Leo nimelia na nimetokwa machozi kwenye daladala

junky

JF-Expert Member
May 11, 2017
413
976
Leo nilikuwa nimepanda daladala aina ya eicher hapa jijini Dar es salaam kama unavyojuwa jiji letu halikauki kwa foleni..lakini udhia wa foleni haukuonekana sababu dereva wa daladala ile alifungulia muziki wa Mnanda au mchiriku kiukweli Mungu amlipe kila la heri yule dereva

Japo sikulia kama kichwa cha habari kinavyosema lakini nilipata feelings za ajabu sana nilikumbukia enzi ya kitambo maisha tunakua kwenye ujana maisha ya Tandale na mwananyamala kwa manjunju ..kipindi unasikia mlio wa muziki kwa mbali unaufuata na kupata burudani na flash back kibao kwenye mechi za ndondo vibao na vigoma hivi vikipigwa na ukizingatia imepita miaka sikusikia mnanda na sauti za hawa mabingwa.

-7 survivor chini ya Juma mpogo
-Atomic chini ya omary omari
-Jagwa dah hawa ndio the best

Kiukweli yule dereva leo kanikonga nyoyo vilivyo nilivyokaribia kushuka nilimfuata na kumtunza 2000...

Asikuambie mtu mnanda mtamu sana kwanza nyimbo zao zina elimisha, wana mistari kuntu,minanda na vigoma vyao vinatia mzuka na mziki huu haunaga fujo au makelele ...sema siku hizi mziki huu umekufa ...
 
sasa hivi mambp yameharibika wana imba "bakora tatu mtoto kaacha shuleee mara usiku wa manane mtoto anataka umaaa umasiuma kumbe anataka ku**maaaa. sasa ukute mwanao anaimba waweza toka mbio
 
Leo nilikuwa nimepanda daladala aina ya eicher hapa jijini Dar es salaam kama unavyojuwa jiji letu halikauki kwa foleni..lakini udhia wa foleni haukuonekana sababu dereva wa daladala ile alifungulia muziki wa Mnanda au mchiriku kiukweli Mungu amlipe kila la heri yule dereva

Japo sikulia kama kichwa cha habari kinavyosema lakini nilipata feelings za ajabu sana nilikumbukia enzi ya kitambo maisha tunakua kwenye ujana maisha ya Tandale na mwananyamala kwa manjunju ..kipindi unasikia mlio wa muziki kwa mbali unaufuata na kupata burudani na flash back kibao kwenye mechi za ndondo vibao na vigoma hivi vikipigwa na ukizingatia imepita miaka sikusikia mnanda na sauti za hawa mabingwa.

-7 survivor chini ya Juma mpogo
-Atomic chini ya omary omari
-Jagwa dah hawa ndio the best

Kiukweli yule dereva leo kanikonga nyoyo vilivyo nilivyokaribia kushuka nilimfuata na kumtunza 2000...

Asikuambie mtu mnanda mtamu sana kwanza nyimbo zao zina elimisha, wana mistari kuntu,minanda na vigoma vyao vinatia mzuka na mziki huu haunaga fujo au makelele ...sema siku hizi mziki huu umekufa ...

hongera kwa kimbukizi
 
Ila Mnanda enzi zile miaka ya 1990 kule Temeke Mikoroshini acha kabisa, mnanda una raha yake kuusikiliza. Tunatembea kwa miguu kutoka Temeke hadi Kariakoo kupitia Uwanja wa Taifa, acha kabisa
 
Mnanda hatari sana, tulikuwa tunafata mdundo kutoka mitaa ya Mazimbu Barakuda mpaka Kihonda mbele ya mizani.

Mnaporudi bila mziki ndio mnajua kuwa mlitembea umbali mrefu.
Hatari mkuu yaani ukisikia kigoma unafuata sauti inapotokea mnakatiza mikono na wala huhisi umbali mpaka unafiki kwenyewe ..dah noma sana
 
Mkuuu umefanya nivute hisia za hii kitu ya mnanda daaaah. Somtym haya yanachangiwa na Vyuma kukaza brother. Enzi za JK pesa zilikuwa bwerere na hayo mambo tuliweza kuyafuata huko Mwaneromango nafsi ikasuuuzika lkn sasa hollaaaa
 
Back
Top Bottom