Leo ningependa kidogo tujadili kuhusu siasa za Kenya

chrisbleez

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
735
1,208
Hamjambo ndugu zangu!

Leo ningependa kidogo tujadili kuhusu siasa za kenya hasa kwa hiki kinachoendelea kwa hivi sasa...kitendo cha raisi uhuru mwigai kenyata kutangaza rasmi kumuunga mkono mpinzani wake raila amolo odinga.

Jambo hili limetushangaza sana na kusema ukweli nimependa sana kuona siasa za wenzetu zikipiga hatua na kwakweli hii imeonyesha upendo wa hali ya juu hata kwa chama cha jubilee wenyewe wanaonesha kumfurahia.

Sasa swali langu ni kwamba chama cha jubilee ambacho ndio chama tawala kwa pamoja kitakwenda kumuunga mkono mpinzani wake raila amolo ondinga kuwa raisi wa jamuhuri ya watu wa kenya na kumuacha makamu wake wiliam ruto?!!!!

Updates;

Uhuru kenyata atangaza rasmi kuwa kenya ni nchi ya sita kwa utajiri barani africa bila kuwa na madini wala mafuta🤭
 
Natamani huyu mama yetu pamoja na yule wa uganda wangejifunza kuhusu siasa za huyu jirani yetu binafsi niseme tu ukweli sikutegemea kama ingetokea hili.
Ndiyo maana Kenya hakuna vyeo vya fadhila mkuu, kila mtu anawajibika kwa nafasi yake na anaipata kwa kufanya live interview, huku majina yale yale yanazunguka upande wa utawala utadhani jamaa wana hati miliki na nchi.
 
Hamjambo ndugu zangu!

Leo ningependa kidogo tujadili kuhusu siasa za kenya hasa kwa hiki kinachoendelea kwa hivi sasa...kitendo cha raisi uhuru mwigai kenyata kutangaza rasmi kumuunga mkono mpinzani wake raila amolo odinga.

Jambo hili limetushangaza sana na kusema ukweli nimependa sana kuona siasa za wenzetu zikipiga hatua na kwakweli hii imeonyesha upendo wa hali ya juu hata kwa chama cha jubilee wenyewe wanaonesha kumfurahia.

Sasa swali langu ni kwamba chama cha jubilee ambacho ndio chama tawala kwa pamoja kitakwenda kumuunga mkono mpinzani wake raila amolo ondinga kuwa raisi wa jamuhuri ya watu wa kenya na kumuacha makamu wake wiliam ruto?!!!!
Uhuru Kenyatta asha endorse Raila pale sagana 3 sasa unatuuliza nini?
 
Hakuna Mkenya anayeishi Kenya anaweza kujadili Siasa za Tanzania, kwanza ukiondoa Magu (RIP) hakuna Kiongozi wa modern times Tanzania anayejulikana Kenya, sasa hivi ukipita mitaani Kenya ukawauliza raisi wa Tanzania ni nani utashangaa, wengi hawatojua jina lake pamoja na kujipendekeza kote.

Nakumbuka kipindi Samia bado Makamu alienda Kenya nimesahahu ziara ilihusu nini, nina mshikaji wangu Mkenya katika kuongea akaniambia hakujua kama Tanzania kuna Makamu wa raisi Mwanamke alishangaa kumuona kwenye TV, wakati Tanzania watu wanajua Jina la kuanzia Raisi wa Kenya, Makamu Jaji Mkuu mpaka Spika siajabu hata wakataja Baraza lote la Mawaziri Kenya …
 
Hakuna Mkenya anayeishi Kenya anaweza kujadili Siasa za Tanzania, kwanza ukiondoa Magu (RIP) hakuna Kiongozi wa modern times Tanzania anayejulikana Kenya, sasa hivi ukipita mitaani Kenya ukawauliza raisi wa Tanzania ni nani utashangaa, wengi hawatojua jina lake pamoja na kujipendekeza kote …
Sio kweli mkuu...raisi wetu ameingia kwenye historia ya dunia kuwa raisi mwanamke ambae yupo top five kama sikosei inawezekana vipi wasimjue?!!!
 
Sio kweli mkuu...raisi wetu ameingia kwenye historia ya dunia kuwa raisi mwanamke ambae yupo top five kama sikosei inawezekana vipi wasimjue?!!!

Hiyo top five is only on your mind, hakuna mtu anayemjua kama unafikiri nadanganya jaribu kama una mtu Kenya muulize jina la raisi wa Tanzania au Makamu wake, utashangaa, Tanzania tunadanganywa na kujidanganya sana.
 
Mkuu nataka kukuelewa lkn embu tumsaidie mtoa mada unazionaje siasa za kenya na umoja wao waliouwanzisha?

Fahama ya kwamba hivi sasa kinachoendelea live ni AZIMIO DAY OF CONVENTIONS. na wanarusha live kupitia vyombo vyao vya tv mule ndani yupo kalonzo musyoka,yupo raila odinga,yupo hyu mtoto wa moi(Gidion moi)

Lengo ni kumuunga mkono raila odinga awe raisi wa jamuhuri ya watu wa kenya
 
Wanaposema historia au ya kale huwa yanajirudia ni haya tunayoyaona sasa hivi. Hakuna makamu rais ambaye amefanikiwa kumrithi bosi wake kupitia njia ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, tangia enzi za Mzee Jomo.

Mwendazake George Saitoti alitoswa kando na aliyekuwa rais Daniel T. Arap Moi, ambaye alimchagua rais Uhuru Kenyatta kuwa mrithi wake. Rais Mwai Kibaki naye hakumuunga mkono wala kupinga ndoto za urais za makamu wake, Kalonzo Musyoka.

William S. Arap Ruto ni naibu rais, sio makamu. Labda atakuwa na bahati ya kuanzisha ukurasa mpya kwenye utamaduni huo. Ila uzoefu wa RAO kwenye siasa sio jambo la kupuuzwa. Uchaguzi wa urais mwaka huu utakuwa na ushindani mkubwa na sio ajabu ukirudiwa tena(run-off).
 
Back
Top Bottom