Serikali inajinasibu kulipa madeni yote ya wastaafu kiasi cha shilingi trillion 1.3. Leo hii katika mkutano wa walimu Dodoma raisi Magufuli amerudia kuwa wamekwisha lipa. Mbona viongozi wa PPF wanasema hawajapokea pesa ya madai ya wastaafu wa ATCL.
Wanasema walichopokea ni malipo ya madeni wao waliikopesha serikali. Hali hii inawasikitisha wastaafu ATCL kwani hawaelewi nani mkweli katika ya raisi na viongozi wa PPF.
Ama waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amepeleka pesaxhizo mahala pengine na anabaki kuahidi kulipa tu. Hii danadana kwa wastaafu wa ATCL inhitaji ufumbuzi kwani ni haki yao kisheria na wamekatwa toka mishahara yao wakati wakiwa kazini.
Serikali iwe ya watendaji wa kweli na wazi kuwa SSRA haina uwezo wa kusimamia mifuko kwani suala la wastaafu ATCL wanalifahamu na hakuna hatua madhubuti walizo chukua hata baadaya mahakama kuamuru kukamata mali za ATCL ili kuwalipa wastaafu hawa haki zao.
Ofisi ya katibu mkuu kiongozi analijua suala hili lakini maagizo yake nae yamepuuzwa. Tunaomba serikali ilipe hawa wastaafu ATCL na sio kufanya siasa na kutoa ahadi hewa.