Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,233
- 8,779
Leo ni siku ya uhuru wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Tunawapongeza wale waliochukuwa juhudi za kuitoa hii nchi chini ya makucha ya wakoloni wa kiengereza , kwa njia za amani na kistaarabu.
Tunawaombea Wazanzibar wote mafanikio katika juhudi zao za kuitoa tena Zanzibar katika makucha ya mkoloni mweusi kutoka Tanganyika
Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibari, Aaamin.
======
Katika sehemu hizi za Afrika Mashariki na kati dola ambayo ilitambulikana katika miaka ya karne ya 19 ni Zanzibar. Hapa Zanzibar palikuwa na Mabalozi wa nachi mbali mbali Wakiziwakilisha nchi zao.
Hii Zanzibar ilikuwa ni Dola kabla ya Tanganyika, Kenya, Uganda na katika nchi nyingine Afrika ya Mashariki na ya kati. Huo ndio utukufu wa Zanzibar.
Katika miaka ya 1880 na 1885, Wakoloni walianza kuingia sehemu hizi... Wakaamua kugawana Afrika. Katika mkutano uliofanyika Berlin 1885 wakamnyang'anya mtawala wa Zanzibar sehemu yote ya Afrika. Zanzibar wakaachiwa visiwa pamoja na Mwambao wa maili kumi kwenda ndani.
Kuanzia kaskazini mwa Kenya mpaka kusini ya Tanganyika. Ilikuwa yote hayo ni mamlaka ya Zanzibar. Wajerumani wakaamua kuununua ule mwambao wa maili kumi wa Tanganyika. Kenya Wajerumani hawakuinunua, mwambao wa Kenya ulibaki sehemu ya Zanzibar, Lamu ilikuwa sehemu ya Zanzibar mpaka mwaka 1963, Kenya ilipopata Uhuru wakakubaliana waache. Tukabaki na Unguja na Pemba kama nchi.
Katika miaka ya 1950, 56, 57, Wazanzibari wakaunda vyama vya siasa, kumwondoa mkoloni.
Tukawa na Afro - Shirazi Party, Zanzibar Nationalist Party au Hizbu, Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP), tukawa na Umma Party.
Hivi ni vyama vilivyotafautiana kwa sera, kwa itikadi, lakini vyote vilishirikiana kumuondoa mkoloni Zanzibar.
Zanzibar ikapata uhuru tarehe 10/12/1963. Hapo Muingereza akaondoka. Alipoondoka Muingereza, Mkuu wa nchi akawa Sultani.
Zanzibar na Kenya zikajiunga na Umoja wa Mataifa kama wanachama kamili 13/12/1963 na bendera ya Zanzibar ilipanda katika Umoja wa Mataifa kama nchi nyingine.
12/1/1964 tukapinduana. Afro-Shiraz Party wakafanya mapinduzi, wakaipindua serikali ya Sultan, na Sultan akakimbia nchi.
Sasa, baada ya hapo ikaundwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ... ilikuwa ni serikali kamili, ni dola yake ya Wazanzibari. Tukawa na wimbo wetu wa Taifa. Tukawana Rais wetu Zanzibar.
Credit: Hotuba ya Maalim Seif Kibanda Maiti