Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume

KARUME DAY NA TBC

Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume.
Mtangazaji Bakari Msuya kaniuliza maswali mengi.

Nimemweleza Mzee Karume nikianza na uhusiano wake na watu wa Dar es Salaam katika miaka ya 1940s hasa na viongozi wa Young Africans Football Club.

Nimemweleza Mzee Karume akiwa na viongozi wa TAA yeye akiwa kiongozi wa juu katika African Association uhusiano ambao ulimsaidia Karume kuunda Afro Shirazi Party (ASP) mwaka wa 1957 kwa msaada mkubwa wa Nyerere na TANU.

Tukaja katika Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano mwaka wa 1964.
Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa TANU hawakuwa mbali na matukio yote haya ya kihistoria.

Kipindi hiki kitarushwa leo baina ya saa moja na saa tatu usiku.

Mzee Mohamed Said Heri ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mohamed Said ni Mjasiri na Msomi mzuri sana hasa katika Historia ya Tanganyika hilo halina mjadala.

Nilipata kusoma Review ya Kitabu chake Cha Uamuzi wa Busara wa Tabora kwenye gazeti moja la nchini Kenya! Nikashangaa sana! Mbona hii kitu haifanyiki kwenye magazeti ya kwetu - gazeti lenyewe nililipata dukani ikanibidi nibadilishane na gazeti la Rai ambalo nilikuwa nimemaliza kulisoma,muuza duka akanipatia Daily Nations (Alikuwa ameyanunua kwa kilo kama vifungashio vya biashara yake).

Nikakikata vema nikatoa na nakala nikaanza kuifuatilia historia hiyo adhimu ya Tanganyika kuelekea Uhuru ambayo sijawahi kuisoma darasani.

Nilienda Maktaba ya mkoa nikaanza kusaka vitabu vya Historia ya Tanganyika kuelekea Uhuru kwa nguvu sana nikabahatika kupata vitabu vifuatavyo:-
1. Modern Tanzanians - (Ed.) John Illife.
2. Discipline and Tears - E.M.Mang'enya
3.Two African Statesmen - John Hatch

Katika Vitabu vyote hivi sijaona yanayofanana na madai ya Mzee wangu huyu.
Nilipoenda kuishi Tabora niakendelea na utafiti wangu mdogo pale mjini kuhusu Harakati hizo nikajifunza mengi sana.

Mzee Mohamed Said ni Hazina nzuri inayokosa radha yake kamili pale tu anapotaka KULAZIMISHA kuisilimisha Historia ya Tanganyika ionekane kuwa Ni harakati za Waislamu kudai Uhuru wa Tanganyika.

Mzee anafahamu visa na visasili vingi kuhusu uhuru wetu na hili la Interview ya TBC na Historia TBC wamepata mtu sahihi.

Shida yangu ipo hapo tu! Uhafidhina wa Kiimani tu.
Swali dogo kwako Mzee: UAMUZI WA BUSARA WA TABORA ULIFANYIKIA KATIKA ENEO GANI PALE TABORA?
Asante.
 
Mna...
Mkutano wa Kura Tatu ulifanyika Parish Hall.

Ama kuhusu Waislam katika kuunda African Association (AA ) 1929 kisha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganika 1933 na viongozi wakiwa ni walewale Mzee bin Sudi (Mmanyema) na Kleist Sykes (Mzulu) viongozi wa AA na kisha kuunda TANU historia ndiyo hiyo Waislam ndiyo waliounda mimi nimezaliwa nimekuta hivyo kuwa babu zangu ndiyo waliounda taasisi hizi.

Sasa mimi nimelazimisha kitu gani hapo?

Kama hakuwafanya hayo sema kuwa mimi sisemi kweli waliounda TANU si wazee zangu.

Hebu angalia hii hapo chini:

KISA CHA "WACHAWI WATATU" KATIKA MACBETH NDANI YA UKUMBI WA MJADALA WA KURA TATU TABORA 1958

Leo FB imenirushia kumbukumbu ya mkutano wa Tabora kuhusu Uchaguzi wa Kura Tatu wa mwaka wa 1958.

Uchaguzi huu nimeueleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes na katika mihadhara kadhaa niliyopata kufanya.

Vilevile nimeandika kitabu ''Uamuzi wa Busara,'' (2007) kuhusu Kura Tatu.

Leo sitaki kujirudia ila napenda tuwaangalie wahusika wakuu wa Kura Tatu katika staili ya ''Dramatis Personae.''

Hii ''Dramatis Personae,'' ni orodha ya wahusika katika michezo ya William Shakespeare, ukifungua kitabu tu unakutana na orodha ya majina yao.

Tunaanza na Julius Nyerere Rais wa TANU.

Mwalimu alitaka sana TANU iingie katika Kura Tatu lau kama TANU nzima ilikuwa haitaki.

Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Sheikh Suleiman ndiye tunaweza kusema alikuwa kiongozi wa wapinzani wa Kura Tatu ndani ya TANU.

Sheikh Takadir baada ya kurudi kutoka Tabora TANU ikiwa imepiga kura ya kushiriki Kura Tatu alimkabili Nyerere uso kwa macho ndani ya mkutano wa Halmashauri Kuu pale New Street (Lumumba Avenue) na akamwambia maneno makali kiasi hakuna mtafiti yeyote wa historia ya TANU hadi leo aliyekuwa na ujasiri wa kuyaandika maneno yale.

Siku ile Mwalimu alilia.

Adhabu ya Sheikh Suleiman Takadir ilikuwa kufukuzwa uanachama wa TANU na nafasi yake ya Mwenyekiti wa Baraza la Wazee akachukua Mzee Iddi Tulio.

Zuberi Mtemvu yeye alikuwa ''siasa kali,'' sera yake ilikuwa Afrika kwa Waafrika na Kura Tatu masharti yake ilikuwa Mwafrika ampigie kura Mzungu, Muasia na Mwafrika.

Hapa sasa tunaingia katika kisa cha watu naweza kuwaita, ''The Three Musketeers,'' au tunaweza kuwaita, ''The Three Conspirators,'' ukipenda, ''The Three Witches,'' yaani, ''Wanga Watatu,'' mfano wa wale ''Three Weird Sisters,'' katika, ''Macbeth,'' ya William Shakespeare.

Mimi nimelipenda jina hili la ''Wanga Watatu,'' kupita yote kwa kuwa katika hawa ''wachawi,'' watatu, wawili walikuwa wapinzani wa Kura Tatu, Mwalimu Kihere na Sheikh Rashid Sembe.

Lakini walipokutana na Nyerere na kufanya kikao Mwalimu aliwabadilisha fikra wakaunga mkono Kura Tatu.

Hawa ni Mwalimu Nyerere, Mwalimu Kihere na Sheikh Rashid Sembe wapangaji wa mpango wa ushindi Mkutano wa Tabora wa kuwashinda wapinzani wote wa Kura Tatu waliokuwa wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir.

Kilichofuatia ndani ya ukumbi wa mkutano Tabora timu hii ya watu watatu kama wanga wafanyavyo ikawa kama vile wamewavamia wajumbe majumbani kwao usiku wa manane wakawanyunyuzia dawa ya kuwageuza mawazo.

Mkakati huu ulikuwa unaongozwa na hawa wazalendo watatu ulishinda.

Waingereza wanasema, ''Carried the day.''

Leo tumebakia na simulizi.

Hii ndiyo historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika katika ukweli wake.

Mohamed Said ni mmoja kati ya JF members ambao wana facts nyingi sana za kihistoria pamoja na kwamba huwa anakuwaga na falacy zake flani hasa za kiimani ambazo binafsi huwa naona zinafanya watu wamu underate hasa wale ambao hawapendi religious identity zitumike katika historia.Kwa mfano AbdulSykes na wazee wengine waliokuwa wakazi wa Dar ambao walishiriki katika strugles za uhuru hawakufanya vile kwa sababu ya uislamu wao bali ni kwa sababu ya Utanganyika wao,Hata mzee Karume aliposhiriki katika kupinga utawala dhalimu wa SUltani Zanzibar hakufanya vile kwa sababu ya uislamu wake bali ni kwa sababu ya Uzanzibari wake.

Kimsingi mimi bado nitaendelea kukuheshimu kwa utajiri wa maarifa na historia uliotupatia na bado nitaendelea kukataa kwamba Waislamu wa Tanzania wamekuwa Marginalized kwani hata ukiande hata katika nchi ambazo waislamu wako majority bado kuna changamoto ya kukasa muamko na kujikuta wakishindwa kutumia vizuri fursa ingawa wengine wakizitumia huanza kunyooshana vidole.

Nafikiri ni vyema Mzee akawekeza pia katika kuwaeleza waislamu wengine madhara ya kutokuhamasisha watoto wao pia kupambana katika ilimu dunia kama wanavopambania ilimu ahera.Awaambe tu ukweli kwamba mchawi wao sio KAFIRI bali mchawi wao ni wao wenyewe.

ALL in ALL kila laheri nitaitafuta hio makala niitazame maana bdo TBC hawajanishawishi kuwatazam labda mpaka Pascal Mayalla atakapopewa kazi ya kuwa Mkuu wa Idara ya habari maelezo na mkurugenzi wa TBC nitafikiria kuiangalia TBC ili nijue kama ataendelea kuwa critical au ataendelea kuwa kada.Asije kuwa kama Polepole na Bashiru enzi za JPM
Huna tofauti na hao unaowakandia, unajichanganya mara Pascal Mayalla mara nini sijui kifupi hueleweki
 
Ngoja kwanza; hivyo vitabu vyote kabatini, umeandika mwenyewe au ni moja kati ya hazina kwa library yako? I wish nikutembelee nami nipate maarifa ya hapa na pale though inabidi niwe na chujio kubwa cause mzee huaga una aleji sana na Wakristo
Sidhani kama utaenda kwake atakuwa na allergy ya udini, siamini kama anachagua watu wa kumtembelea kwa kufuata misingi ya kidini,hata mimi nimevutiwa sana na maktaba yake na usomi wa huyu mzee wetu, sote tunajua bei za vitabu zilivyo juu ni sawa mtaji mkubwa wa biashara,mzee wetu kawekeza kwenye elimu,elimu ni mtaji ambao mwenye nao hafilisiki ni maisha yake,naamini kuwekeza hadi kwa vizazi vijavyo sababu baadhi ya vitabu huwezi kuvipata hivi sasa, kwani pia waandishi wetu wa kisasa wengi wao wao wamekosa uwezo wa kufikiri wanapoandika vitabu ,wao wanawaza pesa tu, kwa hilo nampongeza sana mzee wetu huyu,tumpende au tusimpende bado anabaki kuwa mmoja wa wanahistoria wakubwa wa nchi hii ,kawazidi kwa kiwango kikubwa wale maprofesa wetu, ambao hawajitambui na wamebakia wakiweza pesa tu. Kwa huyu mzee anavyojua historia ya nchi hii na utamaduni wa jiji la Dar Es Salaam nilitegemea hata Safari Channel wangeenda kufanya mahojiano ya makala ya historia ya jiji la Dar Es Salaam.
 
Mfianchi,
Nina vipindi viwili nimefanya na Safari Channel.

Ngoja In Shaa Allah niingie Maktaba.

Mfianchi,
Hakuna tabu ndugu yangu.

Mfianchi,
Safari Channel:

Mfianchi,
Nimekuwekea hapa historia ya Ali Msham na picha kutoka maktaba yake kwa hisani ya wanae.

Kulia wa kwanza ni Ali Msham na aliyekaa kwenye meza ni Julius Nyerere hapo ni nyumbani kwa Ali Msham aliyeigeuza nyumba yake kuwa tawi la TANU.

20210423_004800.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom