Leo tarehe 02 Desemba 2021ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi nchini Ndg. Daniel Chongolo

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Leo tarehe 02 Desemba 2021ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi nchini Ndg. Daniel Chongolo.

Chama Cha Mapinduzi katika akaunti za mitandao ya kijamii kimeandika ujumbe ufutao;

"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakutakia heri katika kuadhimisha kumbukumbu ya siku yako ya kuzaliwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Godfrey Chongolo.

Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu yenye baraka na mafanikio tele; Daima tupo pamoja nawe katika utendaji na kukiongoza Chama Cha Mapinduzi."


#HappyBirthdayChongolo

Ndg. Daniel Chongolo ni Katibu Mkuu wa kumi wa CCM tangu Chama hicho kilipozaliwa Februari 5, 1977. Alithibitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mnamo tarehe 30 Aprili 2021 baada ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika katika Kituo Cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma.

IMG-20211202-WA0022.jpg
IMG-20211202-WA0023.jpg
daniel_godfrey_chongolo-20211202-0001.jpg
 
Dah.....Siku Ya Kuzaliwa...! Unakuja Kuitangaza huku.
Sasa CCM inakwenda Halijojo...! Nani atakwenda Kuinusuru !!
Tuvute Subra..
 
Dah.....Siku Ya Kuzaliwa...! Unakuja Kuitangaza huku.
Sasa CCM inakwenda Halijojo...! Nani atakwenda Kuinusuru !!
Tuvute Subra..
Ni jambo la heri kumtakia kiongozi heri. Mwenyezi Mungu amjalie hekima, busara na maarifa katika kukiongoza Chama Cha Mapinduzi.
 
Badala ya kuishauri CCM mambo huku ni halijojo (mfumuko wa bei) wanatakiana heri ya kuzaliwa
 
Back
Top Bottom