Leon Spinks alifungwa mkono wa kushoto ili apambane na Mohammad Ali?

kitonsa

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
1,211
2,636
Kuna story za kitoto mida ya miaka ya nyuma huyo mwamba alikuwa na nguvu mpaka Mohamed Ali aliomba afungwe mkono wa kushoto.

Nilisikia alifungwa mkono wa kushoto, alivyo fungua alivunja nondo ya ring.

Kuna ukweli hapa?

2505295_Screenshot_2020-09-02-03-29-13.jpg
 
Wazee wa Zamani walikuwa waongo sana sijui kwanini, au kwa vile zamani ilikuwa ukidanganya ni ngumu MTU kutafuta ukweli ni UPI?No google, no you tube , TV changamoto, intaneti hakuna.Angalia pambano hilo
 
itabid atafutwe muasisi wa hio story manake naikumbuka kabisa
Wazee wa Zamani waongo sana, Utasikia kina Gibson Sembuli walikuwa wakichana nyavu, Nyavu zenyewe za katani sijui zimeoza hazina ubora.Eti Kuna mchezaji gani sijui Alikuwa anapiga Kona halafu anaiwahi mwenyewe anakuja kufunga kumbe unaweza kukuta alipiga kona akawahi sekeseke golini akafunga, kingine eti Golikipa Omary Salehe Ombopa alikuwa ana uwezo wa kugeuka hewani, eti anaruka kulia akiwa hewani anajigeuza anarudi upande wa pili.
 
nahis hizi habar zao ndo zimetufanya tukawa wabovu wamambo ya hesabu na physics
 
Wazee wa Zamani waongo sana, Utasikia kina Gibson Sembuli walikuwa wakichana nyavu, Nyavu zenyewe za katani sijui zimeoza hazina ubora.Eti Kuna mchezaji gani sijui Alikuwa anapiga Kona halafu anaiwahi mwenyewe anakuja kufunga kumbe unaweza kukuta alipiga kona akawahi sekeseke golini akafunga, kingine eti Golikipa Omary Salehe Ombopa alikuwa ana uwezo wa kugeuka hewani, eti anaruka kulia akiwa hewani anajigeuza anarudi upande wa pili.
Haahaaahaaaaaaa...
Hizo story zote nilikumbana nazo udogoni
mwishoni mwa miaka ya 80 nikiwa shule ya msingi.
Kuna braza wa zama hizo kitaa alikuwa akishatoka kwenye mishe zake anatukusanya 'madogo' na kuanza kutulisha hayo 'madini' pamoja na mamovi ya mbele ya kina Freddy Williamson,basi tulikuwa tunamkubali msela balaa.
Namkumbuka sana yule 'braza' nikiwa naitazama movie ya kihindi ya Sholay zama hizi za utu uzima wangu,kwani alichonisimulia yeye na nilichokuja kukiona kwenye hiyo muvi sasa dahhhh!.
 
Back
Top Bottom