Leo ningependa kidogo tujadili kuhusu siasa za Kenya

Wanaposema historia au ya kale huwa yanajirudia ni haya tunayoyaona sasa hivi. Hakuna makamu rais ambaye amefanikiwa kumrithi bosi wake kupitia njia ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, tangia enzi za Mzee Jomo.

Mwendazake George Saitoti alitoswa kando na aliyekuwa rais Daniel T. Arap Moi, ambaye alimchagua rais Uhuru Kenyatta kama mrithi wake. Rais Mwai Kibaki naye hakumuunga mkono wala kupinga ndoto za urais za makamu wake, Kalonzo Musyoka.

William S. Arap Ruto ni naibu rais, sio makamu. Labda atakuwa na bahati ya kuanzisha ukurasa mpya kwenye utamaduni huo. Ila uzoefu wa RAO kwenye siasa sio jambo la kupuuzwa. Uchaguzi wa urais mwaka huu utakuwa na ushindani mkubwa na sio ajabu ukirudiwa tena(run-off).
Mkuu unaonekana umekuwa ni mfatiriaji mzuri wa siasa za kenya lkn kinachonipa mashaka zaidi ni huu muungano hasa chama tawala kuunga mkono mpinzani wake ujue si jambo la kawaida.

Je huo wasi wasi wako kuwa william ruto nae atakuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda wewe unatumia kanuni gani unamaanisha nusu ya majimbo ya kenya wanamkubali pia william ruto?

kwangu mimi naona baba raila odinga ananafasi kubwa ya kushinda si ni kweli jameni😆
 
Mimi nimeipenda sana siasa ya Kenya haina unafiki, ila sijajua tatizo la Uhuru kuto muunga mkono Makamu wake wakati walishapanga akimaliza Kenyata aingie Ruto sasa sijui hapa katikati kumetokea nn?
 
Hakuna Mkenya anayeishi Kenya anaweza kujadili Siasa za Tanzania, kwanza ukiondoa Magu (RIP) hakuna Kiongozi wa modern times Tanzania anayejulikana Kenya, sasa hivi ukipita mitaani Kenya ukawauliza raisi wa Tanzania ni nani utashangaa, wengi hawatojua jina lake pamoja na kujipendekeza kote.

Nakumbuka kipindi Samia bado Makamu alienda Kenya nimesahahu ziara ilihusu nini, nina mshikaji wangu Mkenya katika kuongea akaniambia hakujua kama Tanzania kuna Makamu wa raisi Mwanamke alishangaa kumuona kwenye TV, wakati Tanzania watu wanajua Jina la kuanzia Raisi wa Kenya, Makamu Jaji Mkuu mpaka Spika siajabu hata wakataja Baraza lote la Mawaziri Kenya …
Watz ni wafuatiliaji wa Kenya hawana mpango na maswala ya siasa wao ni Pesa tu
 
Hakuna Mkenya anayeishi Kenya anaweza kujadili Siasa za Tanzania, kwanza ukiondoa Magu (RIP) hakuna Kiongozi wa modern times Tanzania anayejulikana Kenya, sasa hivi ukipita mitaani Kenya ukawauliza raisi wa Tanzania ni nani utashangaa, wengi hawatojua jina lake pamoja na kujipendekeza kote.

Nakumbuka kipindi Samia bado Makamu alienda Kenya nimesahahu ziara ilihusu nini, nina mshikaji wangu Mkenya katika kuongea akaniambia hakujua kama Tanzania kuna Makamu wa raisi Mwanamke alishangaa kumuona kwenye TV, wakati Tanzania watu wanajua Jina la kuanzia Raisi wa Kenya, Makamu Jaji Mkuu mpaka Spika siajabu hata wakataja Baraza lote la Mawaziri Kenya …
true story btw... 💯
 
Hiyo top five is only on your mind, hakuna mtu anayemjua kama unafikiri nadanganya jaribu kama una mtu Kenya muulize jina la raisi wa Tanzania au Makamu wake, utashangaa, Tanzania tunadanganywa na kujidanganya sana.
wanamjua Samia bhana acha uongo, i stay there sometime na wanamjua, sema jina moja tu Suluhu ndio wengi wamelizoea kuliko samia.

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimeipenda sana siasa ya Kenya haina unafiki, ila sijajua tatizo la Uhuru kuto muunga mkono Makamu wake wakati walishapanga akimaliza Kenyata aingie Ruto sasa sijui hapa katikati kumetokea nn?
kulitokea kutokuelewana kati ya Ruto na Kenyatta, sababu Ruto humdharau sana boss wake, na hata kuepo hapo kama makamu ni aliwekwa tu ili kuepusha machafuko kwenye uchaguzi ulopita, sababu is trie Ruto anapendwa na wengi anaweza kutoa tamko watu wasiende makazini na hakuna ataeenda, Ruto akiongea anasikilizwa sana, thats why hawezi kua Raisi Ruto. Nowadays watu wengi sana wanahamia chama cha Laila ma wengi wanaondoka kwa Ruto, But mpambano ni mkali sio kidogo.

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unaonekana umekuwa ni mfatiriaji mzuri wa siasa za kenya lkn kinachonipa mashaka zaidi ni huu muungano hasa chama tawala kuunga mkono mpinzani wake ujue si jambo la kawaida.

Je huo wasi wasi wako kuwa william ruto nae atakuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda wewe unatumia kanuni gani unamaanisha nusu ya majimbo ya kenya wanamkubali pia william ruto?

kwangu mimi naona baba raila odinga ananafasi kubwa ya kushinda si ni kweli jameni😆
Sio kwamba nina uoga kuhusu ushindi wa mgombea yeyote yule. May the best man win na atakayeshinda atakuwa rais wangu. Kuhusu muungano wa chama tawala cha Jubilee na chama cha upinzani ODM, rejea kwenye ile 'handshake' kati ya rais Uhuru na Raila Odinga. Yote yalianza hapo, ikiwa ni pamoja na DP Dkt. Ruto kutengwa kisiasa na mwenzake.

Nimesema kuna uwezekano mkubwa kwamba uchaguzi wa urais utarudiwa, yaani run-off. Kwasababu kwa mtizamo wangu sioni mgombea yeyote akifanikiwa kutimiza vigezo vyote viwili muhimu ili atangazwe kuwa mshindi. Ambavyo ni kushinda kwa kura 50%+1 ya jumla ya kura zote. Pamoja na kuongoza kwa kura nyingi zaidi kwenye gatuzi 25 kati ya gatuzi zote 47.
 
Hawa jamaa wa pipoooz power huwa wana uwezo mdogo sana wa kufikiri.

Jana wamepost video youtube yenye maudhui ya watu...ikala copyright claim kutokana na kutumia maudhui ya watu...cha kuchekesha eti wameanza kuilaumu serikali kuwa wao ndo wameifuta.

Frikiria eti Lissu anajitapa kuwa ana damu ya wakenya, duh huu ulimbukeni wa hao pipooooz hautakwisha sasa hivi.
 
kulitokea kutokuelewana kati ya Ruto na Kenyatta, sababu Ruto humdharau sana boss wake, na hata kuepo hapo kama makamu ni aliwekwa tu ili kuepusha machafuko kwenye uchaguzi ulopita, sababu is trie Ruto anapendwa na wengi anaweza kutoa tamko watu wasiende makazini na hakuna ataeenda, Ruto akiongea anasikilizwa sana, thats why hawezi kua Raisi Ruto. Nowadays watu wengi sana wanahamia chama cha Laila ma wengi wanaondoka kwa Ruto, But mpambano ni mkali sio kidogo.

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
Kwamaana hiyo Ruto kamsaidia pakubwa Kenyatta kupata Urais ila sasa Kenyatta anamsaliti hii mbaya sana machafuko yanaweza kurudi tena
 
Back
Top Bottom