Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
1,841
2,000
Mohamed Said ni mmoja kati ya JF members ambao wana facts nyingi sana za kihistoria pamoja na kwamba huwa anakuwaga na falacy zake flani hasa za kiimani ambazo binafsi huwa naona zinafanya watu wamu underate hasa wale ambao hawapendi religious identity zitumike katika historia.Kwa mfano AbdulSykes na wazee wengine waliokuwa wakazi wa Dar ambao walishiriki katika strugles za uhuru hawakufanya vile kwa sababu ya uislamu wao bali ni kwa sababu ya Utanganyika wao,Hata mzee Karume aliposhiriki katika kupinga utawala dhalimu wa SUltani Zanzibar hakufanya vile kwa sababu ya uislamu wake bali ni kwa sababu ya Uzanzibari wake.

Kimsingi mimi bado nitaendelea kukuheshimu kwa utajiri wa maarifa na historia uliotupatia na bado nitaendelea kukataa kwamba Waislamu wa Tanzania wamekuwa Marginalized kwani hata ukiande hata katika nchi ambazo waislamu wako majority bado kuna changamoto ya kukasa muamko na kujikuta wakishindwa kutumia vizuri fursa ingawa wengine wakizitumia huanza kunyooshana vidole.

Nafikiri ni vyema Mzee akawekeza pia katika kuwaeleza waislamu wengine madhara ya kutokuhamasisha watoto wao pia kupambana katika ilimu dunia kama wanavopambania ilimu ahera.Awaambe tu ukweli kwamba mchawi wao sio KAFIRI bali mchawi wao ni wao wenyewe.

ALL in ALL kila laheri nitaitafuta hio makala niitazame maana bdo TBC hawajanishawishi kuwatazam labda mpaka Pascal Mayalla atakapopewa kazi ya kuwa Mkuu wa Idara ya habari maelezo na mkurugenzi wa TBC nitafikiria kuiangalia TBC ili nijue kama ataendelea kuwa critical au ataendelea kuwa kada.Asije kuwa kama Polepole na Bashiru enzi za JPM
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,773

Ubongo...
Nimekusoma.

Ila nitasema neno moja.

Hawa walioandika historia siyo ambayo nilikuja kusahihisha walifanya hivyo kwa kutaka kufuta mchango wa Waislam katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Usinilaumu kwa kusahihisha makosa.
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,773
2,000
Ahaaa, kwa nini mzee wetu?
Idugunde,
Angalia tofauti baina yako na mwenzako katika kuniita.
Wewe umeniadhimisha kwa uzee wangu umeniita kwa adabu ''mzee wetu.''

Wengi hapa kwa chuki ya kushindwa kustahamili ukweli wa ninayoandika hupandwa na ghadhabu na kama njia ya kulipa kisasi haumua kunikejeli na kujaribu kunifedhehesha.

Lakini kwangu mimi siwezi kukasirika kwa kuitwa mzee kwa sababu hakika mimi ni mzee na mzee ana nafasi kubwa ya kuheshimika katika jamii vipi nihisi vibaya?

Lakini ipo tofauti kubwa baina ya ''huyu mzee'' na ''mzee wetu.''

Huyu mzee huyo hapo chini:

1617826219721.png

London 1992

1617826305996.png

Paris 1993

1617826359014.png

Alexandria 1988
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,773
2,000
Ni mdini kupitiliza... Fuatilia mada zake
Otoro...
Angalia hayo niliyoandika toka nikiwa kijana mdogo sana na jiulize ikiwa hawa waliochapa vitabu na paper zangu na kunialika katika vyuo vyao kuzungumza ni watu gani.

Hili ndilo jibu lako:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.

Huyo hapo chini ni ''Huyu mzee:''

1617827286484.png

London 1992

1617827348696.png

Paris 1993

1617827430719.png

Alexandria, Egypt 1988
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,475
2,000
Mohamed Said ni mmoja kati ya JF members ambao wana facts nyingi sana za kihistoria

ALL in ALL kila laheri nitaitafuta hio makala niitazame maana bdo TBC hawajanishawishi kuwatazam labda mpaka Pascal Mayalla atakapopewa kazi ya kuwa Mkuu wa Idara ya habari maelezo na mkurugenzi wa TBC nitafikiria kuiangalia TBC ili nijue kama ataendelea kuwa critical au ataendelea kuwa kada.Asije kuwa kama Polepole na Bashiru enzi za JPM
Duh...!.
P
 
Generalist

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,222
2,000
KARUME DAY NA TBC

Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume.
Mtangazaji Bakari Msuya kaniuliza maswali mengi.

Nimemweleza Mzee Karume nikianza na uhusiano wake na watu wa Dar es Salaam katika miaka ya 1940s hasa na viongozi wa Young Africans Football Club.

Nimemweleza Mzee Karume akiwa na viongozi wa TAA yeye akiwa kiongozi wa juu katika African Association uhusiano ambao ulimsaidia Karume kuunda Afro Shirazi Party (ASP) mwaka wa 1957 kwa msaada mkubwa wa Nyerere na TANU.

Tukaja katika Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano mwaka wa 1964.
Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa TANU hawakuwa mbali na matukio yote haya ya kihistoria.

Kipindi hiki kitarushwa leo baina ya saa moja na saa tatu usiku.

Ni Mzee lakini uko na Nguvu zako. Heko.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,026

Nimekuona ukienda mubashara mzee,hakika kongowe kwako na pia nimependa sana maktaba yako, ni hazina kubwa kwa kweli ,ni watu wachache ambao hutoa pesa yao mfukoni kununulia vitabu badala ya kwenda kunywea bia, hakika nikiri tu kuwa ni mwan historia nguli hapa nchini na mupo wachache sana ilifaa uwe mkufunzi wa chuo kikuu, marehemu JPM alipenda sana kutuasa juu ya umuhimu wa somo la historia kwa ajili ya mustakabli wa nchi yetu.Taifa lolote lisilo na historia ni kama mfu ambaye maiti yake haijulikani ni ya nani. Pmoja na sisi wengine kukuangalia kuwa ni mdini sana lakini panapo stahili kutoa pongezi wacha tutoe,hakuna mwanadamu aliye mkamilifu, simulizi zako huwa ni za kusisimua na kutafakarisha, heshima kwako mzee. Daima maandiko yako yamekuwa yakivuta watu si kwa ubaya tu au uzuri tu bali kutokana na kipaji na uwezo ulionao. Mungu azidi kukubariki ili uendelee kutuhabarisha mengi ya nyuma ambayo hatuyajuia na sisi wengi si wasomaji vitabu.Asante sana.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,026
2,000
KARUME DAY NA TBC

Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume.
Mtangazaji Bakari Msuya kaniuliza maswali mengi.

Nimemweleza Mzee Karume nikianza na uhusiano wake na watu wa Dar es Salaam katika miaka ya 1940s hasa na viongozi wa Young Africans Football Club.

Nimemweleza Mzee Karume akiwa na viongozi wa TAA yeye akiwa kiongozi wa juu katika African Association uhusiano ambao ulimsaidia Karume kuunda Afro Shirazi Party (ASP) mwaka wa 1957 kwa msaada mkubwa wa Nyerere na TANU.

Tukaja katika Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano mwaka wa 1964.
Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa TANU hawakuwa mbali na matukio yote haya ya kihistoria.

Kipindi hiki kitarushwa leo baina ya saa moja na saa tatu usiku.

Hii sebule itakuwa imepokea wageni wengi mashuhuri,ni sebule nadhifu na ni chimbo la historia, nimependa hii maktaba binafsi hakika hapa ni juhudi za miaka mingi kuwa na vitabu kama hivi,wenye maktaba kama hizi majumbani mwao naweza kusema kwa hapa tanzania hawazidi 50, kwani Watanzania hatuna utamaduni wa kujisomea vitabu au kununua vitabu, tunaona kununua vitabu ni kupoteza pesa na kusahau kamaelimu ni bora kuliko pesa.
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,501
2,000
Ngoja kwanza; hivyo vitabu vyote kabatini, umeandika mwenyewe au ni moja kati ya hazina kwa library yako? I wish nikutembelee nami nipate maarifa ya hapa na pale though inabidi niwe na chujio kubwa cause mzee huaga una aleji sana na Wakristo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom