Leo nimenunua maembe 3 kwa Sh. 10,000/- bila kupenda

Hili jambo nilifunzwa na mama mmoja hapo Kariakoo sokoni mwaka 1988. Siwezi Mpatia muuzaji hela ili atafute chenji. Atumie yake au aombe kwa wenzake
Shikamoo! kumbe huwa tunajibizana mbovu na baba zetu na mama zetu wakati mwingine hapa JF! mwaka 1988 nilikuwa sijazaliwa.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nimecheka hadi nimekaa chini
 
Wadau Leo nimezidiwa ujanja nimebaki nacheka kweli mjini shule nimemkuta mtu ana maembe dodo mazuri Mbagala stand nikayapenda, nikauliza bei akasema ni sh. 800 na yapo 4 Mimi nilitaka mawili tu....
Heading yako inasomeka kua umenunua maembe matatu kwa elfu kumi bila kupenda,

Halafu unasema Embe moja ni sh.800 na yalikua Maembe 4.

Sasa mkuu ina maana uliacha Embe moja na kuchukua Embe zako 3 kisha ukaondoka?
 
Wadau Leo nimezidiwa ujanja nimebaki nacheka kweli mjini shule nimemkuta mtu ana maembe dodo mazuri Mbagala stand nikayapenda, nikauliza bei akasema ni sh. 800 na yapo 4 Mimi nilitaka mawili tu..
Unaweza kuta kagongwa gari kafa, hayo maembe aliyawekea tego atakayeiba naye anapata madhara so ulipaswa uwaachie wenzake, imekula kwako
 
Wadau Leo nimezidiwa ujanja nimebaki nacheka kweli mjini shule nimemkuta mtu ana maembe dodo mazuri Mbagala stand nikayapenda, nikauliza bei akasema ni sh. 800 na yapo 4 Mimi nilitaka mawili tu...
Siyo mbaya atapata pesa ya daftari na kalamu za wanawe
 
Siku hizi ndio wizi wa Dar ulivyo ukimpa hela kubwa anajifanya anaenda kuchange anaondoka mazima, muda mwingine wanakuwa wawili mmoja anabaki anakuwa anauza bidhaa ukimpa hela ajifanya kaenda kuomba change anaondoka mazima ukiwauliza majirani wanakwambia huyu kijana hatumjui amekuja mwenye hii biashara sijui katoka naye wapi katua tu mzigo kamuacha hapa huyu kijana.

Baada ya muda anakuja mwenye mzigo ambaye ni mhusika mkuu majirani zake wakimuuliza vipi huyu mtu uliyemuachia hii biashara yako kaondoka na chenji ya watu alienda kuomba change hajarudi anakana kabisa kwamba yeye hakumuachia mtu yeyote biashara yake ndio kwanza amekuja ili afungue.
 
Dada yangu aliwahi kumpa bodaboda elfu 10000 akaenda kutafuta chenji na boda yake 🙄🙄🙄. Baada ya muda ndo anashtuka akasepa faster.
 
Mtaa Aggrey pale jioni wanakuja watu wanajifanya mafundi simu ukiwapa simu wanajifanya wanaenda kununua kifaa basi ndio imetoka hiyo harudi tena hadi kesho.
 
Wadau Leo nimezidiwa ujanja nimebaki nacheka kweli mjini shule nimemkuta mtu ana maembe dodo mazuri Mbagala stand nikayapenda, nikauliza bei akasema ni sh. 800 na yapo 4 Mimi nilitaka mawili tu.

Nikampa 10,000 akawa chenji hana ikabidi aniache na maembe Yale manner na kiroba chake anaenda kuchukua chenji na kuleta mfuko aisee nimekaa Masaa nawili hajarudi. Nikawauliza majirani pale wanauza vitu wanasema hawamjui. Basi nimeondoka, kiroba nimetupa, nimechukua embe nipo home
Alipanwa na haja kubwa, alikuwa anakuulizia pale. Analalamika umeondoka na maembe yake. Ungemsubiri tu.

Sent from my SM-A415F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom