Leo Ramadhani siku ya tano Afande Sele bado yupo hai. Je, ni kweli Albadiri inaweza kudhuru mtu?

KIFO NI AHADI.
Kusoma Al badri NI Jambo jingine na KUJIBIWA NI JAMBO JINGINE.
hapo hata kama haijajibiwa haimaanishi afande sele alikuwa sahihi.
Muda wake utafika
Kwanza Kishki hajasoma Albadiri, alichofanya ni kumuapiza Afande Sele kutokana na jazba yake, Al Badiri ni kisomo kinachosomwa na baadhi ya wanaoamini ni kuwa unamshitakia Mungu kupitia wale waliyopigana vita vya Bader na nina uhakika Kishki hajafanya hivyo.

Alichokifanya ni kumuomba Mungu kwa ajili ya kitendo alichokifanya Sele pale msikitini kwake na kwenye kuomba kuna kukubaliwa au kutokubaliwa. Lakini juu ya yote hayo tulisikia kutoka kwa Sele akiomba msamaha kwa aliyoyatenda na vilevile sheikh wa mkoa naye alizungumzia juu ya kadhia hii na kwa ujumla wake mambo yaliwekwa sawa na maisha yanaendelea, hii habari aidha mtoa mada hajajua kuwa case ni dismiss au kama anajua ila anataka kuleta "uchochezi" hiyo ni tafsiri ndogo kwa uzi huu. Tunaomba tupo kwenye mfungo basi tutumie muda mwingi kutafakari kusudio zima la funga zetu.
 
Akbadiri ni kiini macho ingekuwa inafanya kazi marais wengi na viongozi wakubwa wa ulaya na usa wangekuwa washasomewa
 
Akbadiri ni kiini macho ingekuwa inafanya kazi marais wengi na viongozi wakubwa wa ulaya na usa wangekuwa washasomewa
Hivi vitu vinatafakarisha sana inawezekana tunachoaminishwa hakiko hivyo
 
Mawazo ya Mungu si sawa na mawazo ya mwanadamu
Alisema kabla ya Ramadhan lakini hakusema ya mwaka gani 🤣🤣🤣🤣 hawa ma Shekh wengine shida sana badala ya kumuombea mtu arudi katika njia ya sawa unaenda kuomba afe ili iweje? Ndio maana Mungu si Athumani.
 
Aliongelewa afande Chefes'ewle siyo afande Sele 🤣🤣
Albadiri ilisomwa na KISHKI ili afande Sele afe kabla ya Ramadhani lakini bado anaendelea kudunda.

Je, ni kweli Albadiri inaweza kuua mtu au ni hadithi tu? Kwenye uzoefu wako umeshawahi kusikia mtu kafa kwa albadiri. Tupe uzoefu wako.

Pia soma
 
Yeye nd anatakiwa atubu na aombe msamaha kw mola wke ili kukiri kosa lake lkn uwez kusema ss binaadam tumsamehe ajatukosea sisi kamkosea mung wke kama kwel unauoendo na mungu afande sele si wa kutetewa anastail adhabu na hukumu yke ni kubwa na atapewa pamoja na wale wanaomtetea wote
 
Albadiri ilisomwa na KISHKI ili afande Sele afe kabla ya Ramadhani lakini bado anaendelea kudunda.

Je, ni kweli Albadiri inaweza kuua mtu au ni hadithi tu? Kwenye uzoefu wako umeshawahi kusikia mtu kafa kwa albadiri. Tupe uzoefu wako.

Pia soma
Una uhakika ilisomwa al badir? Kwanza nikwambie albadir ni ushirikina haupo kwenye uislam, pili afande sele aliomba radhi kwa kitendo alichofanya
 
Kuna haja kubwa mashehe wawe wenye elimu kubwa, sio hao wanaokimbia darasani na kubaki na elim ya madrasa. Lakin sio mashehe tuu bali hata baadhi ya wachungaji. Maana hawa ndo wanaoharibu jamii
 
Hatimae Ramadan imeisha Ila Afande Sele anadunda tu, masheikh wametuangusha sana aisee, wametuongoza chaka na albadir yao uchwara.

Wale masheik watimuliwe aisee 😃 washeikh uchwara wale.
 
Back
Top Bottom