Leo nimeenda kwenye kikao cha wazazi darasa la Saba, hakuna mzazi hata moja kaja na gari. Kuna kitu nimejifunza

Leo niliitwa shuleni kwenda kwenye kikao cha mjukuu wangu yupo darasa la Saba anatarajia kufanya mtihani mwaka huu. Nikachukua baskeli yangu na kwenda kwenye kikao shuleni. Nimefika nimechelewa sana ila kuna kitu nikawa najiuliza baada kufika pale nje, mbona hakuna hata gari moja ya mzazi na pikipiki baskeli na waenda kwa miguu.

Hii ilinipa mawazo na kuwaza mambo tofauti hata nilipoingia ndani wazazi tuliopo ni mavazi yetu tu yanakupa jibu sisi wazazi namna gani mungu ibariki Tanzania wabariki na watu wake
Hii story yako inanikumbusha enzi za utumwa, nikianza kazi kwenye kampuni haina hata parking za magari ya staff nilikuwa napata mashaka sana kwamba hapa ni kambi ya malofa.
 
Baadaye muwashangae watoto wenu kukosa koneksheni.!
Wachache watakuelewa, hiki kitu huwa nabishana sana na wenzangu ofisini! Wanaweza wakafurahi now ila tatizo watoto watakutana nalo huko mbeleni, yanayonikuta mimi sitaki vijana wakutane nayo!
 
Ni muhimu sana kuwa na gari hata kama huliendeshi kila siku.

Gari lina umuhimu sana,hasa unapotaka kutoka usiku mfano kama ukiuguliwa au kutoka wakati wa mvua.

Hata uwe na pesa nyingi kiasi gani kama hauna gari wewe ni masikini tu,
Sio kweli,watu wanatumia bolt na maisha yanaenda
 
Shikamoo babu pole sana
Hiyo ni shule ya kata,Hebu nenda shule za english medium utaona tofauti
Pia wanaume wengi wanajua vikao vya std 7 hakuna pombe ndio maana hawaji
hebu nenda shule za english medium kama feza halafu lete mrejesho
 
Back
Top Bottom