Leo nikijibiwa haya maswali yangu muhimu mawili tu nitakuwa ni mwenye furaha na nitazidi kuipenda JF

Nina mashaka na hila swal la pili linaweza kuwa ni hapa hapa bongo na anayeongelewa hapo ni lissu na hao unaozuga makomando sio bali ni hawa wasiojukikana ambao yanawakuta ya kuwakuta recently
 
Kwahiyo kumbe wale wote wanaouwawa na Mashirika ya Kijajusi ya Marekani, Urusi na Israel huwa wanakuwa na Ugomvi binafsi nao? Ndiyo maana naipenda nchi yangu ya Tanzania kwani yenyewe haina huu Ukatili kwani Watanzania Siku zote tunapendana, hatugombani na ni Watu wa Amani daima.
Pole kwa haya maneno yako unayoyaamini
 
Swali # 1.

Je, ni kweli kwamba wale Watu ambao huwa wanakuwa ni Waajiriwa wa Idara Nyeti hasa za CIA au KGB au MOSSAD ( sijajua wa Tanzania ) huwa wakipewa Jukumu la ama Kumuua au Kumjeruhi Mtu iwe ama kwa Chuki zao tu Kwake au kwa Maslahi mapana ya Marekani, Urusi na Israel baadae na Wao huuliwa ili Kupoteza Ushahidi?

Swali # 2.

Je, ni kweli kwamba Makomandoo hasa wa Marekani au Urusi au Israel ( sijajua wa Tanzania ) huwa wakifikisha Umri wa Miaka 50 huwa Wanauliwa ili baadae wasije wakawa wanatumika na ama Maadui wa ndani au wa nje wa nchi?

Kwa mfano kuna Mtu yupo Urusi ameniambia ( japo najilazimisha Kumuamini ) kwamba ana Rafiki yake Mmoja hivi wa Kirusi ila ni Mwanasiasa huko na ni Mpinzani mkubwa tu wa Rais Putin kuna Watu wa Idara Nyeti ya Urusi walitumwa kwenda Kumuua lakini labda kwa Mapenzi yake Mwenyezi Mungu pamoja na kwamba walimjeruhi vibaya kiasi cha Kumsikitisha kila Mrusi ila hakufa na hadi hivi leo yupo Hai japo anaeendelea kupatiwa Matibabu.

Ameniambia kuwa wale Watu wote wa Idara Nyeti ya nchini Urusi waliopewa hilo Jukumu la Kumuua baada ya Kushindwa Kulitekeleza hivi sasa wote wameuliwa kiasi kwamba hata Maiti zao hazijulikani zimezikwa wapi huko nchini Urusi.


Najua JF kuna Wataalam zaidi hivyo hapa mtanisaidia nami pia kuweza kupata Maarifa zaidi japo nashukuru mno Mungu kuwa haya Matukio sijawahi kabisa kuyasikia hapa Tanzania au Uganda au Rwanda achilia mbali Kenya na Burundi na siombei pia haya ya huko Marekani, Urusi na Israel yafanyike au yatokee huku Kwetu.

Karibuni.
kwa swali la kwanza, kuna ukweli ndani yake CIA wana tabia hiyo kwa mission ambazo ni za hatari na ni za usiri mkubwa. HITMAN anapotumwa huwa kuna tail nyuma .ili akimaliza kazi yake naye anamalizwa na hiyo tail huwa haijui chochote kinachoendelea au inalishwa uongo isipokuwa kutekeleza order ya kuua tu.
kwa #2 sina uhakika kabisa
 
Back
Top Bottom