Leo twendeni kigamboni ... Na swali zima kwa nini wahusika wamelisahau eneo hili?

Mimi nadhani ni aina ya watu waishio huko pamoja na kipato chao ndiyo sababu ya hizo appearance za ajabu ajabu. Inawezekana wadosi walichelewa kuweka makazi yao Kigamboni, hivyo maeneo ambayo yalishikiliwa na akina sisi yamebaki na hali kama inavyoonekana.
 
Wavuvi huwaga hawana maendeleo hasa huu wetu mdogo mdogo wa kuganga njaa ila kumbuka kuna a lot of beaches ukienda mbele na watu wamefumua mahekalu izo nyumba uzionazo ni za wenyeji ambao mtu akiwa na dau anawahamisha ingawa nao wabishi sometimes
 
Toneradio usijali, Kigamboni ni lazima paendelee. Serikali imeweka mpango mkakati wa nguvu kuhakikisha kuwa Kigambo linakuwa jiji la mfano ifikapo 2030. Hebu jionee mwenyewe kwa kufuata link hii: http://bit.ly/9s0rUv
 
Toneradio usijali, Kigamboni ni lazima paendelee. Serikali imeweka mpango mkakati wa nguvu kuhakikisha kuwa Kigambo linakuwa jiji la mfano ifikapo 2030. Utekelezaji wa mpango huu tayari umekwisha anza, usijali ni rahisi mno!

Hebu jionee mwenyewe kwa kufuata link hii: http://bit.ly/9s0rUv
 
Pia huduma mbovu za pantoni ni kero nyingine....
Kipindi fulani nilifululiza kwenda huko nikagundua kwamba suala la foleni kuingia kwenye gati la kusubiria ferry inategemeana na hekima/busara ya dereva. Polisi huwa wanaangalia senema ya bure ya magari kuchomekeana na hata lile banda la kusubiria abiria ni mkusanyiko wa matatizo hasa magonjwa ya kuambukizana....


 
NIMEKUA NIKIJIULIZA SANA HIVI HUKU KIGAMBONI KWA NINI KUMESAHAULIKA SANA BILA KUPATA MAJIBU. SASA WADAU NAOMBA TUCHUKUE MUDA KUTAZAMA TASWIRA HIZI ZA HAPA ZA KIGAMBONI LABDA MTAKUA NA MAJIBU MAZURI

BOFYA HAPA KWENDA KIGAMBONI
Mkuu naona huijui kigamboni kabisaaaaaaaaa

ningependa upite kisota, kibada, ras kutani, geza, machava, mjimwema na hata maeneo ya kwa mwingira ujue unaongea nini

Hizo picha ukiangalia zote ziko karibu zaidi na ikulu kuliko na wakazi halisi wa kigamboni...

Kuhusu ferry kama alivyosema PAW ile ni disaster which could be avoided kama pasingekua na petty corruption ya maaskari wanaokula alfu mbili-mbili (pande ya kigamboni), mia tano (pande ya magogoni - hawa ni polisi), madereva wavivu wa kujali, na wanaoongoza vivuko hasa mainjinia na makepteni kwani wanadelay maksudi ili wafaidike na mafuta au kudai maipo yao (it is uhujumu uchumi really - if you look at the definition)

hebu pata picha moja ya maeneo ya kigamboni si vibaya kuona kwanini vijana wengi wanenda kujenga kule

TATIZO NI HABBITUAL POOR PLANNING
 
Hii nilikua naonesha taswira ambazo zipo mwanzo kabisa unapo ingia kigamboni ukitokea kivukoni ... Tukumbuke macho ya watu hujaji tangia mwanzo..sasa umeona hilo dude la taka limesha oza kabisa.. Lakini wahusika wanapita kila siku hapo je hawaoni?
 
Back
Top Bottom