Leo nimeokota noti ya shilling 10,000 ikiwa ni mara ya pili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.Je, hii ni bahati tu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Habari wadau,

Kwanza nianze kwa kusema hii si mara yangu ya kwanza kuokota hela kama ambayo naamimi hata wewe msemaji huenda umewadia kuokota hela pengine zaidi ya mara moja.

Katika hali ya kawaida(kwani naamini ni kwa wengi), nimekuwa nikiokota hela ndogo ndogo(shilingi 1000,2000,500, n.k) tena katika interval kubwa tu kiasi kwamba nakuwa sikumbuki hata mara ya mwisho niliokoto lini.

Cha ajabu na kinachonifanya hata mimi nishangae na kujiuliza hilo swali hapo juu kwenye heading, ni mimi kuokota noti ya shilingi 10,000 tena mara mbili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Mara ya kwanza ilikuwa ni tarehe za mwanzoni za mwezi wa December ambapo nilikiwa katika matembezi yangu mjini nikaokota noti ya shilingi 10,000 na leo ni mara ya pili nimeokota noti kama hiyo nikiwa katika bar moja.

Leo hii nimekuja katika bar moja ambayo hata jana nilikuwepo.Tofauti na jana, leo hakuna wateja wengi hivyo meza nyingi kwa kiasi fulani ziko tupu na nimekaa pale pale nilikuwa nimekaa jana. Meza moja baada ya meza niliyokaa mini,kulikuwa na watu kama watatu ambao baada ya kupata vinywaji, wakaondoka na kwakweli hata sura sijawakariri .

Baada ya wahusika kuondoka, zilipita kama dakika sita nikajikuta nimegeuza shingo upande wa ile meza waliokuwa wamekaa na kuona noti ya shilingi 10,000 iko chini.Bila kuchelewa, nikainuka faster nikaiokota na hakuna alie-note chochote huku wahusika wakiwa nao wameaondoka na hata sura sijawakariri unless waje kuulizia kama kuna mtu kaokota hela kwenye meza waliokuwa wamekaa(wakija nitawapa).

Halafu kingine cha ajabu, ndani ya dakika kama mbili au tatu baada ya mimi kuokota hiyo hela, akaja muhudumu special anaefagia chini ya meza na kuokota vitu kama tissue akafagia kwenye ile meza iliyo tupu kisha akaja kwenye meza yangu na akaendelea kwenye meza nyingine kiasi kwamba ningechelewa kidogo tu, ile 10,000 angeokota yeye.

Sasa najiuliza, kuokota huku noti kubwa kubwa kama hizi tena ndani ya muda mfupi hivi, ni bahati tu au ni Mungu ananirudishia kile kidogo nachowapa ombaomba mitaani?

Kusema ukweli, mimi nikipita sehemu au nikiwa nimekaa mahali na akapita ombaomba, huwa sisiti kuwapa chochote na nimekuwa nikifanya hivi mara kwa mara na mara ya mwisho nilimpa ombaomba mmoja siku kama tatu hivi zilizopita.

Vile vile, some days back(miezi kama minne iliyopita) nikiwa chuoni(UDSM) mida ya saa moja kasoro jioni,niliokotoa noti za shilingi 1,000 zilizokuwa zimeachana umbali wa hatua kama mbili maeneo ya geti la chuo cha maji huku wanafunzi wakiwa wengi wanaotoka na kuingia chuoni mpaka nikapata wasi wasi wa kuokota noti ya pili ingawa ni wazi ziliangushwa na mtu mmoja akiwa anaetembea.

Kwanza namshukuru Mungu kwa bahati hii hasa hii ya kaokota noti kubwa ndani ya takribani mwezi mmoja katika kipindi hiki kigumu cha Tanzania ya Magufuli, na pia naomba niwaulize wenzangu juu ya uzoefu wao katika kuokota hela pengine kuna wenye bahati kubwa zaidi ya kuokota minoti barabbarani.

Karibuni tupeana uzoefu na tuelezani kama kuna uhusiano wowote wa kuwapa ombaomba fedha na kuokota hela na vitu vya aina hiyo na pia kama kuna mtu/watu ambao hawajawahi kuokota hela yeyote nao watueleze.
 
Imani ndio humfanya mtu aamini anachoamini..mm sina imani na kuokota hela kuna uhusiano na kutoa sana kwa wasiojiweza...ingekuwa hvyo kina marehem Mengi au Billgate wangekuwa wanaokota hela nyng sana kwa siku#kidding#
 
Habari wadau,

Kwanza nianze kwa kusema hii si mara yangu ya kwanza kuokota hela kama ambayo naamimi hata wewe msemaji huenda umewadia kuokota hela pengine zaidi ya mara moja.

Katika hali ya kawaida(kwani naamini ni kwa wengi), nimekuwa nikiokota hela ndogo ndogo(shilingi 1000,2000,500, n.k) tena katika interval kubwa tu kiasi kwamba nakuwa sikumbuki hata mara ya mwisho niliokoto lini.

Cha ajabu na kinachonifanya hata mimi nishangae na kujiuliza hilo swali hapo juu kwenye heading, ni mimi kuokota noti ya shilingi 10,000 tena mara mbili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Mara ya kwanza ilikuwa ni tarehe za mwanzoni za mwezi wa December ambapo nilikiwa katika matembezi yangu mjini nikaokota noti ya shilingi 10,000 na leo ni mara ya pili nimeokota noti kama hiyo nikiwa katika bar moja.

Leo hii nimekuja katika bar moja ambayo hata jana nilikuwepo.Tofauti na jana, leo hakuna wateja wengi hivyo meza nyingi kwa kiasi fulani ziko tupu na nimekaa pale pale nilikuwa nimekaa jana. Meza moja baada ya meza niliyokaa mini,kulikuwa na watu kama watatu ambao baada ya kupata vinywaji, wakaondoka na kwakweli hata sura sijawakariri .

Baada ya wahusika kuondoka,zilipita kama dakika sita nikajikuta nimegeuza shingo upande wa ile meza waliokuwa wamekaa na kuona noti ya shilingi 10,000 iko chini.Bila kuchelewa, nikainuka faster nikaiokota na hakuna alie-note chochote huku wahusika wakiwa nao wameaondoka na hata sura sijawakariri unless waje kuulizia kama kuna mtu kaokota hela kwenye meza waliokuwa wamekaa(wakija nitawapa).

Halafu kingine cha ajabu, ndani ya dakika kama mbili au tatu baada ya mimi kuokota hiyo hela, akaja muhudumu special anaefagia chini ya meza na kuokota vitu kama tissue akafagia kwenye ile meza iliyo tupu kisha akaja kwenye meza yangu na akaendelea kwenye meza nyingine kiasi kwamba ningechelewa kidogo tu, ile 10,000 angeokota yeye.

Sasa najiuliza,kuokota huku noti kubwa kubwa kama hizi tena ndani ya muda mfupi hivi, ni bahati tu au ni Mungu ananirudishia kile kidogo nachowapa ombaomba mitaani?

Kusema ukweli, mimi nikipita sehemu au nikiwa nimekaa mahali na akapita ombaomba, huwa sisiti kuwapa chochote na nimekuwa nikifanya hivi mara kwa mara na mara ya mwisho nilimpa ombaomba mmoja siku kama tatu hivi zilizopita.

Vile vile, some days back(miezi kama minne iliyopita) nikiwa chuoni( UDSM) mida ya saa moja kasoro jioni,niliokotoa noti za shilingi 1,000 zilizokuwa zimeachana umbali wa hatua kama mbili maeneo ya geti la chuo cha maji huku wanafunzi wakiwa wengi wanaotoka na kuingia chuoni mpaka nikapata wasi wasi wa kuokota noti ya pili ingawa ni wazi ziliangushwa na mtu mmoja akiwa anaetembea.

Kwanza namshukuru Mungu kwa bahati hii hasa hii ya kaokota noti kubwa ndani ya takribani mwezi mmoja katika kipindi hiki kigumu cha Tanzania ya Magufuli, na pia naomba niwaulize wenzangu juu ya uzoefu wao katika kuokota hela pengine kuna wenye bahati kubwa zaidi ya kuokota minoti barabbarani.

Karibuni tupeana uzoefu na tuelezani kama kuna uhusiano wowote wa kuwapa ombaomba fedha na kuokota hela na vitu vya aina hiyo na pia kama kuna mtu/watu ambao hawajawahi kuokota hela yeyote nao watueleze.
UKiokota unainamaje?
Huo ni mtego
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom