Nilichukua gari kwenda kupokea mzigo wangu kutoka mkoani pale Mbezi Kibada cha mkaa.
Wakati tunaenda tulipiti njia ya wazo hili na kutokea barabara ya Goba. Njiani nilisimamishwa na maaskari mara tatu, kila mala wakimwambia dereva wanataka kukagua lesseni yake. Kumbe hiyo ni lugha ya kutaka pesa na dereva wangu alikuwa akiambatanisha lesseni na shs 2000.
Polisi baada ya kupokea hela walirudisha leseni tukaendelea na safari. Ilifika mahali nikawajia juu askari na kuwaambia kuwa usumbufu wao unachanguankuua biashara.
Askari mmoja mkurya ana mvi alinitishia ila sikutishika.
Baada ya kupakia mzigo tukapitia njia ile ile. Kuingia tu barabara ya goba tukasimamishwa, baada ya kilometa kama mbili tukawakuta tena askari wawili wa kike wana gari hurrier pembeni nao wakikusanya pesa nk.
Nachotaka kusema ni kuwa usumbufu wanaopata wafanyabishara jijini kutoka kwa askari hawa unachangia kuongeza ugumu wa maisha kwani usafirishaji bidhaa unakuwa juu sana kutokana rushwa ya polisi, na mzigo mwishoni utamuangukia mlaji wa mwisho.
Nimeambiwa kuwa mchezo huu ni rasmi ndani ya Jeshi la Polisi na kila Askari analazimika kupeleka mga kwa wakubwa zake hadi unamfikia mkubwa kabisa.
TAKUKURU wanajua, usalama wa taifa wanajua na Rais analijua. Je, inawezekana kwa kuwa traffic wamegeuka TRA hayo ndiyo malipo yao?