Leo wakazi wa Kigamboni tumekomeshwa, Kivuko kimoja tu kinafanya kazi


Nadhani hili lafaa kufanyiwa kazi. Kwamba Pantoni likiwa Moja magari yote yapitie Darajani. Na pia muda wa Pick time ya watu kuwa wengi Magari hivyo hivyo ya pitie Darajani.

Muda mwingine tunadharaulika kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu isipokuwa tunalaza bongo bure
Tatizo kubwa ni kuwa uongozi huwa hautoi taarifa zozote kwa wenye magari kama kuna shida. Sijui wale askari wa SUMA JKT na wafanyakazi wengine wanafanya kazi gani. Mwenye gari anapanga foleni saa nzima na mkatisha tiketi anamkatia, yaani inashangaza hata mkatisha tiketi anakuwa hana habari ya kinachoendelea.

Vv
 
Watanzania tunapenda kulalamika sana,kwanini msipite darajani?
Kuwaga na akili we...kwa MTU anaekwenda posta kazin hana private care inamchukua almost 1 hour na zaidi akipitia darajani ....ila akitumia kivuko ni dakika 15 kashafika mjini.....

Afu uwezi kusema analalamka kwasababu ni wajibu wa serikali kutengenza miundombinu yetu
 
Si mnasema huku ni shithole sasa nendeni kwa huyo Trump au Mange
 
Leo tarehe 18.1.2018 wakazi wa Kigamboni tumeisoma number kwa kirumi ni baada ya usafiri wa pantoni kusumbua.hapa ferry kuna pantoni tatu lakini kwa siku ya leo inayofanya kazi ni moja tuu.tena ile ndogo imezidiwa kwa kweli watu ni wengiii imebidi iwe inachukua abiria tu na kuwavusha huku wenye magari wakiachwa waisome number vizuri.ni vilio kwa wafunzi kwa huo mkanyagano aisee.tunaomba serikali mtusaidie jamani hivi viwili vifanye kazi kabla maafa hayajatokea kwa kivuko kuzidiwa.

Bahati mbaya nimeshindwa kuweka picha kwa usalama wangu na kwa mapenzi ya simu yangu.tumekatazwa kuchukua picha.napenda kuwashukuru wanajeshi wa leo pale ferry kwa kuweza kuwapanga raia la sivyo leo yangekuwa mengine.

========

View attachment 678488

Pichani ni wananchi wakigombania kupanda kivuko cha MV KAZI mapema leo.
 
Back
Top Bottom