Leo tuomboleze jamani...ila kesho kila mtu arudi kwenye zamu yake!!!

kuti kavu

Member
Joined
Feb 25, 2009
Messages
68
Points
95

kuti kavu

Member
Joined Feb 25, 2009
68 95
Ni matumaini yangu kuwa asilimia kubwa ya wadau wa forum hii si watu wanaofuata mkumbo wa kiitikadi za kichama au kisiasa pekee, bali ni watu wenye kuguswa na maisha duni anayoishi Mtanzania wa kawaida. Na kama imani yangu ina ukweli ndani yake ni wazi mioyoni mwetu tuna wahukumu viongozi wa nnchi yetu si kwa sababu ya vyama walivyotoka pekee ila kwa utendaji wao na utekelezaji wa majukumu waliyotumwa kuyatekeleza na wananchi.

Mchakato wa kuwatafuta viongozi wa miaka mitano ijayo umeshamalizika rasmi leo...kwa sisi tunaouguswa na mendeleo ya mtanzania kwanza na si ushabiki wa kukaririshwa pekee, kwa kiasi tuna furaha kwamba angalau idadi ya viongozi tuliokuwa tunawatilia mashaka wamepumzishwa rasmi kwa nguvu ya wananchi...na ni wazi kila mmoja wetu anaamini Bunge letu na pia serikali za mitaa zitakuwa za kitofauti safari hii kutokana na damu mpya ya madiwani na wabunge ambao (tuna imani nao) iliyopenyezwa na wananchi katika vyombo hivi...TUNA HAJA YA KUJIPONGEZA KATIKA HILI!!!

Lakini pia kuna maeneo ambayo lazima tukubali tulianguka , na hii inatupa sababu ya kuumia, kulia na kulalama. Lakini pia tukumbuke vita hii ya kumkomboa mtanzania hatukutegemea tutaishinda kwa usiku mmoja....jambo la kushukuru ni kuwa tumepiga hatua kubwa kuelekea Ushindi....Kwa hiyo tulie, tunung'unike, tuumie....baada ya hapo tunyanyuke na kuendeleza mapamabano.

Ombi langu kwa wenzangu tunaoguswa na umaskini na ufukara wa wa Tanzania, safari hii tuanze mapema, tuanze mapema kuwafumbua macho wenzetu juu ya umuhimu wa kuchagua viongozi kutokana na uwezo wao kiutendaji, tuwatoe ile hofu kuwa kuwakataa wale waliowazoea (hata kama ni wabovu) kutatutumbukiza katika matatizo....tuwashirikishe elimu ya uraia, na tujitahidi kuwaanika wale wasiofaa...kwakifupi pale tulipoanguka pasitukatishe tamaa bali tupageuze kuwa chachu ya kujiandaa kwa ubora zaidi kwa raundi inayofuata.

Dawa ya kupambana na mamba si kujifunza kuogelea nae, bali ni kumkaushia maji ya dimbwi la maji anamoishi..na idadi ya viongozi bora tulio waongeza na ile ya wabovu tuliowaondoa ni sawa na idadi kubwa ya ndoo za maji ambazo tayari tumezipunguza toka dimbwini kwa mamba...Tusikate tamaa, tujiandae kuyakausha zaidi maji yao safari ijayo...ila kwa sasa kila mtu ana haki ya kuomboleza pale tulipo umizwa...kwa sababu kesho asubuhi, kila mtu anatakiwa ashike zamu yake kuendele na mapamambano ya ku momboa mTanzania.

Ila leo...ngoja na mimi niomboleze kwa yangu....:A S cry:
 

Forum statistics

Threads 1,392,161
Members 528,552
Posts 34,100,321
Top