Leodegar Tenga ajitosa kugombea nafasi ya rais wa Cecafa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,847
Posted Date::10/30/2007
Leodegar Tenga ajitosa kugombea nafasi ya rais wa Cecafa
Na Sosthenes Nyoni
Mwananchi

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametangazwa rasmi kuwania nafasi ya uenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) katika uchaguzi utakaofanyika Desemba 7.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Hoteli ya Millenium Towers jijini Dar es Salaam jana , Makamu wa Rais wa TFF, Crescentius Magori alisema kuwa jina la Tenga lilipendekezwa na kamati ya utendaji ya shirikisho hilo katika kikao kilichoketi jijini Dar es Salaam Februari mwaka huu.

Alisema kuwa baada ya Tenga kupewa taarifa juu ya mapendekezo hayo aliomba apewe muda wa kutosha ili aweze kutafakari na ndipo hivi karibuni alipokubali ombi la kamati hiyo.

“ Kamati ilikaa na kuona kuwa Tenga anaweza kusaidia kuiimarisha (CECAFA) hasa baada ya kuona ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na hasa ukiangalia mambo mengi mazuri aliyoyafanya ndani ya TFF” alisema Magori.

Alisema kwa kumweka mtu madhubuti kama Tenga pia kutaleta mabadiliko na kuifanya Afrika Mashariki kuwa Kanda Bora na kuondoa dhana ya kanda nyingine ya kwamba kanda hii ni sehemu ya kuvuna pointi.

Aliongeza kuwa ili kuhahikisha Tenga anachukua nafasi hiyo pia wameitaarifu Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo juu ya uteuzi huo na kuiomba isaidie kutafuta uungwaji mkono kupitia balozi zilizoko nchi wanachama wa Cecafa.

Kwa sasa, Cecafa iko chini ya uongozi wa rais wake, Denis Obua kutoka Uganda na katibu wake, Nicolaus Musonye ambaye ni raia wa Kenya.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom