Freeman Mbowe: Kupona kwa Mhe. Lissu ni Mpango wa Mungu, Watanzania tuendele Kumuombea

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kupona kwa Mhe. Lissu ni mpango wa Mungu, nawaomba Watanzania wenzetu waendelee kumuombea kwa Mungu pamoja na kuchangia gharama za matibabu, kwa kuwa gharama zake ni kubwa ambazo chama pekee hakiwezi kuzimudu bila ya misaada kutoka kwa watu mbalimbali.

Unajua ahueni humtokea mgonjwa taratibu taratibu na ndivyo inavyotokea kwa Lissu, ingawa sisi wote tuna hamu apone mara moja aje aendelee kupigania haki za wanyonge kama alivyokuwa akifanya.

Sisi tunatoa taarifa za maendeleo ya Lissu kulingana na Madaktari wanavyotuambia, hatuwezi kusema chochote nje ya wataalam hao, kwa kuwa ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua maendeleo ya mgonjwa husika.

UPINZANI NI KAZI NGUMU Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.

Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.

Huwezi kuendesha nchi bila kuruhusu ukosoaji, iwe kutoka upinzani au kwenye chama unachokiongoza, unapowazuia watu wasipumue na kutoa madukuduku yao, unatengeneza hasira kubwa ndani ya jamii.

Mwanahabari Huru

Mbowe.jpg
 
Lisu atapona tu,Mungu ndie aliemfikisha hapo alipo.Mungu wetu ni mwema hawezi kutuumiza kiasi cha kwamba na yeye anakadi ya Ccm.
Lazima atende maajabu ili ukoo wa Sizonje na Bashite waaibike mbele yetu.
 
Ugua pole TL.
Mbowe inabidi afahamu kitu kimoja,kama mabalozi wenyewe wakienda ikulu wanakunywa juisi na pipi,maana yake huko wapinzani hamna tena zile zama za kwenda kunywa maziwa na cocoa ikulu ,hela zote zinaenda kwenye miradi.
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Ongeza maombi Lissu apone, changia kadri uwezavyo, gharama za matibabu usilinganishe na kununua visheti.
Jiepushe kuonyesha maambukizi ya chuki za wamiliki wa smg.
 
Ugua pole TL.
Mbowe inabidi afahamu kitu kimoja,kama mabalozi wenyewe wakienda ikulu wanakunywa juisi na pipi,maana yake huko wapinzani hamna tena zile zama za kwenda kunywa maziwa na cocoa ikulu ,hela zote zinaenda kwenye miradi.
Miradi yenyewe haipo!
Wakandarasi wapo hoi!
Kama huamini we tangaza kandarasi ya kufukuza na kumkamata kuku. usishangae utitiri wa makampuni utakaoibuka!
Tena makampuni class 1, 2 na 3.
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Do you know ni kiasi gani serikali huilipa viongozi wanaoenda Apolo India kwa matibabu??
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
umechanga pesa au unachanga maoni...
 
Lisu atapona tu,Mungu ndie aliemfikisha hapo alipo.Mungu wetu ni mwema hawezi kutuumiza kiasi cha kwamba na yeye anakadi ya Ccm.
Lazima atende maajabu ili ukoo wa Sizonje na Bashite waaibike mbele yetu.
Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.
That which is has been long ago, and that which is to be has been long ago: and God seeks again that which is passed away.
 
Kuna picha imetolewa leo humu, TL yuko dispensari ndo huko wanalipa 10 M kwa siku?
Kupona kwa Mhe. Lissu ni mpango wa Mungu, nawaomba Watanzania wenzetu waendelee kumuombea kwa Mungu pamoja na kuchangia gharama za matibabu, kwa kuwa gharama zake ni kubwa ambazo chama pekee hakiwezi kuzimudu bila ya misaada kutoka kwa watu mbalimbali.

Unajua ahueni humtokea mgonjwa taratibu taratibu na ndivyo inavyotokea kwa Lissu, ingawa sisi wote tuna hamu apone mara moja aje aendelee kupigania haki za wanyonge kama alivyokuwa akifanya.

Sisi tunatoa taarifa za maendeleo ya Lissu kulingana na Madaktari wanavyotuambia, hatuwezi kusema chochote nje ya wataalam hao, kwa kuwa ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua maendeleo ya mgonjwa husika.

UPINZANI NI KAZI NGUMU Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.

Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.

Huwezi kuendesha nchi bila kuruhusu ukosoaji, iwe kutoka upinzani au kwenye chama unachokiongoza, unapowazuia watu wasipumue na kutoa madukuduku yao, unatengeneza hasira kubwa ndani ya jamii.

Mwanahabari Huru

Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Kumbe mteja wa rambirambi, kawambie walokutuma, BADO.
 
10 M kwa siku ni za kutengenez mtu mpya maabara si hospitali. Na Mbowe hataondoka huko pengine asikie ruzuku imetoka tena, aje achukuwe.

Endelea kumchangia watanzania wezangu.
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
 
kwa siku kama sija kosea ni 10m

Wameiweka hii milioni 10 sababu kuna operations zinazoenelea kila wakati wanapoona sasa operation hii inastahili au muda wake umefika.Kuna operations nyingine ni ghali zaidi,na hapo inaendana na vipimo vyake vinavyochukuliwa kila siku au baada ya siku kadhaa.

Ukitaka kujua gharama ya private hospital kubwa na yenye ufanisi jaribu kumpeleka mgonjwa wako hapo Aghakhan,usipoangalia vipomo peke yake inaweza kukugharimu milion sita na ushee.Tuwe wavumilivu.Afya ya Lissu kwanza
 
Back
Top Bottom