ommytk
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 482
- 1,053
Nikampa 10,000 akawa chenji hana ikabidi aniache na maembe yale manne na kiroba chake anaenda kuchukua chenji na kuleta mfuko aisee nimekaa Masaa nawili hajarudi. Nikawauliza majirani pale wanauza vitu wanasema hawamjui. Basi nimeondoka, kiroba nimetupa, nimechukua embe nipo home.
Pia soma: Uzi maalumu wa kupeana njia wanazotumia MATAPELI
Siku hizi ndio wizi wa Dar ulivyo ukimpa hela kubwa anajifanya anaenda kuchange anaondoka mazima, muda mwingine wanakuwa wawili mmoja anabaki anakuwa anauza bidhaa ukimpa hela ajifanya kaenda kuomba change anaondoka mazima ukiwauliza majirani wanakwambia huyu kijana hatumjui amekuja mwenye hii biashara sijui katoka naye wapi katua tu mzigo kamuacha hapa huyu kijana.
Baada ya muda anakuja mwenye mzigo ambaye ni mhusika mkuu majirani zake wakimuuliza vipi huyu mtu uliyemuachia hii biashara yako kaondoka na chenji ya watu alienda kuomba change hajarudi anakana kabisa kwamba yeye hakumuachia mtu yeyote biashara yake ndio kwanza amekuja ili afungue.