Uchaguzi 2020 Leo nitazungumzia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi na mafanikio makubwa tuliyo yapata 2015 hadi 2020

Besta Mlagila

Senior Member
May 29, 2018
101
191
Na: Beatrice Condrad

Kauli mbiu ya Chama Cha Mapinduzi 2020 ni: TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.

Kwanza kabisa napenda kutoa UTANGULIZI wa Ilani yetu ya Uchaguzi 2020 kama ifuatavyo;

1. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa vyama vya TANU na ASP na baadaye CCM, imejengwa katika misingi ya ujamaa na kujitegemea inazingatia utu, usawa na haki. Misingi hii imeimarishwa na siasa safi na Uongozi Bora wa CCM imekuwa ndiyo nguzo ya kudumisha, umoja na mshikamano wa Kitaifa. CCM itaendelea kuzisimamia Serikali zake kuhakikisha kuwa zinazingatia, kulinda, na kudumisha misingi hii adhimu.

2. CCM itahakikisha kuwa Tanzania unaendelea kulinda Uhuru wake, kudumisha Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, na kuimarisha Muungano wetu wenye mfumo wa Serikali mbili pamoja na Tunu nyingine za Taifa ikiwemo Falsafa ya Mwenye wa UHURU ili kuendelea kujenga Taifa imara linalojitegemea kiuchumi na Kisiasa lenye ustawi wa watu wake na linaloenzi na kuthamini mila nzuri , Desturi na Utamaduni wetu .

3. CCM inaamini kwamba uzalendo kwa Nchi ndiyo msingi wa Maendeleo ya kweli ya Tanzania ambayo yataletwa na Watanzania wenyewe. Hivyo basi, CCM itaendelea kuhimiza Wananchi kuwa Wazalendo kwa nchi yetu kwa kufanya kazi kwa uadilifu ,bidii na maarifa Kama msingi imara wa Maendeleo.

4. CCM inaamini pia kuwa kila mtu anajukumu la kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea Maendeleo yake na Taifa kwa ujumla. Imani hii ndiyo chimbuko la KAULI MBIU ZA... ( HAPA KAZI TU) na kuacha kufanya kazi kwa mazoea aidha, CCM inatambua kuwa Serikali inazoziongoza zina jukumu la Msingi la kuhakikisha kuwa walio wanyonge katika jamii wanapata fursa ya kipekee ya kustawisha maisha yao na kuondokana na unyonge wao ili kupunguza tofauti za matabaka.

5.. CCM inatambua kuwa Nchi yetu ina watu wenye uwezo na Rasilimali za kutosha kama vile ardhi, madini , gesi asilia, misitu, wanyama, mali kale/ Mambo ya kale, bahari, maziwa na mito, pamoja na nafasi na fursa nzuri za kijiografia. Rasilimali na fursa hizi zikitumiwa vizuri zitakuwa chachu kubwa kwa Maendeleo ya Taifa kama ambavyo imethibitika katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 na kwamba "TUKIAMUA TUNAWEZA" Ni katika muktadha huu CCM inaamini kuwa TANZANIA ni nchi tayari.

6.. Katika miaka mitano (5) ya Utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 chini ya Uongozi wa DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na DKT. ALLY MOHAMED SHEIN ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, mafanikio makubwa yamepatikana katika nyanja na sekta zote za Maendeleo kwa ustawi wa Wananchi .

MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2015 HADI 2020 NI PAMOJA NA;

A..Kuendelea kulinda na kuimarisha umoja, mshikamano, amani, utulivu, ulinzi na usalama.

B..Kuendea kulinda na kuimarisha na kudumisha Uhuru, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania.

C.. Kuendelea kulinda na kuimarisha Demokrasia ya vyama vingi, haki za binadamu, nchi isiyofungamana na dini yoyote na kupambana na unyanyanyasaji na udhalilishaji wa aina zote.

D..Kuendelea kuwa na Nchi isiyofungamana na upande wowote ili kuweza kutetea na kulinda maslahi ya nchi yetu kwa kuzingatia misingi tunayoiamini.

E..Kuimarisha Utumishi wa Umma unaozimgatia ueledi, nidhamu , uadilifu, bidii na maarifa katika kazi.

F..Kuimarisha mifumo ya Kisera, Kitaasisi na Kisheria, ikiwemo kutungwa kwa sheria inayotaka Serikali za mitaa kutenga 10%ya mapato yake kwaajili ya Uwekezaji wawanawake 4%, Vijana 4% na watu wenye Ulemavu 2%

G..Kuimarishwa kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina kulikowezesha kusimamia na kuboresha utendaji wa mashirika ya umma yaliyoweza kuchangia jumla ya shilingi Trilion 1.052 Kama gawio na Michango kwa Serikali.

H..Kuhamisha Serikali MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA.

I..Kuthibiti na kuhimarisha Mapambano dhidi ya rushwa, Uhujumu Uchumi na Ufisafi, na hivyo kuokoa fedha na rasilimali nyingine na kuzielekeza kwenye mipango ya Maendeleo ya nchi.

J..Kuthibiti na kuhimarisha Mapambano dhidi ya Uzalishaji, uagizaji, usambazaji, uuzaji na Matumizi ya DAWA ZA KULEVYA, Utakatishaji wa Fedha haramu na biashara ya kusafirisha binadamu( HUMAN TRAFIC).

K..Kujitosheleza kwa Chakula na kuzalisha ziada kwaajili ya masoko ya nje.

L..Kuimarisha Uchumi wa Viwanda ambapo idadi ya Viwanda imeongezeka kutoka Viwanda 52,633 mwaka 2015 Hadi kufikia viwanda 61,110 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.1%. Kutokana na hatua hii, Uzalishaji wa bidhaa na ajira umeendelea kuongezeka.

M..Kutekeleza miradi ya kimkakati yenye tija kubwa katika uchumi na ustawi wa jamii ikiwemo na miradi ifuatayo:

✓Mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere (stiglas gauge)

✓Ujenzi wa Reli ya Kisasa( SGR)

✓Kufufuliwa kwa shirika la ndege la Taifa kwa kununua ndege mpya 11

✓Kununua meli mbili mpya Zanzibar

✓Ujenzi wa jengo la Abiria katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa ABEID AMAN KARUME.

N..Kuimarisha mfumo wa uthibiti, usimamizi na umililiki wa madini na hivyo kuongeza mapato yatokanayo na mazao ya madini kutoka shiling bilioni 168 mwaka 2015 Hadi shilingi bilioni 567.57 mwaka 2020.

O.. Kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 kwa mwezi mwaka 2015 Hadi kufikia wastani wa shilingi trililioni 1.3 mwaka 2019. Kwa upande wa Zanzibar mapato ya Serikali yameongezeka kutoka wastani wa shililingi bilioni 428.5 mwaka 2015/2016 Hadi kufikia shilingi bilioni 748.9 mwaka 2018/2019. Maendeo hayo yameongeza uwezo wa Serikali wa kutekeleza miradi ya Maendeleo na kutoa huduma za jamii kwa Wananchi.

P.. Kuchukua hatua za kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na athari za mazingira ikiwa ni pamoja na kuondoa MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI.

Q.. Kuendelea kupiga hatua za Maendeleo katika maeneo mbali mbali Kama vile ujenzi wa miundombinu ya Kisasa, kukua kwa kasi kwa Uchumi na Kuimarika kwa Ustawi wa Jamii .

TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI 10 AMBAZO UCHUMI WAKE UNAKUWA KWA KASI BARANI AFRIKA NA IVYO KUWA MIONGONI MWA NCHI ZA UCHUMI WA KATI MWAKA 2020, Miaka mitano kabla ya kufikia lengo lake mwaka 2025.

Mitano (5) tena kwa JPM kwa Maendeleo ya Tanzania.

Imeandaliwa tarehe 20/08/2020
 
L..Kuimarisha Uchumi wa Viwanda ambapo idadi ya Viwanda imeongezeka kutoka Viwanda 52,633 mwaka 2015 Hadi kufikia viwanda 61,110 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.1%. Kutokana na hatua hii, Uzalishaji wa bidhaa na
Unaota wewe!
 
Objectives mlizowekewa na wananchi zilikua ni zipi na kati ya hizo mme meet ngapi? Tuanzie hapo
 
Jambo ambalo kwa miaka yote hii takribani 10 sasa mmeshindwa kuligundua ni moja tu: Tumewachoka! Mnatumia nguvu kubwa sana kuendelea kubakia madarakani, lakini wapi!

Waachieni Nchi watu wengine hata kwa miaka 10 tu ili tuone na wenyewe watatufanyia nini! Hamuoni mnapata mateso kuzunguka na kundi kubwa la wasanii njaa ili tu kuwavutia watazamaji nyakati hizi za uchaguzi?
 
Kwanini huwa inahitaji nguvu kubwa mno kuonesha mafanikio ya awamu hii? Hii inamaanisha tu hakuna cha maana, na kwamba mengi mabovu ya awamu hii yanafichwa na machache mazuri kwa kutumia propaganda.
 
Back
Top Bottom