Leo nimesikia aibu sana

Leo bwana nilikwenda supermarket moja hivi, nilipongia nikakuta kuna kifoleni kidogo kwani mbele kulikuwa na mteja ambaye anaongea English, Kiswahili hajui ilikuwa ni wakati wakulipia na muuzaji nae Kiingereza hajui, niliumia sana kwani yule mteja mimi namjua ni dada wa Kimakonde na kaolewa na mzungu, anajua Kiswahili vizuri tu nahisi kushinda Kiingereza chenyewe.

Nilikaa nikasema why anafanya hivi lakini, huyu dada nilishawahi hata kucheza naye pool table ni Mswahili kabisa na ni Mmakonde kwa wazazi wake Mikoroshoni, kasoma Msasani Primary School.
Haha haha mtoto wa Lutembo anatusababishia foleni
 
Uzi huu sio tena wa dada alieongea English bali ni wa mwana jf aliekosea matamshi ya kingereza is ntiti😁😁🤭🤣
 
Sasa kakosea wapi, unajua wengi mlio soma enzi za Nyerere mnaona kuongea kiswahili ni lazima hata kama hutaki.......njoo ofisini kwangu if you can't answer in Engilish just quit, wakati mimi ni msahili kabisa. Kila lugha inawakati wake.

Kuna mazingira ukiongea kiingereza unakua unadhalilisha watu na kujizalilisha mzee saloon Sokon tandale ama kwenye daladala umuongeleshe konda ni ufalas huo
 
Kuna mazingira ukiongea kiingereza unakua unadhalilisha watu na kujizalilisha mzee saloon Sokon tandale ama kwenye daladala umuongeleshe konda ni ufalas huo
Hapo utakua kichaa ukienda kwa mama tilie au kwa konda ukaongea kiingereza, ila supermarket bar shule gym sioni kama kuna tatizo.
 
Sasa kakosea wapi, unajua wengi mlio soma enzi za Nyerere mnaona kuongea kiswahili ni lazima hata kama hutaki.......njoo ofisini kwangu if you can't answer in Engilish just quit, wakati mimi ni msahili kabisa. Kila lugha inawakati wake.
Na hiki ndicho kiingereza cha ofisini kwako mkuu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom