na mmoja mkubwa wa katikati? Nini maana yake? Nini maana ya namba 3?

Leonardo Da'Vinci katika mchoro/picha yake inayofahamika kama The Last Supper, pia ameweka hiyo milango mitatu!

View attachment 750215

What does it mean?

Cc
Palantir zitto junior Malcom Lumumba Astelia
Mkuu Da'Vinci kumbuka mafundi wa babeli walitawanyika na kwenda shm mbalimbali, pia haohao ndio chimbuko ya lugha zote. So hio inaonesha walisambaa dunia nzima. Ujenzi wa aina hio ni wao ndio waliusambaza na ndio maana hayo majengo yalijengwa miaka ya zaman sana
 
si ndo fashion ya miaka hiyo... na pia watu walikua wakisafiri kama mnavosafiri sasa hivi.. si ngamia walikuwepo...

vitu vingine nahisi tunavipaga uzito usiostahili, tunavitafutia Hidden secret ambazo hazi exit
Story zetu za kuchangamsha vijiwe vya kahawa,tunapigana kamba sana kwenye hivi vijiwe uzushi mwingi alafu kila mtu anajua.
 
Ni ngumu kujadili kazi za Like Leonardo da Vinci bila kumjua yeye mwenyewe ni nani....

Leonardo Da Vinci (Vinci, Toscana, Italia, 15 Aprili 1452 – Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipaji vingi[1] kutoka nchini Italia.

Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifuujenzi, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi.

Ndiye mwakilishi bora wa tapo la Renaissance.

Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.

Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".

Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.

Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli, kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya jua kuwa umeme.

Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani ni Mona Lisa na Karamu ya mwisho.

Mchoro mwingine unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro.
To be continued.....
 
Leonardo da Vinci


Leonardo da Vinci alivyojichora.
Leonardo Da Vinci (Vinci, Toscana, Italia, 15 Aprili 1452Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipaji vingi[1] kutoka nchini Italia.
Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifuujenzi, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi.
Ndiye mwakilishi bora wa tapo la Renaissance.
Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.[2]
Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".
Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.
Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli, kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya jua kuwa umeme.
Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani ni Mona Lisa na Karamu ya mwisho.
Mchoro mwingine unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro.

Maisha

Utoto, 1452–1466

Mchoro uliojulikana awali wa Leonardo, Arno Valley, (1473) - Uffizi, Florence, Italia.
Leonardo alizaliwa tarehe 15 Aprili 1452, mkoani Toscana, katika mji mdogo wa kilimani wa Vinci, katika mabonde ya Mto Arno, karibu na Florence nchini Italia.
Babu yake, Ser Antonio, anajivunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwa hawajaoana. Baba yake alikuwa mwanasheria, Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci.[3][4] Mama yake, Caterina, alikuwa mhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutoka Mashariki ya Kati.[5][6] Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".
Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba ya shambani na mama yake. Halafu akaja kuishi Vinci na baba yake, mke wa baba yake aliyeitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco.
Wakati Leonardo ameshakua, aliandika vitu viwili tu kuhusu maisha yake ya utotoni. Alikumbuka kwamba alivyokuwa amelala kwenye kitanda chake cha watoto nje ya nyumba yao ndege mkubwa alikuwa akipaa na kumzungukazunguka juu yake. Mikia yake ikawa inamfutafuta sura yake.[7] Kumbukumbu nyingine muhimu ya Leonardo ilikuwa vipi aligundua pango milimani wakati anapeleleza. Alikuwa na hofu kubwa sana huenda kukawa na kiumbe kikubwa cha ajabu kimejificha mle ndani ya pango. Lakini pia alikuwa na hamu na shauku ya kujua kilichopo mle ndani.
Giorgio Vasari aliandika kuhusu maisha ya Leonardo kwa ufupi baada ya kifo chake. Ameelezea hadithi za kuvutia kibao kuhusu utundu aliokuwa nao Leonardo. Anasema kwamba Leonardo alichora bamba la taarifa la mbao-mzunguko likiwa na picha ya mijoka inayotema moto. Messer Piero alichukua michoro ya mwanawe hadi Florence na kuiuza kwa wauzaji wa bidhaa za kisanaa.[8]
Ujana na utu uzimaEdit

Ubatizo wa Kristo kadiri ya Verrocchio na Leonardo (1472–1475) — Uffizi.
Leonardo alianza kuchora tangu yungali bado kijana. Alifunzwa usanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio.
Sehemu kubwa ya maisha yake alimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Italia.
Mwaka 1516 Leonardo alikwenda Amboise, Ufaransa, baada ya kupata mwaliko kutoka kwa mfalme Fransisko I. Kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu wa Monalisa.
Leonardo aliishi mjini Amboise, katika nyumba yake nzuri aliyopewa na Mfalme huyo wa Ufaransa, miaka yake ya mwisho, toka mwaka huo mpaka mwaka 1519.
Afya yake haikuwa nzuri kwa sababu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517, lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.
Kifo
Alifariki huko Amboise tarehe 2 Mei 1519 akiwa na umri wa miaka 67, akazikwa St. Hubert.
 
mkuu usijifanye hujanielewa, muingiliano wa watu unatokana na kusafiri kutoka sehemu moja mpaka ingine, na hao wa sehemu hio mpaka ingine tena.. ndio maana kuna watz wako australia wako brazil etc....

waliotoka hapa walifika congo wakongo wakaenda SA wa SA wakaenda kwingine huko wakichukua tamaduni za hapa na pale...mpaka zikafika huko.
maswali tunayafanya wenyewe yawe magumu ... ila yanaweza kuwa mepesi ukitaka. maana hizo siri tangu zimeanza kusemekana sijawahi kuzisikia zimefahamika maana mnaoumiza vichwa mko wengi

Nakuelewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom