CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Leo nimeona post ya ndugu yangu Ado Shaibu wa ACT. Inadai wanawake wa ACT wanamtaka (hawaombi) raisi aitishe kikao cha maridhiano! Mwisho Ado akaongeza "takataka" binafsi za kudai tume huru na katiba mpya!
Yaani kichekesho!
Kumbe walisusa huku kiroho kinauma? Walidanganyana wataitwa?
Kiongozi wa ACT Zitto wakati anatangaza kususa achaguzi alidai WASILAUMIWE! Yaani alitoa kitisho! Sasa wanawake wa Chama chake wanamtaka (hawamuombi) waliyemtishia ndio aitishe kikao cha maridhiano! Ingefaa wajue serikali inasubiri watende hicho ambacho wanadhani watalaumiwa wakikitenda. Ama sivyo watuambie wamekwama kutekeleza kitisho!
Hivi unayemwambia "asikulaumu" atakutana na wewe ili iweje? Akulaumu?
Hivi kama kususa kulihusiana na tume kutokuwa huru (kwa mtazamo wao) au kukosekana kwa katiba mpya kwa nini walihamasishana kujiandikisha? Si wangesusa toka mwanzo? Tushike lipi? Mlinyimwa form, mlinyimwa kurudisha form, wagombea walikatwa au katiba na time?
Je huu si uthibitisho kuwa tangu awali mlipanga kuharibu uchaguzi ili mdai tume na katiba mpya? Tuseme msingekatwa, kukataliwa, kukwepwa kama mnavyodai mngeshiriki chini ya tume hii iliyopo na katiba iliyopo? Hili wazo la tume na katiba limewajia kabla au baada ya kususa?
Hamuoni mnaanika uchawi wenu sokoni?
Hizi kauli na vitisho vya kitoto vinawaponza!
Nawashauri hivi: hakuna atakayewaita kutafuta mwafaka maana hakuna mgogoro wa kitaifa. Wala huyo mnayetaka aandae kikao Hana huo muda. Mlitaka kukutana naye wahini majimboni kwani huwa anapita huko kutatua kero halisi za wananchi. Akifika eneo lako omba mic umueleze tatizo lako ni katiba, tume, kunyimwa kuchukua au kurejesha form, kukatwa wagombea! Na sio maji, zahanati, shule, barabara! Halafu usikilize atakavyokujibu ili upate huo mwafaka.
Kama hili huwezi endelea kususa na kutishia ila usitende uhalifu maana utajuta!