Leo nimepatikana ushamba ni kitu kibaya sana ndugu zanguni

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Jamaa yangu anafanya project flani Morogoro na Shirika Moja la Kimataifa. Sasa kwa kuwa siku zote huwa namshauri ajitahidi basi anunue gari akishindwa aangalie hata gari ya Toyota. Kaagiza Toyota Prado Mayai imefika last week.leo kaja Dar amalizie some stuff aondoke nayo.

Kapanda Bus anasema hakuna ndege Morogoro. Basi akaomba nije mchukua Ubungo.Bahati nzuri nami nlikuwa na Issues flan pale Ubungo Plaza.mida ilipofika akanambia amekaribia nisogee Stand ya Mkoa.

Hapo ndo Nlipojilaumu kwa Ushamba. Nmezunguka Ubungo karibia masaa mawili.siioni stand ya Mkoa.Nikahisi labda GOOGLE MAP haisomi vizuri.nmezunguka sana siioni stand Kuu ya Mkoa.

Baadaye nikaona kuuliza si ujinga nikapark gari Ubungo Tower nikamwita mtu wa Taxi nikampa tsh 30,000 anipeleke stand ya Mkoa.jamaa nikaona kama amepigwa na butwaa kidogo nikahisi labda nimempa pesa kidogo basi nikamwongeza tena 20,000. Akanambia "bro unaenda stand ya mkoa ubungo?" Nikamwambia ndiyo.we niongoze kwa taxi yako nikufuate.

Basi tukatoka ubungo plaza akanipitisha barabara flani tukarudi main road kuzunguka mara nikamwona anachepuka kushoto kutaka nipeleka sijui mitaa gani uswahilini.nikasimamisha gani nikapiga horn.akapark akaja dirishani.

Nikamsisitizia stand ya mkoa nliambiwa ipo hapa karibu ye ananipeleka wapi. Maskini sijawahi kushangaa mpaka kuacha mdomo wazi.anasema "boss hapa ndo stand ya mkoa"

Wanaume sisi wa Dar es salaam mbona tunavaa vizuri,tuna magari mazuri,tunakaa kwenye apartment za gharama.sisi wengine tunatumia mpaka Mil 1 kwa siku au zaidi kama safari ya Bagamoyo. Kweli tunashindwa changishana kujenga Stand Kuu ya Mkoa ya Kisasa?

Stand imechoka,ni kama gofu...inakuaje hapo panaitwa stand ya Mkoa? Why mnahatarisha maisha ya abiria?ni sehemu ya hatari sana kwa maisha ya binadamu.nmehuzunika sana kusema ukweli.sikutegemea kama stand ya mkoa inaweza kuwa hivyo.

Mimi nmezoea kutumia ndege na private car. Sijawahi panda magari haya mnaita ya mkoani.nlitegemea ingekuwa kama Usa, Uk,Canada n.k

Nlishtuka nikadhani ni uwanja wa wanajeshi kufanyia mazoezi.nikastaajabu kwa nini raia wengi wamo mle na kuna mabus ya jeshi (nliona ni makuu kuu sana) na ya kiraia.

Nmempokea jamaa yangu amechoka sana.nikampeleka kwanza akale Hotel nzuri then nikaenda naye oysterbay akapumzike.nmemwambia akafanyiwe massage sea cliff maana sidhani kama atakuwa Ok. Akaogelee na kufanyiwa massage.mimi ntaenda mchukua saa tatu akiwa ameshakula aje home kulala.

Siku zote nikiambiwa ubungo stand ya mkoa nlikuwa nawazia kama sehemu classic sana.leo nmeonekana mshamba.dereva taxi nlipa tsh 50,000 anipeleke hapo nikaona kama nimlalia sana. Ila nikajipongeza nami sasa naanza kuwa mjanja. Mle ndani nmeshangaa unaingia unatoka unalipia tsh 10,000? Sasa kwa nini wasingecharge tsh 30,000 hizi gari zetu na usafiri kama wa toyota,nissan,subaru wawe wanalipa tsh 10,000? Ili kuinua mapato.ipatikane pesa wajenge Stand nzuri ya kisasa. Na waendao kwa miguu hawa walipie tsh 5,000 tu.

Jamani ni aibu kwetu watanzania.tujitahidi kupenda nchi yetu.najua nikiwaleta wadogo zangu hapo watalia sana.maana wao machozi yao yapo karibu wanapoona kuna sehemu kuna umaskini.

Afadhari mimi nmeanza kuwa sugu.anyway....nmetoka gym now nimepumzika huku wananikanda miguu ili i relax najua ninyi waswahili huwa mnaona kama huu ni ubishoo.wala si ubishoo ni kujijali.usidhani kuwa na miguu migumu kama msasa ni sifa.huo sio uanaume.

Uanaume ni kutunza mwanamke,kumjali,kumtendea wema na kumpa haki yake ya kimwili na kiakili ipasavyo.kuweni smart si gharama sana.hapa nlipo ni tsh 70,000 tu wanakukanda,wanakuweka miguu kwenye barafu,kuna kama vimipira wnakwambia ukanyage,wnakupaka mafuta ya ku relax muscles na ...ukitoka hapo ni kama unatembea hewani.

Nikitoka hapa naenda sea cliff kumpitia jamaa yangu nirudi naye home.leo ni kama Jumatatu. Natumia Mercedes Benz. Haya maisha basi tu ni vile hatuna pesa.ndo maana tunaishi hivi.anyway.... wadau tuwe tunakumbukana kwenye maombi.mambo mengi,muda hautoshi kabisa.

Hiyo ndo stand ya mkoa/jiji dar es salaam.nmeumia sana.sitamani kukumbuka.
 
Trump ndugu yako? 😠
 
Wakati ndo unapofanyia misele yako kila siku
Boss wa online
 
Back
Top Bottom