Leo Nimejaribu kwa pupa Kusoma kitabu, nimeishia ukurasa wa 3 chali. Shikamooni JF bookworms

Kitabu ulichoanza nacho sio sahihi, kwa kuanza kusoma vitabu kwa mara ya kwanza.

Mimi nina best zangu watatu nimewaambukiza kusoma vitabu, kwa kuwasimamia na kuwapa vitabu kwa mtiririko mzuri. Sasa hv wanapenda sana vitabu.

- Wiki iliyopita nimesoma vitabu vi3 na nimemaliza.
- Kwa siku nasoma vitabu masaa 6 daily
- Kipindi hiki cha corona muda mwingi nipo free zaidi ya masaa 8 kusoma vitabu na nainjoy sana.
- Ukizoea kusoma vitabu, hata kuangalia Tv hupati muda.

Mwanzo mgumu, Hongera kwa kuanza
(welcome to the club)
 
Mkuu

Habari za siku, mimi ni msomaji mzuri wa vitabu vya historia, saikolojia pamoja na motivation.

Sijawahi kusoma novel, vipi unaweza kunitajia novel moja ambayo itanifanya nihamasike kusoma novel nyingi zaidi?

Vitabu nilivyosoma mpaka sasa
1. The history of money cha Jefferson
2. The wealth of Nation cha Adam Smith
3. The History of Catholic Church (mwandishi simkumbuki)
4. Sapiens: A brief history of man cha yuvai halal Noah)
5. Homo Deus: Brief history of tommorow (nipo nakisoma)

View attachment 1452858

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko vizuri,,, kimeshiba kweli kweli page za kutosha.
 
Hiki hata Kama kina siri ya kuishi milele sisomii...
khaaaa, sasa hapa utamaliza lini? ukisahau si hasara?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hicho cha The wealth of nation kinapage zaidi ya elfu moja, hicho cha history of catholic page zaidi ya elfu 2, History of money kina page 250 hivi,

Kuvisoma hivyo vitabu inabidi uwe umehamasika kujua jambo fulani ndio utavisoma vizuri.

Mfano kuna siku nilihamasika kujua pesa ilianzaje anzaje ??? Basi nikaamua mtandaoni nikasaka kitabu nikaanza kuchimbua nilijikuta nakesha kwa utamu wa niliyoyasoma. Kupitia humo nikajikuta nataka kujua ukatoliki ulianzaje maana kwenye historia ya pesa utawala wa ki roma umetajwa sana na ndio uliozaa ukatoliki.

Kiufupi inabidi uangalie unataka kujifunza nini ndio uchague kitabu kinacho kufa

Mimi ninavyo vingi tu. Vingine nimedhulumiwa na watu, soft copy nnazo kama 800 vyote nimesoma,

Ingia mtandaoni tafuta vitabu vya OSHO anza na hivyo kwanza vitakufaa

JPEG_20200517_211414_2038132069438184254.jpg
JPEG_20200517_211445_4205986898255341414.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitabu ulichoanza nacho sio sahihi, kwa kuanza kusoma vitabu kwa mara ya kwanza.

Mimi nina best zangu watatu nimewaambukiza kusoma vitabu, kwa kuwasimamia na kuwapa vitabu kwa mtiririko mzuri. Sasa hv wanapenda sana vitabu.

- Wiki iliyopita nimesoma vitabu vi3 na nimemaliza.
- Kwa siku nasoma vitabu masaa 6 daily
- Kipindi hiki cha corona muda mwingi nipo free zaidi ya masaa 8 kusoma vitabu na nainjoy sana.
- Ukizoea kusoma vitabu, hata kuangalia Tv hupati muda.

Mwanzo mgumu, Hongera kwa kuanza
(welcome to the club)
Kumbe ndio maana umepotea sana JF.
 
Mkuu Pantomath , kwanza nikupe hongera kwa kuwa na "desire" na uthubutu wa kusoma vitabu. Hakika hayo uliyopitia ni mwanzo tu, ninaamini utakuwa msomaji mzuri siku za mbeleni. Kitu cha msingi ni kujaribu tena na tena.
Nimekuwekea nakala ya kitabu ambacho ni kizuri kwa wanaoanza kusoma vitabu (beginners). Ninaamini kitakuwa msaada kwako.
 

Attachments

  • 1. MAAJABU YA VITABU-1.pdf
    694.5 KB · Views: 24
Mkuu Pantomath , kwanza nikupe hongera kwa kuwa na "desire" na uthubutu wa kusoma vitabu. Hakika hayo uliyopitia ni mwanzo tu, ninaamini utakuwa msomaji mzuri siku za mbeleni. Kitu cha msingi ni kujaribu tena na tena.
Nimekuwekea nakala ya kitabu ambacho ni kizuri kwa wanaoanza kusoma vitabu (beginners). Ninaamini kitakuwa msaada kwako.
Kaka nashukuru sanaa, Naahidi kukisoma hiki na nitaleta mrejesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina mashaka kama mtoa mada atamaliza kusoma hii.

Akiweka nia ataweza tuu. Kila jambo mtu analolifanya ni kuwa amelipa umuhimu. Hivyo kama akiamua kuupa umuhimu KUSOMA basi atajikuta anasoma tuu na anamaliza. Kisha atakuja hatua ya pili ya nisome nini na nini nisisome hapo ndo atagundua kuwa muda hautoshi.
 
Kusoma ni kipaji afadhali mimi niliepiga hadi darasa la saba nikastaaafu kusoma


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
😃😃Aisee vitabu 9 ndani ya siku 1!!, kwanza ulitakiwa uwe na ratiba ya kusoma vitabu labda saa 2 au 3 zinatosha kwa siku 5 ndani ya wiki, alafu usisome kitabu ili ukimalize haraka bali unasoma ili uelimike na uinjoy kusoma na usilazimishe, ndani ya miezi 6 huwa nasoma vitabu 4 au 5 tu vinatosha.

Alafu ukitaka uinjoy zaidi kusoma vitabu, basi wakati unasoma usisahau korosho/karanga au popcorn pembeni pamoja na maji ya kunywa, lazima uzoee na utajisahau kama upo duniani😁.
 
Mkuu Pantomath kwanza hongera sana kwa kuanza kujisomea. Nitakwambia machache labda yanaweza kukusaidia:

Katika usomaji vitabu hakikisha unatafuta genre ya vitabu ambavyo wewe mwenyewe unapendelea sio kwa sababu fulani kasema kitabu fulani kizuri. Mfano, mimi siwezi kabisa kusoma motivational "how to" books hata kisifiwe vipi. Vitabu kama rich dad, poor dad au think and grow rich siviwezi kabisa.

Pili, kusoma vitabu kuna elimisha, kufurahisha na kupanua imagination. Katika kuelimisha sio lazima utoke na ideas za kupiga pesa ndefu au world-problem solving skills katika usomaji wako, unaweza toka na misamiati miwili tu au kuboresha uandishi wako hizo pia ni faida. Nasisitiza hili sababu wengi wanakata tamaa ya kuendelea kusoma vitabu mara tu wakimaliza kusoma kitabu kimoja na kuona hawajaongeza kitu kama walivyotarajia.

Maarifa yapo kwenye vitabu japo ni usemi wa kweli ila sio necessarily kwenye ulimwengu wa leo. Huo usemi ulikua applicable zaidi miaka ya nyuma wakati technolojia bado duni. Maarifa sasa yapo kila kona hasa mtandaoni; youtube, coursera nk. Binafsi natumia kusoma vitabu just for relaxation.

Aidha usomaji vitabu sio mashindano, sio lazima na wewe umalize kitabu kila wiki. Soma at your own pace, hata kama kitabu kimoja kitakuchukua mwaka ni wewe. Usifanye mashindano na kina Zito wanaodai wamesoma 100 books in a year wanataka sifa tu. Kadhalika usipoteze muda kusoma kitabu ambacho unaona hukielewi, haijalishi upo page ya kwanza au ya mia kama unaona hakikuvutii weka chini chukua kingine, sio lazima kila kitabu ukimalize.

Currently, nasoma My life, my purpose cha Rais Mkapa, it's one of my favorite books so far, needless to say, I like autobiography/memoirs and history books.
 
Back
Top Bottom