Leo siku ya mihadarat duniani:matajiri wanawatesa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo siku ya mihadarat duniani:matajiri wanawatesa vijana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Jun 26, 2011.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Leo ni siku ya madawa ya kulevya......wengi wetu hapa tunawafahamu na tunaishi nao watumiaji wa madawa ya kulevya......madawa yamewaathiri sana vijana wa kitanzania......wengi wetu tuna ndugu zetu na jamaa zetu ambao wameathirika na dawa za kulevya......
  Mimi ni muathirika wa dawa za kulevya soma kisa hiki

  Baba yangu mdogo alikua anatumia madawa ya kulevya.....hasa cocaine na heroine.....siku moja alienda kwa huyo jamaa anayeuza madawa hayo,walikuwa vijana weengi mule ndani wanajidunga...ghafla polisi wakavamia eneo lile na kufanya ambushi,baba yangu mdogo akakamatwa pamoja na vijana wengine kama saba hivi na mwenye nyumba ambaye ni muuzaji wa madawa hayo rejareja na jumla.

  Kesi ikaunguruma kwa mwaka mzima.....hatimaye baba yangu mdogo na wale mateja wenzie wakatiwa hatiani kwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela,lakini yule muuzaji akakutwa hana hatia akaachiwa(pesa iliongea).

  Alipokua jela mimi ndiye niliyekuwa naenda kumuona kila weekend,huko gerezani nilikua nampelekea sabuni,sukari,nguo,shuka,na hata mkate.....hali ya ba'mdogo ilianza kubadilika siku hadi siku,alianza kudhoofika,si yeye tu hata wafungwa wenzie ambao alifungwa nao kwa ile kesi,hali ilipokua mbaya nikawataarifu nyumban,ikabidi tuhangaike hadi mgonjwa akalazwa hospitali ya mkoa wa Dodoma chini ya Ulinzi wa magereza,tukamuuguza lakini bahati mbaya akafariki......kunbe ba'mdogo alikufa kwa HIV,maana hata wale wenzie nao walianza kupukutika kwa vifo kule magereza......inasadikika walitumia Bomba la sindano 1 wakati wakijidunga........
  Hivi ndivyo madawa ya kulevya yalivyoniathiri

  Serikali bado haijaamua kupambana na wauza mihadarati....jk list yake mbona haitaji??????tangu 2006 hadi leo......?????
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kenya wameamua kuwagawia mateja syringe ili wasichangie.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mmmmh.......lakini kenya vinara wakubwa si wabunge?????mara nyingi bbc huripoti jinsi vijana wa mombasa na malindi walivyoathirika.....
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  What a coincidence! Si ndio tarehe kama ya leo ndio aliyofariki Amina Chifupa?
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ni Miaka minne sasa
   
Loading...