Leo rasmi nimeanza kutumia dawa kwa ajili ya pressure. Naanza staili mpya kuishi

Mzee Wassira hii siyo ile pressure ya kukosa ubunge wa Bunda? We mze mbishi sana sijapata ona, unalilia machangu wako wa Dodoma wakati wenzako hawana mpango na wewe. Pumzika kwa amani, we ishi kwako ukijilia ugali wako na dagaa wa Ziwa Victoria, achana na machangu.
Mimi sio mzee wasira. Japo najua joking. Hiyo ni avata tu.
 
Pole kiongozi, badala ya kuzi-miss hizo lite, we achana nazo tu usije ukafikia hatua ya kuishi kwa kutegemea dawa!!

Mother nae alianza kuugua pressure!!

Mara ugonjwa wa moyo

Mara eh, kisukari...

Hao jamaa watatu kwa kawaida wana tabia ya kutembea pamoja!!

Hapo akaanza mwendo wa vidonge... huku vya pressure, kule moyo sijui kufanya nini, kutanabai, FIGO!!

Huku na kule, mara ini, na tunapata habari za ini ilishakuwa too late!!
Ahsante mkuu.
 
Ahsante kwa ushauri mzuri. Niwe mwazi kabisa. Dawa nilizoanza kutumia nimesitisha. Jana na leo sijatumia, na sababu za kusitisha ni kwamba baada ya kuanza tu kutumia, ahsubuhi yake nikaanza kusikia mwili hauna nguvu. Nikajua ni kwa kuwa nilikojoa sana usiku huo.
Ahsubuhi nikaanza kunywa maji. Nilikunywa maji lita 5. Nilikojoa sana. Jioni ile hali ya mwili kukosa nguvu niliendelea kuisikia mpaka jioni ya saa 2 usiku.
Nikanyanyua simu kuongea na dr m1 ambaye ni rafiki yangu. Akanishauri nikacheck tena, labda kipimo cha mwanzo hakikuwa sahihi. Nikaenda kupima, this ilikuwa sehemu nyingine. Kupima ikasoma 180/110 imepungua 7/5.

Nikarudi home, nikanywa dawa. Kukojoa kama kawa. Ahsubuhi ile hali ya kuishiwa nguvu nikaona kama imezidi. Nikaendele kunywa maji lita 5 nyingine. Mpaka jioni nikajiona sipo sawa tofauti na kabla ya kuanza kutumia dawa.
Kwa hiyo usiku huo sikutumia tena dawa. Nikaamka kidogo nipo poa. Jana tena sijatumia, leo nimeamka mzima kabisa.
Nimeamua kuacha dawa kwa muda na sasa nabadili staili ya vyakula.
Ni mwendo wa mbogamboga, matunda, kupunguza chumvi na mazoezi.
Leo jioni nitaenda kucheck. Nitaleta mrejesho hapa.
Ahsante.
Dawa ni muhimu. Sema hujapata ile inayokufaa. Nenda kwa wataalamu wa mambo hayo na useme dawa uliyopewa na vile ilikufanya. My dad ana pressure hua anapima kila siku anarecord na anakunywa dawa asubuhi na jioni. Pressure ikawa inaenda vizuri akapunguza dozi anywe mara moja kwa siku haikuchukua hata masaa 24 akaanza kujiskia vibaya ikabid aendelee na dozi ya mara 2 kwa siku.
Yeye katika dawa zake kuna aspirin pia kulainisha damu.

Japo anakunywa dawa anajitahid kula vizuri pia. Kwahiyo na wewe kaka jitahid kuonana na wataalamu unaweza siku ukashangaa unainua mkono hauinuki.
 
Mimi
Mmh... ..

Zimetulea..

Hata za mzungu nazo ni sumu pia.
Kapime figo, na visa vya watu 2 walikuwa ni watumiaji wa zuri wa miti shamba kwa muda mrefu hivi ninavyoongea wote wanahudhiria dialysis 2 na 3 kwa week.

Dawa za hospital zina viwango na description zinazoeleweka kitaaluma, mti shamba ni ramli.
 
Pole sana Mkuu kila la heri katika matibabu yako.

Nimekuwa nasumbuliwa na pressure kwa muda sasa. Leo nimepima ilikuwa 187 juu na chini 115.
Baada ya mashauriano na dr nimeamua kuanza kutumia dawa.

Nimepewa dawa za kutumia wiki moja then nirudi kucheck tena.

Ndio kwanza nina 44 yrs. Nitazimiss sana lite, na lager.
 
Ahsante kwa ushauri mzuri. Niwe mwazi kabisa. Dawa nilizoanza kutumia nimesitisha. Jana na leo sijatumia, na sababu za kusitisha ni kwamba baada ya kuanza tu kutumia, ahsubuhi yake nikaanza kusikia mwili hauna nguvu. Nikajua ni kwa kuwa nilikojoa sana usiku huo.
Ahsubuhi nikaanza kunywa maji. Nilikunywa maji lita 5. Nilikojoa sana. Jioni ile hali ya mwili kukosa nguvu niliendelea kuisikia mpaka jioni ya saa 2 usiku.
Nikanyanyua simu kuongea na dr m1 ambaye ni rafiki yangu. Akanishauri nikacheck tena, labda kipimo cha mwanzo hakikuwa sahihi. Nikaenda kupima, this ilikuwa sehemu nyingine. Kupima ikasoma 180/110 imepungua 7/5.

Nikarudi home, nikanywa dawa. Kukojoa kama kawa. Ahsubuhi ile hali ya kuishiwa nguvu nikaona kama imezidi. Nikaendele kunywa maji lita 5 nyingine. Mpaka jioni nikajiona sipo sawa tofauti na kabla ya kuanza kutumia dawa.
Kwa hiyo usiku huo sikutumia tena dawa. Nikaamka kidogo nipo poa. Jana tena sijatumia, leo nimeamka mzima kabisa.
Nimeamua kuacha dawa kwa muda na sasa nabadili staili ya vyakula.
Ni mwendo wa mbogamboga, matunda, kupunguza chumvi na mazoezi.
Leo jioni nitaenda kucheck. Nitaleta mrejesho hapa.
Ahsante.
Dawa za pressure hunywewa asubuhi. Unless iwe umefanyiwa kipimo cha kurecord saa 24 na kuonekana una tatizo wakati wa usiku. Nenda hospitali kubwa kama JKCI watakusaidia
 
Cheza na huo mmea ndani ya wiki mbili utakuja kutupa mrejesho. Hii ni kiboko ya presha, kisukari, vidonda vya tumbo na kipanda uso. All the best mkushi
IMG-20201107-WA0019.jpg

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom