Leo nimenunua maembe 3 kwa Sh. 10,000/- bila kupenda

ommytk

Senior Member
Jul 30, 2015
166
500
1610013884750.png
Wadau leo nimezidiwa ujanja nimebaki nacheka kweli mjini shule nimemkuta mtu ana maembe dodo mazuri Mbagala stand nikayapenda, nikauliza bei akasema ni sh. 800 na yapo 4 Mimi nilitaka mawili tu.

Nikampa 10,000 akawa chenji hana ikabidi aniache na maembe yale manne na kiroba chake anaenda kuchukua chenji na kuleta mfuko aisee nimekaa Masaa nawili hajarudi. Nikawauliza majirani pale wanauza vitu wanasema hawamjui. Basi nimeondoka, kiroba nimetupa, nimechukua embe nipo home.

Pia soma: Uzi maalumu wa kupeana njia wanazotumia MATAPELI

Siku hizi ndio wizi wa Dar ulivyo ukimpa hela kubwa anajifanya anaenda kuchange anaondoka mazima, muda mwingine wanakuwa wawili mmoja anabaki anakuwa anauza bidhaa ukimpa hela ajifanya kaenda kuomba change anaondoka mazima ukiwauliza majirani wanakwambia huyu kijana hatumjui amekuja mwenye hii biashara sijui katoka naye wapi katua tu mzigo kamuacha hapa huyu kijana.

Baada ya muda anakuja mwenye mzigo ambaye ni mhusika mkuu majirani zake wakimuuliza vipi huyu mtu uliyemuachia hii biashara yako kaondoka na chenji ya watu alienda kuomba change hajarudi anakana kabisa kwamba yeye hakumuachia mtu yeyote biashara yake ndio kwanza amekuja ili afungue.
 

Luv

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
1,849
2,000
Wadau Leo nimezidiwa ujanja nimebaki nacheka kweli mjini shule nimemkuta mtu ana maembe dodo mazuri mbagala stand nikayapenda nikauliza bei 800 na yapo 4 Mimi nilitaka mawili tu . nikampa 10000 akawa shenji ana ikabidi aniache na maembe Yale manner na kiroba chake anaenda kuchukua chenji na kuleta mfuko aisee nimekaa Masaa nawili ajarudi nawauliza majirani pale wanauza vitu wanasema awamjui basis nimeondoka kiroba nimetupa nimechukua embe nipo home

Pole mkuu
 

Distant Relatives

JF-Expert Member
Nov 21, 2020
214
500
Ni bora mwizi wa namna hii, kuliko yule anakuchukua, kisha anakuweka ndani, mwaka mzima, unateseka, huioni familia yako, unakula hovyo kisha unampa hela anayoitaka ndio anakuachia.

Mwizi wa hivi ni mbaya, sbb anakuibia huku anakupora haki zako za kijamii na kibinadamu, ila huyo mwizi wako yeye anakuibia lakini hakuchukulii haki zako, si unaona time hii uko kwako!
 

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
7,288
2,000
Ni bora mwizi wa namna hii, kuliko yule anakuchukua, kisha anakuweka ndani, mwaka mzima, unateseka, huioni familia yako, unakula hovyo kisha unampa hela anayoitaka ndio anakuachia. Mwizi wa hivi ni mbaya, sbb anakuibia huku anakupora haki zako za kijamii na kibinadamu, ila huyo mwizi wako yeye anakuibia lakini hakuchukulii haki zako, si unaona time hii uko kwako!
Unataka kusemaje kwa mfano?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom